Kipigo cha mbwa koko ukizaliwa Afrika hakiepukiki

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
AFRIKA KIPIGO CHA MBWA KOKO HAKIEPUKIKI.

Na, Robert Heriel

Leo sina maneno mengi kama wengi wasivyotaka makala ndefu.
Haya twende sasa.

Kipigo cha mbwa koko Afrika hakiepukiki maadam umezaliwa Afrika na wewe ni Muafrika.

Ukiwa tumboni mwa mama yako apapaswa na kichapo ambacho anapigwa Mama yako na Baba. Wengine hupokea kichapo mpaka mimba zinatoka. Vichapo vya mbwa koko vimedizainiwa aina aina. Nitaeleza baadaye, aah! Nimekumbuka mlisema hamtaki mada ndefu hivyo sitaeleza.

Mimba kichapo, Ukizaliwa kichapo hakiepukiki kwa manesi wa kibongo bongo kule leba. Utapigika na matusi juu.

Ukipelekwa shule kichapo cha viboko vya waalimu wenye hasira kali mpaka makalio yakakamae. Ukimaliza shule usijedhani utapumua, thubutu, kichapo kipo palepale huko mtaani ndiko kuliko na kichapo cha paka mwizi.

Usipokuwa na kazi kichapo ni kikali zaidi kwani unaonekana kitoronto.

Ukiwa una kazi kichapo ndio zaidi na zaidi, mijeledi na vibomu kutoka kwa ndugu, ukweni, rafiki na jamaa ni kama vile wametumwa wakumalize.

Ukiwa masikini kichapo ni kikali cha mbwa koko.

Ukiwa tajiri kichapo mwanzo mwenga, mawe na vijembe vya wadau kuwa pesa zako niza kumwekua mwekua kama sio za Binti ndembo mawe haya huwahusu wale wasio na elimu na kazi nzuri.

Kama ni tajiri mwenye elimu kichapo chake ni mianzi watu wakimshutumu ni Illuminant kama sio Freemason.

Ukifa ndio kabisa wala usijedhani utapumzika. Kipigo kiko palepale😁😁 Kaburi lako litapasuliwa nazi na washirikina watafuta pesa za jini subiani.

Afrika Kipigo mwanzo mwisho huwezi kukiepuka kwa vyovyote vile.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Back
Top Bottom