Kipindi cha Morning Magic cha Magic FM

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
368
425
Hiki kipindi huwa napenda kukisikiliza sana., kina watangazaji watatu ambao ni Salum Mkambala, Mary Edward na Orest Kawau na huwa wanamualika Mwandishi wa Habari Kibwana Dachi.
Kinachonikera katika kipindi hiki:-
Hawa watangazaji hasa Mary Edward na Orest Kawau huwa ni wabishi sana na wanapenda kujifanya kwamba wanajua kila kitu., muda mwingine wanaongea vitu ambavyo hawana uhakika navyo na kupotosha umma wa wasikilizaji.
Kibwana Dachi huwa anajitahidi sana kudadavua mambo vizuri na kwa weredi kiasi chake., ila huyu Bwana Orest Kawau anapenda sana kubisha na kujifanya anajua hata vitu ambavyo havijui pamoja na mwenzake Bibiye Mary Edward.
Mnachitakiwa kujua nyinyi ni watangazi mnaosikilizwa na maelfu ya watu wenye umri, taaluma na ujuzi mbali mbali. Mnapoongea vitu jitahidini kuongea vitu ambavyo mna uhakika navyo msipotoshe wasikilizaji., mnapoongea mambo ya uongo na msiyokuwa na uhakika nayo sisi tunaojua tunawasikiliza na kuwadharau.

Kipindi ni kizuri sana ila hizo kasoro chache zinawaharibia.
 
kipindi kizr, ila tatzo moja hajapangilia mda wa matangazo, mwingiliano wakati wa kuongea, na mpangilia wa uchambuzi, wakifanyia kazi hayo huenda kikawa kipindi bora kabisa cha asb kuliko vipindi vyote vya radio tz,

hayo matatzo nikiyoyataja yanakifanya kipindi kuwa kama cha wavuta .... ila wakirekebisha asee wako vzr sana
 
Asee kweli mkuu hao wawili ulowataja wana huo ugonjwa japo huyo orest au marry mmoja anaonekana ndiye kama mkuu ktk kipindi so wakikaa kwenye postmortem zao watajirekebisha.
 
Dachi yuko safi sana na anaonekana ana hekima mno.

Ukiona ujuaji mahali jua ni isharaya elimu ndogo au kupenda attention.
Leo walikuwa na Mzee mmoja anayejua hesabu, mwishoni orest kama kawaida akasema neno payi ni kikokotozi, Mzee akamwambia siyo kikokotozi ni dhana, sasa kwa hali hii ya kutoelewa unaweza kuwa n shida.
 
kipindi kizr, ila tatzo moja hajapangilia mda wa matangazo, mwingiliano wakati wa kuongea, na mpangilia wa uchambuzi, wakifanyia kazi hayo huenda kikawa kipindi bora kabisa cha asb kuliko vipindi vyote vya radio tz,

hayo matatzo nikiyoyataja yanakifanya kipindi kuwa kama cha wavuta .... ila wakirekebisha asee wako vzr sana
Kweli kabisa Mkuu., wakirekebisha kasoro zao kitakuwa kipindi bora kabisa cha Asubuhi
 
Kweli kabisa Mkuu., wakirekebisha kasoro zao kitakuwa kipindi bora kabisa cha Asubuhi
Yap umenena vema sana.
Zamani kile kipindi cha Radio One cha kumepambazuka kilikua kinabamba sana kabla ya RFA haijaja na Watanzania Tuzungumze Magazeti baadae wakaendekeza ujinga ujinga kile kipindi chao cha magazeti kimepoteza umaarufu kabisa.

Sasa naona Magic Fm kipindi chao cha asubuhi nacho kinakuja kwa kasi sana lakini kuna baadhi ya watangazaji kama Marry na Bwana Kawau wanaanza kukiharibu kwa kupoteza ile dhana ya wao kuwa waongoza kipindi na wachokonoaji wa mada ili wataalamu wazungumze badala yao wamekuwa wataalamu wao, wazungumzaji wao kila kitu wao.

Ningewaomba hawa jamaa wajifunze kwa mtangazaji wa Channel ten Bwana Tom Chilala katika kipindi chake cha Mada moto au mzee Makwaia, anatupia maswali ya anachonokozi kitu halafu anakaa pembeni mtangazaji unatiririka.
Ila kwa kweli Magic Fm kipindi chenu kizuri sana
 
Kipindi kizuri kizuri ila Kawau anakiharibu. Anajifanya anaajua kuliko wenzie. Na pia anajifanya anajua sana kingereza kumbe siyo kabisa. Hata usomaji wa habari Mary na Kawau hawajui, wanakuwa kama wana kigugumizi. Mkambala anasoma fluently ila mara nyingi sauti yake nzito huwa haisikiki vizuri, huwa kama yuko mbali na maiki.

Waache kuingiliana, wajaribu kuongea mmoja mmoja, kwa zamu. Kuwa kiongozi wa kipindi kusimfanye Kawau kuwa anajua kila kitu kuliko wenzie.
 
Asee kweli mkuu hao wawili ulowataja wana huo ugonjwa japo huyo orest au marry mmoja anaonekana ndiye kama mkuu ktk kipindi so wakikaa kwenye postmortem zao watajirekebisha.
Orest ndiye MOD wao, ila kweli kuna wakati wanachemka hasa Mary
 
Hiki kipindi lazima asubuhi nikisikilize huku Ileje kupitia kisumbuzi cha Azam .

Kiko poa sana. !
 
Hv huyu kibwana dachi n nan au ana elimu gan nmejarbu kumfuatilia nmehc atakuwa co MTU wakawida maana anajua vtu vngi lile jamaa halafu haogopagi katk speech zake
Hata sijui mkuu,jamaa yuko vizuri sana kichwani.
Kiukweli hata mimi natamani sana kufahamu kuhusu hayo.

Ila watu wa hivyo wapo mkuu,mwenyewe nina jembe langu kama huyo Kibwana,hakuna kitu ambacho hakijui!
 
...nawakubali sana hawa wadau, napenda staili yao ya pekee sana. namkubali sana kawau na mary, kibwana dachi hayuko makini na kipaza sauti, mkambala mara kadhaa huwa anakurupuka ila wakimpanga huwa anakuja vizuri na hoja zenye akili. nakumbuka mara moja mpaka kibwana dachi akamsifia "sikuizi kijana uko vizuri". kwa ujumla mimi naona mapungufu ni machache na yanarekebika. cha msingi wajitahidi kuwa na hoja ngumu na wazidadavue pasi na wogaa watafanikiwa kuwa watangazaji booora kuliko wote(hasa wahuni wa mawingu)....
 
Back
Top Bottom