Kipindi cha Kampeni Kinawadia - Neema Inafunuliwa kwa Muda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi cha Kampeni Kinawadia - Neema Inafunuliwa kwa Muda

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ELNIN0, Jul 16, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Wananchi wenzangu kipindi cha Kampeni kimefika tena - Kipindi cha ulaji , Neema ya muda inafunuliwa
  Ni kipindi ambacho wananchi mtaonekana ni lulu, mtawaona hao waheshimiwa na suti zao wakiwapigia magoti wakitaka kura ya kuwawakirisha mjengoni. Ni kipindi ambacho ukata utapungua, hela za kampeni zitamwagika hovyo hovyo, hiki kipindi ni cha kuchuma na kusahau matatizo ya miaka 5 iliyopita kwa muda tu.

  Nachowashauri watanzania wenzangu, fikirieni kwa kina kwamba bila kuwa na bunge ambalo nusu ni wabunge wa utawala na nusu ni (opposition) wapinzani basi tusahauni kupata uwakilishi mzuri bungeni, mtakubaliana na mimi hoja nzuri tu zilikwama kupita sababu zimetolewa na wapinzani, na wapinzani ni wachache wakati wa kupigia kura hizo hoja.

  Kipidi hiki mimi nakiita kipindi cha Neema kufunuliwa, Wajanja (Wapiga debe) watanufaika sana maana watafanya kazi ya udalali - kuchukua mafungu ya kapeni na kuja kuwagawia ninyi wananchi, kumbukeni hela hizi huwa hazina risti ni kuzitafuna kwa kwenda mbele zikipita mbele yako.

  Mifano mizuri tu imeshaanza kuonekana, wasanii sasa hivi ni lulu kipindi hiki wamepanda chati hadi kuitwa kwenye mikutano ya wakubwa – na wao kwa werevu wao wameshahau vilio vyao vyote na wanakubali sasa kuingia kwenye contracts za muda mfupi tu za kupiga madebe ya vyama.

  Kumbukeni Kipindi hiki ni kifupi na hizi hela za kampeni haziwezi kabisa kubadilisha maisha yenu, Ushauri wangu, pesa hizi zikipita mbele yako wewe zilambe maana hazina risti wala ushahidi lakini lakini kumbuka tarehe 31 October ufanye uamuzi kwa busara kwa maslahi ya taifa lako na si vinginevyo.

  Nawatakia maandalizi mema ya uchaguzi mkuu - kumbukeni kura yako ni muhimu sana kwako wewe binafsi, kwa mustakabali wa taifa lako, ukoo wako, familia yako hasa watoto wako waje kuwa na future nzuri.
   
Loading...