Habari zenu
Nilikua naomba mtu aliyewahi kupitia kipindi cha talaka na mwenza wake hasa wanawake..tupeane experience kipindi karibu na talaka, wakati wa talaka yenyewe na maisha baada ya talaka..
Ilikuchukua muda gani ku move on?
Kipindi baada ya talaka ulifanyaje maisha yaendelee kama kawaida?
Na kabla ya talaka ilikuwaje
Hii itawahusu waliopitia talaka wakiwa wameshapata watt au ambao hawakubahatika kuzaa na wenza wao wakatalikiana wao kama wao
Nahitaji sana mnitie moyo mana nimechoka sana ndugu zangu ni majuto baada ya majuto..nimechoka sana sana lkn kama mnavyojua pamoja na yote talaka ina ugumu wake kiasi fulani ila bado nahitaji sana ishauri wenu
Tafadhali msitumie matusi nimewaomba kwa heshima ndugu zangu[emoji122]
Mimi nishaipitia hiyo hatua. Kwa hiyo nitachokiongelea nina tajiriba nacho moja kwa moja.
Muomba talaka ni nani kati yenu? Mume au mke?
Kwa kweli talaka ni ngumu hususan huku kwenye hii jamii yetu. Sisi hatujazoea watu kutalikiana. Hivyo machoni mwa watu huonekana kama ni jambo geni au la ajabu hivi.
Kwa uzoefu wangu, talaka huwa ni rahisi zaidi kukabiliana nayo kwa yule mwombaji.
Na kama wote wawili mmeridhia ndo inakuwa bora zaidi.
Pia, ili kuwepo na amani, ni vyema kama hiyo talaka itakuwa ‘uncontested’. Yaani, hakuna kubishana bishana kuhusu sijui mali, kupingana kuhusu custody ya watoto, na mambo mengine kama hayo.
Kuhusu maumivu na hisia zingine ziambatanazo na kuumizwa kimapenzi, hiyo ni kawaida. Ni suala la kiuasili tu.
Hivyo kubali kuwa kuna nyakati utakuwa unasikia maumivu. Usijilazimishe kutokuumia. Acha asili ichukue mkondo wake. Na usirukie mahusiano mapya kwa matumaini ya kwamba yatakusaidia kusahau yaliyotokea.
Na baada ya muda utakuja kuizoea hiyo hali mpya, maumivu nayo yatapungua, na maisha yatasonga mbele.
Muda huponya kweli. Take it from me!
Good luck!