Kipi Kinakuvutia JamiiForums?

Kipi Kinakuvutia JamiiForums?

Mi kinachonivutia ni hizi ID fake tu kwa kweli mana zinasababisha watu wanafunguka kwa uwazi kabisa mana kuna vitu vingine huwa vinaongelewa mpaka unasema daah ingekuwa majina yetu halisi sidhani kama jf pangekuwa sehemu salama.
 
Habari zenu wadau wa JF.

Naam wakuu kama tunavyo tambua na kuelewa kuwa Forums inayo bamba na kupedwa zaidi Afrika Mashariki basi bila shaka ni Jamii Forums.

Hivyo basi kufikia hatua hiyo kuna vitu vinavutia kwa washirika wake kupitia mijadala mbalimbali, kipi kinakuvutia na unakipenda zaidi.??

Binafsi navutiwa na majibu ya Raia humu ndani, mfano mtu kaomba ushauri majibu atakayo pewa yanaenda tofauti na alicho kusudia kupokea.
napenda ukiuliza kitu kama unataka kujua basi lazima utaelekezwa kiustaarabu kuna siku niliwahi kupewa frequency za tv bureee tena tv za kulipia niliangalia kama miezi nane hivi sema wakahama but bado wanarudi na kutoka bureee niliwakubarii
 
JF ni kisima cha maarifa.
drinking.jpg
 
Mi nikisikia tetesi yeyote mtaani nakimbilia humu nisipoikuta basi najua uzushi tuuu.
 
Nimejifunza vingii sana , sasa hivi naweza kubishana na mtu kwa ujasiri kabisaaa ,kumbe nimeiba mawazo ya watu humu ndani hahaha lol, halafu kila habari napata sikumbuki mara ya mwisho niliangalia taarifa ya habari lini maana najikuta vingi nishavisoma hapa,kwa hyo hata kale kaking'amuzi toka uchaguzi uishe sijawahi kukatia hela
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom