Kipima Joto ITV - Matusi ya bungeni

Wananchi tujilaumu machaguo wetu.

Wabunge watangulize utaifa. wafanye kazi kwa ajili ya wananchi.
 
Issa William Nyanda

Inasikitisha na inahudhunisha mwenendo wa bunge.

Wabunge wamwogope Mungu wataepuka tabia zinazokera. Wamesahau majukumu yao, kutunga sheria, Kusimamia sheria na kukosoa serikali pale imekosea.

Wabunge waruhusiwe kukosoa pale penye ukweli, lakini kupongeza pale mazuri yaliyopo.

huyu amesema hajawai kuona wabunge wa upinzani wakiipongeza serikali.!!
 
Deus Kibamba

Anashukuru kwa michango.

Bunge linaendeshwa kwa kukiuka taratibu sheria na kanuni.

Sehemu kubwa ya kuvunja sheria iko wazi lakini wanafumbia macho licha ya spika kuwa na wasaidizi.

Wanakiuka kuhusu kumzungumza mtu yeyote ambaye hana nafasi ya kujibu. Spika alipaswa kuwa anarejea hayo.

Haifai spika kuanza kutoa watu nje wakati waliotoa MATUSI MAKUBWA wamo ndani.

Bunge letu linakaribia bunge la Somalia ambapo amani huvunjika kwa wepesi ndani.

Kuna mambo ambayo wabunge wangepaswa kuyafanya hawafanyi.

Kudai mikataba na kuijadili. Gesi, madini, nk wadai mikataba wajadili. Hii ni kazi yao ya 5 kwa mujibu wa ibara ya 63 ya katiba yetu.

Kuna wabunge ambao mchango wao ni KUDADADEKI.

Matumizi ya nguvu isiyo lazima si vizuri. Tujiepushe kutumia polisi bali taratibu zetu za kawaida.

Kama tunaandika katiba mpya lakini haya yaliyopo hatuyatekelezi tunapoteza muda.
 
Kuna mazuri bado yapo japo kuna kejeli na vijembe.

Kuna upendeleo wa utekelezaji wa kanuni. tusi la nguoni linavumiliwa, kuomba mwongozo kunakuwa ni kosa na mtu anapewa adhabu, tena kubwa.

Huwezi kuvuna miwa kwenye shamba la mihogo.

Watanzania tumepanda mihogo, tuvumilie tu. Kuna mbunge alitoa matusi Arumeru hajachukuliwa hatua. Waziri aliwaita wananchi wa Mtwara wahuni hakuna hatua. Mbunge mwingine alipigana Dodoma hakuna hatua zilizochukuliwa.
 
Anna Maria Chuo cha Ardhi.

Hatukubaliani na mwenendo wa bunge.

Wabunge wameaminiwa na wananchi na wote wana lengo moja. Lengo hilo linaweza kufikiwa kwa njia mbalimbali. Tuvumiliane pale tunapochangia. Tuongeze ubora wa hoja, na si jazba.
 
Lawi Nyanda.

Tumeonewa sana, tumepuuzwa sana tumenyanyaswa sana, na unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe.

wawakilishi wetu wametusaliti, wanatulia kodi yetu, wanatuibia. Kama wameshindwa kazi watoke wapo watu ambao wanauwezo.
 
Wabunge wanapaswa kutoa maoni na kufuatilia kuwa serikali inatekeleza.

Spika hafanyi kazi yake vizuri, ana upendeleo.

Mfumo wetu ni mbaya. Mbunge ni Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa ambaye ni mteuliwa wa raisi na hivyo anakuwa mwakilishi wa mihimili miwili.
 
kila kitu kina historia, ccm walimwaga Ugali sasa M4C tunatapanya mboga. CCM na spika wamekuwa na upendeleo sana juu ya serikali ya chama cha ccm hata km wanaiba live! Kwa upendeleo wa wazi toka mwanzo, upinzani umelalamika sana lkn spika anaendeleza malavidavi na ccm. Ndiyo hivyo sasa tunavuna mabua sasa
 
Juma - Chuo cha Ardhi.

Mwanasiasa anapaswa kuwa mtu anayeongea ili avute watu.

Kiti cha spika kitekeleze wajibu wake.

Wananchi tuwakatae wabunge ambao wanaenda bungeni kutukana. Kuchangia hoja wabunge watuwakilishe wananche.
 
Samuel Chasi

Walio na macho hawana madaraka na walio na madaraka hawana macho.

Bunge limekaa kishabiki zaidi. Kwa nini bunge la Samuel Sitta lilienda vizuri?

Watanzania tumeona, na tuwatose watu ambao hawatetei watu, bali kejeli
 
Prosper Kigaye

Mbunge anayesema hii kazi ya kutukana niachie mimi. Huyu amelewa madaraka na ametusaliti wananchi. Mchangia amelia kashindwa kumaliza.
 
Mtondo

Wanasiasa wamekumbwa na Political Schizophernia.

Wabunge wavumiliane katika hoja. Hoja inaposhindwa kuwa na mashiko waweke vema
 
Zakaria - Chuo cha Ardhi

Haya mambo yametoka kwenye jamii. Matusi yametoka huku kwenye jamii, na ndio yamefika mpaka kwenye bunge.

Watu wameporomoka kimaadili kwa kuwa wamekata tamaa.

Spika kiti ni kikubwa kinahitaji busara kubwa, ajue kuwa yeye anasimamia muhimili na aupe nafasi muhimil wake ufanye kazi.

Bunge limekuwa katika vita vya siasa. Wabunge wajue kuwa bunge si lao ni la wananchi.
 
Kiti kinayumba! Wabunge wa CCM hawajielewi! Huwezi kujua nani Mbunge nani waziri! Wabunge wote wa CCM ndani ya Bunge ni kama Kambale! wote wanandevu! Wote wanaropoka!
 
Ernest Nyoni

Hivi mmoja akianza matusi ni lazima wengine watoe matusi.

Wabunge ambao hawana hoja za msingi wanapopata nafasi za kejeli ndio wanataka wajitangaze, lakini wanajitangaza kwa aibu.

Wabunge hawasomi na hawana point za kuchangia kwa hiyo wanaongea upuuzi.

Wananchi tunaona, tuwakatae wabunge ambao hawatufai. 2015 KURA YAKO MUHIMU
 
....... YANA MWISHO........

Iwe kwa heri au shari, ni mapito tu watanzania wanapita kwa sasa, la kushukuru kila mtu anaona yanayotendeka, CCM wananyonya damu mpaka wamama waliotoka kujifungua, CCM ni zaidi ya ma - vampire.....dawa inachemka 2015 watainywa tu iwe kwa kupenda au kwa kulazimishwa, tumechoka na hii kansa CCM.
 
Tuhusishe hili suala na vitu vingine.

Kuna matabaka na misuguano ya matabaka tokana na kugawana vibaya rasilimali. Serikali inatunga sheria ya kulinda walio nacho na kupuuza wasio nacho. Hii pia ipo katika kanuni za bungeni.

Mambo ya bungeni hayaakisi mambo yaliyopo huko mtaani kwa wananchi.

Tunapigania usawa, lakini kuna watu wanaweka vikwazo kupata usawa. Spika Sitta alifanyiwa kampeni asiwepo ili wanaopigania usawa washindwa.
 
Kolimba aliposema Nchi imepoteza dira, aliitwa Dodoma na akarudi kwenye boksi.

Wapinzani watulize mpira chini kwa kuwa chama tawala wameamua kucheza rafu. Wabaki kwenye hoja za msingi zenye maslahi kwa wananchi.
 
Idd Majuto - Mwanachuo

Hakubaliani na hali hii.

Faida ya haya matusi ni kujua mchele na pumba, wananchi watoe pumba waache mchele.

Wabunge wanatukanana wakiwa bungeni lakini wakitoka wanashirikiana. Watu wajitambue na wasitegemee wabunge kubadili maisha wao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom