Kipi kinakatika umeme au waya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipi kinakatika umeme au waya

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mwenzetu, Jul 15, 2011.

 1. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Wana JF mnijuze,kipi kinakatika umeme au waya?
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Vyote.
   
 3. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Umeme unakatika, waya unavunjika!
   
 4. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  moja, kwa mazoea ni kuwa chenye kukatika ni kile chenye umbo lenye kuonekana..ni kwa kwa mantiki hiyo unapata tabu kufikiri kuwa umeme nao hukatika kwa vile hauna umbo lenye kuonekana(tunaona nyaya na athari ya umeme lakini si umeme wenyewe).

  nadhani hapa kiswahili kilikosa neno stahiki na hivyo kikaazima kutoka lugha ya kiingereza(power cut off) na kwa makubaliano kwa vile kitu kinapokatika kunakuwa na ends mbili zisizo na muunganiko basi hewala kukosekana kwa huduma ya umeme wacha kuwe ni umeme kukatika!

  kwa hiyo mkuu..umeme unakatika, maji yanakatika kadhalika simu inakatwa.

  kuhusu waya mkuu..unakatika..ingawa kuna mkuu wangu mmoja amesema waya unavunjika, sidhani!
   
 5. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  @Al Zagawi:
  Asante kwa ufafanuzi fasihi. Hii mada ukiiangalia kwa pupa inaoneka kama ni rahisi vile, lakini ukiikaribia zaidi ndio ugumu wake unavyoziidi kuongezeka. Swali langu la nyongeza ni: ipi tofauti kati ya kukatika na kuvunjika? Kijiti cha kiberiti kinakatika au kinavunjika?
   
 6. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  ............nashukuru kwa ufafanuzi,
   
 7. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  .............rungu,usichanganye lugha na wewe unapokuwa kazini,maana unapokuwa kazini hata maji yanaweza kuvunjika,jaribu kudhibitisha kwa kumuuliza mtu aliyepigwa rungu uone................ha........haa........haaaa,nashukuru kwa jibu.
   
 8. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  .....tusubiri wataalamu wa lugha......................,rungu na kirungu.............pia itafuata
   
 9. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Duh, hii kali!
   
 10. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  mkuu wangu rungu, asante kwa kushukuru...

  sasa tuendelee na mada...tofauti ya kukatika na kuvunjika!

  kukatika...kwa mazoea(sijui kwenye kamusi wanasemaje, hapa natumia uzoefu tu) tunatumia neno hili katika vitu visivyo na maumbile yenye kuonekana kama huduma mbalimbali mfano huduma ya umeme imekatwa, huduma ya maji imekatwa, huduma ya simu imekatwa. na neno mbadala kwa baadhi ya huduma ni kusitisha..mfano kuduma ya kusajili namba za simu imesitishwa kuanzia tarehe fulani mpaka tarehe fulani. tanbihi; kwa makosa watu hutumia neno imesimamishwa badili ya imesitishwa.

  Kuvunjika...kwa mazoea tunatumia neno hili kwa vitu vyenye maumbile yenye kuonekana na ambavyo ends mbili zinapokosa kuungana kwa kutenganishwa na ikiwa katika tendo la kutenganisha kuna sauti inazalishwa. ni kwa mantiki hiyo njiti ya kiberiti inavunjika na waya unakatika(kumbuka waya unapokatika huwa hakuna sauti yenye kusikika kwa uwazi.

  lakini kama alivyosema mkuu Rungu hapo juu...hii mada ni ngumu pengine wakija wataalamu humu wataweza kutusaidia...bahati mbaya mzee wetu wa mbinu za kiswahili katika TBC1, Suleiman Hegga, sidhani kama anapita maeneo haya.
   
 11. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  kuvunja :1- tunaweza kusema ni kwa kutumia kitu kisicho na makali, mfano vunja mlango kwa kutumia jiwe , vunja nyumba kwa kutumia mitaimbo nk.
  2- kuvunja kwa kutumia nguvu za mwili , beki wa timu A kamvunja mguu mshambuliaji wa timu B.

  kukata : 1- ni kuvunja ila hili linatumika kwa kitu chenye makali, panga,kisu shoka nk . kata mti ,tawi
  2- kusita kwa huduma kama maji ,umeme nk.
   
 12. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Mjadala huu umetulia!
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Matumizi mengine ya kuvunja na kukata ni:
  - Kuvunja mahusiano
  - Kuvunja ungo
  - Kuvunja mkutano
  - Kuvunja (kukata) mbavu
  - Kuvunja sheria
  - Kuvunja mkataba
  - Kuvunja mwiko
  - Kuvunja pesa
  - Kuvunja mgongo
  - Kuvunja moyo
  - Kuvunja rekodi
  - Kukata shauri
  - Kukata mawasiliano
  - Kukata viuno
  - Kukata karata
  - Kukata sala
  - Kukata tamaa
  - Kukata roho
  - Kukata mshahara
  - Kukata kauli
  - Kukata kamba
  - Kukata maji
  .................
  Hii ni kusema kuwa hata "umeme unakatika", na hili tusilichukulie kama ni upungufu wa Kiswahili bali ni utajiri wa lugha yetu.
   
 14. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  -Kukata kiu
  -Kukata mbuga
  -Kuvunja ukimya
   
 15. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  ni kweli mkuu..tunajifunza huku tukijipunguzia shinikizo za kule kwenye siasa
   
 16. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Duh,amakweli kukatika kwa umeme na waya,sasa imekuwa tena kuvunja na kukata,mara ungo,haya tena viuno.Rungu nisaidie,kwani Mammamia kama alivyotujuza huu ni utajiri wa lugha yetu.kirungu na rungu tofauti ni nini?.................,Kwa haraka haraka tuu si kila kukatika kuna hasara,hata pia kuvunja.......................ukichukulia maneno ya Mammamia hapo juu utaona kuwa,kweli lugha yetu inautajiri mkubwa,unaweza kubisha lakini tafakari na chukua hatua.......................jaribu kukata,si umeme ila kiuno uone...............,vilevile waulize waliovunja ungo........je,wanajuta...............Nikupongeze sanaaaaa Mammamia,si kwa kukata kiuno au kuvunja ungo,bali kwa kutujuza upana wa lugha yetu..............kiswahili hoyeeeeeeeeeeee
   
 17. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Oyeeee! Duh, aisee hata mimi sijui tofauti ya kirungu na rungu. Wacha akina X-Paster waje na tafsiri zao!
   
 18. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  kwa mazoea rungu na kirungu ni kitu cha namna inayofanana lakini saizi ndiyo inatofautisha baina ya vitu hivyo viwili...ikiwa ni kidogo huitwa kirungu na kinyume chake ni rungu.

  lakini maneno yote mawili yanatumika katika lugha za msimu kumaanisha vitu au hali tofauti na asili ya maneno yenyewe mfano..rungu litakushukia ni tamathali ya semi ikimaanisha utapata adhabu kali mfano wa kupigwa na rungu. mfano mwingine ni...alinipiga kirungu hutumika kumaanisha aliniomba pesa.

  kiswahili lugha adhimu, ngumu kwa wasoipa umuhimu...nawasilisha
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Mkuu........hata kiuno pia kinakatika:typing:
   
 20. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,094
  Trophy Points: 280
  Vyovyote utakavyotamka au kutumia neno lakini maanake ni nchi kuwa gizani kwa sababu context iko wazi. Unafikiri neno likikosewa wakati kwa situation iliopo ujumbe ni clear Jairo, Ngeleja, Malima na JK wata-escape punishment kutoka kwa wananchi?
   
Loading...