Kipi tujifunze kama Taifa katika picha hii ya Mama Maria Nyerere akiwa pamoja na Mbowe na Dr. Slaa

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
DSC_7031.JPG

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akifungua kikao maalum cha Baraza Kuu la CHADEMA, January 2013. Huku picha ya Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere ikionekana kwa nyuma.
Mbowe+na+Mama+Maria.JPG

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akitoa salamu za chama hicho kwa Familia ya Mwalimu Nyerere, wakati vongozi mbali mbali na wabunge wa chama hicho, walipomtembela Mama Maria Nyerere (katikati) nyumbani kwake Butiama jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa.
Mtoto%2Bwa%2BNyerere.JPG

Mtoto wa tatu wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Magige Kambarage, akitoa nasaha zake kwa viongozi na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walipozulu katika kaburi la baba yake Butiama.
Viongozi%2Bwa%2BCHADEMA%2Bwakitoa%2Bheshima.JPG

Hapa wageni ambao ni viongozi wa Chadema na wenyeji wa familia ya Nyerere wakimwombea mwasisi huyo wa taifa.
===========================================================
Nimejaribu kuangalia hizi picha ili nisome ujumbe ulioko ndani ya picha halafu nikafikiria mapendekezo ya UKAWA-ndani ya Bunge Maalum inayoongozwa na Mh. Mbowe na pia UKAWA-nje inayoongozwa na Dr. Slaa ambapo waliamua kukaa chini wakisaidiwa na Tundu Lissu na kuandika mapendekezo ya wajumbe wachache, baadaye wakaamua kumpa Mh. Tundu Lissu ili ayawakilishe ndani ya Bunge Maalum siku ya Jumamosi, tarehe 12 April 2014.

Mapendekezo yake yalikuwa yamejenga maudhui kuwa Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga katika utawala wake na hakuviweza vya kuchinja. Mwl. Nyerere alikuwa ni muongo na mdanganyifu katika utawala wake na hakuweza kusema ukweli. Mwl. Nyerere alikuwa ni tapeli na aliwatapeli wananchi kuwaaminisha kuwa wameungana wakati hawakuungana kama nchi moja mpaka mwaka 1984.

Wakati hayo yakijiri, Muasisi wa CHADEMA amenukuliwa akisema,
Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:

Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei,

Founder Chairman of CHADEMA.

Hawa viongozi wakuu wa CHADEMA walienda kumjulia hali Mama yetu, Mama Maria Nyerere na kuhani kwenye kaburi la Baba wa Taifa wakati wanaamini ndani ya mioyo yao kuwa Marehemu Mume wake(Baba wa Taifa) katika utawala wake alikuwa ni muongo, mdanganyifu na mjanja janja ambaye hata Muungano wetu aliufanya kwa ujanja ujanja na udanganyifu na aliendelea kuwadanganya wananchi mpaka alipoaga dunia. Kwa mantiki nyingine, walienda kumsalimia Mke wa Rais ambaye alikuwa anaishi na Rais tapeli wa kisiasa.

Inaonyesha kuwa, viongozi wakuu wa CHADEMA wanamtumia Baba wa Taifa kwa maslahi zaidi ya kisiasa. Viongozi wakuu wa CHADEMA wanamuweka Baba wa taifa katika pande mbili kama sarafu. Upande mmoja wanamuita tapeli ili kuliingiza ndani ya fikra za CHADEMA kundi la baadhi ya watu wenye fikra hizo na upande wa pili wanasema ni kiongozi shupavu na Baba wa Taifa ili pia kuliingiza kundi la watu wengi wanaofahamu hivyo.

Kama kweli Baba wa Taifa alikuwa ni tapeli, kwa nini waliamua kwenda kuhani kaburi la kiongozi wanaeamini kuwa ni tapeli?. Kwa nini wanaweka picha za Baba wa Taifa kwenye ofisi na mikutano yao. Hivi ni nani mnafiki na mlaghai wa kisiasa hapa?.
 
Nyerere hakuwa Mungu wala Malaika, alichokisema TL ni kukosoa baadhi ya mambo yaliyofanywa chini ya utawala wa Nyerere ambayo mpaka sasa yanaligharimu taifa hili. Hii ndio democracy ya kweli na sio unafiki wa kukumbatia maovu. Kukusoana ni nyenzo muhimu ya kufikia ukweli.

