Kilimo cha mkulima wa mvua kwa sasa, labda wapewe ruzuku na serikali. HakikopeshekiTaasisi za kifedha pia zimegoma kuwa rafiki wa mkulima, mkulima hakopesheki akikopesheka basi kwa masharti lukuki, sector za kifedha zimulike fursa zilizopo ktk kilimo ili kuwawezesha wakulima kufanya kufanya kilimo chenye tija.
Kuna hoja 2 muhimu katika maelezo yako.Haya Sasa ndiyo mambo ya Kujadili! Sema Sahv watanzania asilimia kubwa akili, mawazo yao wako kwenye mambo ya udaku bongo fleva bongo movie..
Ngoja turudi kwenye uzi Sasa-
Kwanza lazima mtambue kuwa sekta ya kilimo Tanzania inachangia karibia asilimia 29 ktk uchumi wa tanzania
Kuna vikwazo vingi Ambavyo vinarudisha nyuma au kukwamisha sekta ya kilimo Tanzania, mfano uhaba wa pembejeo ambazo hazitoshelezi, mbegu nazo hazina ubora, mbolea napo kizungumkuti, madawa nayo kasheshe...., kingine Kuna changamoto ya masoko
KITU KINGINE NILICHO KIONA KAMA SERIKALI INATAKA NCHI IPIGE HATUA KUBWA KWENYE KILIMO, waje na sekta 1 au 2 Yaani sekta dume
Wahamasishe watu, wakulima kulima sana mazao 1 au 2 kwa kiasi Kikubwa Mf mahindi, mpunga na hayo mazao ndiyo yatiliwe mkwazo snaaa
Huku wengine wakilima mazao mngine kama kawaida
Hapo ndipo kutaonekana na kupata mafanikio
Ova
Katika kilimo inaweza kuwa tofauti kidogo.Nafikiri hujawahi kulima ndio maana unasema hvyo. Mazao mengi sana hayana soko la uhakika japo hayazalishwi kwa wingi sana, Sasa yakizalishwa kwa wingi tena itakuwaje? Na ukumbuke hayazalishwi kwa wing sana coz pia wengi wenye mitaji wanakikwepa kilimo. Miaka mingi kilimo kinajiendesha chenyewe tu, kusiwepo na ruzuku watu wanalima ila mwisho masoko yanakuwa ishu. Angalia matunda na mbogamboga, mahindi, mpunga, mbaazi n.k
Habari Dada !Hello JF,
Hii ni moja ya kati za threads zangu za mwisho mwisho..LOL
I am trying to cut my time spending browsing JamiiForums...
So far, i am doing great, sijapost chochote in four days..LOL.....
Anyway,
Ningependa kujua nini kinachokosekana kwenye Kilimo chetu???
Ili kiwe chenye tija kwa manufaa ya watanzania....????
Tuna depend kwenye Kilimo, yet nahisi hili ni eneo moja ambalo halijawa exploited fully...
Again, tu brainstorm wapi pana tatizo..
Thanks all..
Wakulima wananyonywa sana
Katika kilimo inaweza kuwa tofauti kidogo.
Ukiwa na bidhaa kubwa ndipo inakuwa rahisi kupata soko kuliko kama utazalisha kwa kiwango kidogo.
Urahisi wa kutafuta soko la kilo 40 za Ufuta au Alizeti ukiwa kijijini ni kwamba utaishia kutegemeo wanunuzi waliokuzunguka.
Ukibadili hizo kilo kuwa tani....say tani 40, ni kiasi ambacho soko litakutafuta wewe
Hapo kwenye woga wa njaa ndio palipochangia pia kudidimiza wakulima. Mnafunga masoko ya nje ili tu kuzuia vyakula vibaki ndani utazan tunawaza kula tu. Fungue masoko watu watalima vingi tu na tutakuwa na chakula cha kutoshaNyie mnaolilia soko tafadhali mjikite kwenye mazao ya biashara pekee, chakula kikipanda bei hata hao ‘wakulima’ watashindwa kumudu na kuishia kulialia.
Endeleeni kujadili, naendelea kujifunza.
