Kipindi cha dk 45 itv ni cha mawaziri wale wale na viongozi wa ccm pekee........?

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...Hakuna anayeweza kupinga kuwa kipindi cha DK 45 kinachorushwa na ITV chini ya S.Semunyu kama mtayarishaji na mtangazaji kilivuta usikivu na hisia za watu sana wakati kinaanza.Na hii inatokana na umahiri wa mtangazaji kuwahoji maswali wageni wake pale studio.Tangu kimeanza hiki kipindi ni kama kina mwaka mmoja na miezi kadhaa hivi,lakini kinachosikitisha kila siku tunapata wageni walewale tena kwa kurudia zaidi ya mara moja.Hii haitoi uwanja mpana wa kupata maoni kutoka pande mbalimbali za uongozi.

...Mbaya zaidi ni bora kama mtayarishaji wa hiki kipindi angekuwa anawaalika watu tofauti tofauti toka huko CCM,lakini cha kushangaza sasa ameanza kurudia kuwaita watu aliokwisha waalika muda mfupi uliopita.Alianza Wasira na sasa Chami...sidhani kama kwa mwendo huu hiki kipindi kitaendelea kujijengea heshima,nahisi kitaanza kupiromoka kwa kasi sana.Kwanini hataki kuwaalika watu toka upande wa pili,toka vyama vya upinzani au watu wengine na sio kurudia watu wale wale tena wengine wameanza hata kutoka kwenye mawazo ya watanzania na hawataki kuwasikiliza.

...Hali hii inaweza kuchukuliwa kama ilikuwa ni janja ya huyu jamaa kuanzisha kipindi kwasababu ya kulinda maslahi ya watu fulani,na kwa kweli ifahamike wazi kuwa kwa sasa waandishi wengi wa habari wameanza kukosa weledi wanafanya mambo kwa maslahi ya kundi fulani la watu.

Nawasilisha!!
 
Aiseee mie naona mawaziri tu na viongozi wa ccm

1.Nahodha
2.Sitta
3.Wasira
4.Sumaye
5.Nyarando
6.Cyril
7.Nundu
8.............
 
Una matatizo na hoja au sura za wageni waalikwa? Acha wivu wa ukewenza,
 
ila ndugu yamgu unamoyo,hadi sasa bado wakifatilia!!
mie nilivyoona ana-anza round,nikasepa.hadi sasa najua km kipo nikisoma hapa jf.
siku akibadirika tu na kuanza kudili na magamba daily narudi
 
ila ndugu yangu unamoyo,hadi sasa bado wakifatilia!!
mie nilivyoona ana-anza round,nikasepa.hadi sasa najua km kipo nikisoma hapa jf.
siku akibadirika tu na kuacha kudili na magamba daily,narudi
 
ila ndugu yamgu unamoyo,hadi sasa bado wakifatilia!!
mie nilivyoona ana-anza round,nikasepa.hadi sasa najua km kipo nikisoma hapa jf.
siku akibadirika tu na kuanza kudili na magamba daily narudi

iyo ID yako mkuu...Jobe Ayubu "kwasakwasa" ilikuwa bonge ya beki ya Yanga baadae Reli ya moro..alikuwa ni noma kwa kupanda na kushuka,utamtaka ubaya.
 
ila ndugu yangu unamoyo,hadi sasa bado wakifatilia!!
mie nilivyoona ana-anza round,nikasepa.hadi sasa najua km kipo nikisoma hapa jf.
siku akibadirika tu na kuacha kudili na magamba daily,narudi
Duh! Jina lako limenikumbusha sana beki nguli wa Lipuli ya iringa miaka hiyo aitwaye Jobe Ayub Kwasakwasa!!!!
 
Hiki kipindi ni cha kiupendeleo jamani hivi kwanini wasiwahoji hata majembe kama lema, heche ,slaa hata siku moja kuliko hao magamba daily, jamani kwa yeyote mwenye email ya itv aiweke hapa mi niwape madongo yao kwani wanamageuzi 2shachoka kuona upumbafu unaendelea ktk vyombo vya habari au wanataka tusiwe tunaangalia chanel zao,! Eboooooooooooooooooo........!!!
 
Back
Top Bottom