  • :der:
 
Hatuna cha kujifunza kwa mijitu inayomtukana mwasisi wa taifa hili.
 
poleni sana watanzania kwa kuishi nchi moja na watu kama hawa walioamua kumdhalilisha hayati Baba wa Taifa kwa kumfananisha na matapeli akina Msofe ila Mungu yupo
Mbowe+na+Mama+Maria.JPG

Mnafiki ni mtu mbaya sana.
 
Nyerere hakuwa Mungu wala Malaika, alichokisema TL ni kukosoa baadhi ya mambo yaliyofanywa chini ya utawala wa Nyerere ambayo mpaka sasa yanaligharimu taifa hili. Hii ndio democracy ya kweli na sio unafiki wa kukumbatia maovu. Kukusoana ni nyenzo muhimu ya kufikia ukweli.

  • :der:

Nani kasema Baba wa Taifa alikuwa Mungu?.

Kukosoa na kumuita mtu muongo na tapeli achilia mbali binadamu mwenye stature ya Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere ni vitu viwili tofauti.

Kilichotakiwa kukosolewa (kama kipo) ni kazi alizozifanya na siyo personality yake kama viongozi wa UKAWA-nje na ndani walivyofanya wakiongozwa na viongozi wakuu wa CHADEMA
 
Ni kujifunza kwamba kila roho itaonja mauti,na jukumu tulilonalo kama taifa ni kuhakikisha kwamba tunafanya yaliyo mema yanayomfurahisha MUNGU,ili siku tukitwaliwa kutoka katika dunia hii tuweze enda kuiona mbingu

AMINA
 
poleni sana watanzania kwa kuishi nchi moja na watu kama hawa walioamua kumdhalilisha hayati Baba wa Taifa kwa kumfananisha na matapeli akina Msofe ila Mungu yupo
Mbowe+na+Mama+Maria.JPG

Mnafiki ni mtu mbaya sana.

- Hawa Chadema ni janga la Kitaifa kama sio la Kidunia!1

Le Mutuz System
 
Hatuna cha kujifunza kwa mijitu inayomtukana mwasisi wa taifa hili.

Lazima kuna cha kujifunza.

Hata kichaa huwa ana jambo anaweza kukufundisha negatively or positively. Ndiyo maana nikauliza swali ili tupate angalizo kwa manufaa ya taifa letu endelevu.
 
Mbona mmebakia kulisema hilo la utawala wa uongo? Kwanini amuelezei mengine aliyoyaeleza Lissu kama Mzee Jumbe yupo kizuizini huko Mjimwema, mbona siwasikii mkilizungumzia hili. Je mnaona mambo kama hayo yalikuwa halali?
 
- Hawa Chadema ni janga la Kitaifa kama sio la Kidunia!1

Le Mutuz System
We all know a picture is worth a thousand words.

Bado ninaendelea kuyasoma maneno ya picha hizi ili
nielewe ujumbe wake vizuri kwa faida ya taifa la leo na kesho.
 
Mkuu MwanaDiwani, nimekuwa nikikufuatilia sana kwa hoja zako ambazo kitaalamu hazina mashiko. Na ningependa kudhibitisha nilicho kisema kwa kukuuliza maswali matatu
  1. Je! Nyerere hakuwai kufanya jambo baya/uwongo ama ujanjaujanja katika kipindi cha uongozi wake?
  2. Kama jibu ni hapana, aliwahi., Je! nidhambi kueleza mabaya/makosa ya Nyerere ili yarekebishwe?
  3. Kama nyerere alifanya hila kwa kusudi ya kuijenga ccm, leo hii kuna mwana ccm yoyote anaweza kuyataja?
 
Ni kujifunza kwamba kila roho itaonja mauti,na jukumu tulilonalo kama taifa ni kuhakikisha kwamba tunafanya yaliyo mema yanayomfurahisha MUNGU,ili siku tukitwaliwa kutoka katika dunia hii tuweze enda kuiona mbingu

AMINA

Ndugu, umeongea vizuri sana.

Je, unadhani ni kazi ya binadamu kumuhukumu binadamu mwingine bila utetezi wake?.
 
Muone huyu alivyonyenyekea kumbe ni chui ndani ya taifa letu changa pole sana Mama Maria kwa kuwakalibisha Mashetani.
SlaakusalimiananaMama.jpg
 
Back
Top Bottom