Kuna hoja 2 muhimu katika maelezo yako.
1. Ubora wa pembejeo.
Si kweli kwamba pembejeo hazipo, zipo nyingi sana. Tatizo lipo kwenue ubora kuwa mdogo hali inayopelekea mkulima kutojua ni zipi nzuri na zipi aachane nazo.
Nini kifanyike.
Serikali kusimamia kwa utahbiti uingizwaji na uzalishaji wa pemebejeo bora ili kupunguza utitiri wa pembejeo sokoni huku nyingi zikiwa hazifai.
2. Kutenga kanda za uzalishaji.
Endapo kutakuwa na kanda za uzalishaji (Production Zones) ambazo zitasimamiwa kiufasaha kuanzia:-
a). Elimu ya uzalishaji & udhibiti wa magonjwa na visumbufu.
b). Elimu ya uongezaji thamani ya mazao.
c). Mfumo wa masoko kuboreshwa.
d). Kuchagua mazao machache muhimu katika kanda husika na kuyasimamia kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuimarisha masoko.
Haya yakifanyika kwa ufasaha, kero za waKulima zitapungua na tija kuongezeka.
Anywa, itoshe kusema kila eneo la uzalishaji lina changamoto tofauti na jingine na utatuzi wake pia kutofautiana.
Hatufanyi processing baada ya kuvuna. "Post harvesting technologies" ziko poor sana.Umaskini ndio sababu, tunatumia products za kutoka nje nyingi sana inapekelea kunufaisha viwanda vya nje,
Lakini ukija kwenye kile kinachozalishwa nchini kwetu, hakina dhamani kwa sababu soko lake ni kumuuzia maskini mwenzako tu, na mbaya zaidi mazao ya kilimo unapochelewa kutoa ghalani ndipo ubora unazidi kupungua.
Thanks mkuu, nimependa hio ya Kanda/production zone..ni kweli hatuwezi collectivelly kulima kwa umoja sababu mazingira tulionayo ni tofauti, 'matunda' Tanga, 'Fishery' pwani, 'Bee-keeping'; Singida na Tabora.. wote tukiwa wazalishaji katika mazingira yetu tutamove on as a nation, sijui haya ya Fishery yanafall under Kilimo?? LOL...
Katika mada hii nimeuliza specific Elimu ya Kilimo ihusu nini,naona umejibu A na B, thanks mkuu........
Hii ya kuchagua mazao machache muhimu naona imejirudia, binafsi naona, tuangalie nini kinahitajika ndio tulime na sio kwamba tulime ndio tuangalie soko linahitaji nini.....kuna mazao Demand yake haikauki kama Kahawa, sema tu hatuna FLOW nzuri ya watendaji,kutoka mkulima mpaka consumers... hapo katikati kuna watu wana interests zao.. very sad
Uko sahihi mkuu,sisi kama wananchi hatuna muamko, inabidi tubadilishe mindset zetu kwanza...kilimo kinaonekana ni cha wachache waliofeli maisha , i guess Kilimo kiwe introduced slowly kwenye curriculum za wanafunzi..by the time wanamaliza shule wanakua na msimamo postive kuhusu kilimo.....
Question is; huko shuleni tutawafundisha nini kuhusu kilimo?? mkuu embu tiririrka..lol
Tatizo lipo kwa wakulima wenyewe, wanashindwa ku-anticipate zao gani walime wakati gani, yaani unakuta wakisikia nyanya ziko juu woooote wanaingia mkenge, mwishowe zinaoza mashambani, wakati huo huo parachichi zinaadimika na bei kupaa, hawana akili inshortHello JF,
Hii ni moja ya kati za threads zangu za mwisho mwisho..LOL
I am trying to cut my time spending browsing JamiiForums.
So far, i am doing great, sijapost chochote in four days..LOL.
Anyway,
Ningependa kujua nini kinachokosekana kwenye Kilimo chetu?
Ili kiwe chenye tija kwa manufaa ya Watanzania?
Tuna depend kwenye Kilimo, yet nahisi hili ni eneo moja ambalo halijawa exploited fully...
Again, tu brainstorm wapi pana tatizo..
Thanks all..