Kipima Joto ITV - Matusi ya bungeni

Kipima Joto ITV - Matusi ya bungeni

Chanzo kikuu ni kukiukwa kwa maadili kwa viongozi wetu.

Watu wamepata madaraka kwa rushwa, ambayo ni kukiuka maadili, tutegemee nini? Matusi yanathibitisha hilo.

Spika asilaumiwe, spika analinda maslahi yake pia.
 
Bunge ni sehemu tukufu.

Haya yanayotokea yanaondoka utukufu wa bunge.

Kiti cha spika hakitendi haki ndio maana hakuna amani.

Katiba mpya, spika asitoke kwenye chama chochote na awe ni mwanasheria.
 
Baraka Molel

Kwa mujibu wa kanuni na sheria za bunge, mtu anayechaguliwa bungeni anawakilisha wananchi. Bunge letu watu hawana maadili ya uongozi. Tungehakikisha kuwa watu tunaowachagua wana maadili ya uongozi.

Adhabu ziwa kubwa sio kutoa mtu nje tu.
 
Michael Aweda - Chadema

Amani ni tunda la haki. Haki ikikosekana amani itatoweka

Kiti cha spika kimeyumba hakitendi haki.

Wako waliotolewa bungeni kwa kuomba mwongozo mara nyingi, wanaoporomosha matusi mazito wameachwa.

Kila dakika ya bungeni ni gharama kubwa ya walipa kodi, tujionee pumba na mchele na tutoe maamuzi 2015.
 
Kipimajoto hakikidhi matakw ya wengi kinatke jipanuke ttx wanaoenda ni wale wle viherehere
 
Naona wachangiaji wengine maneno yao wameyatoa humu jf.....
 
Mwanaharakati.

Spika ameingiza propaganda bungeni.

Kuna presha ya uchaguzi 2015, kuna chama kinaona kimekaliwa vibaya na hivyo ni kucheza rafu.

Waziri mkuu anatoa hotuba muda wote anasema wapinzani tu, amepuuzia kero za wananchi.
 
kuna kilaza anajidai kuwa alianza siasa akiwa na miaka tisa kwa hiyo anayo siri ya siasa.halafu akaleta reference ya ndugai kuwa wabunge wote ni marafiki.halafu akamalia watu waombe Mungu awajalie maisha bora na sikusubiri wabunge.sijui kaenda fanya nini km haoni haja wala wajibu kwa mazingira yanayomzunguka..hizi ni junks zinayokua km mwigulu.
 
Mabunge yote ya vyama vingi ni yenye mgongano.

Wale wanaoona wanaonewa na kiti cha spika wajijengee heshima kwa kuonyesha uvumilivu.
 
Karibu 90% ya wachangiaji wameonyesha kuto kuridhishwa na mwenendo wa kiti cha spika, katika wote walio changia wameonyesha kuridhika na namna upinzani unavyo ibana serikali, na katika wengi walio changia karibu 99% ni vijana wanaotaka mabadaliko na wengi wana sisitiza kuitumia vizuri nafasi hiyo 2015.

Habari mbaya ni kwamba, kama vijana ndio wengi kitakwimu, basi chama makini hakiwezi kuwekeza kwa wazee.
 
Back
Top Bottom