General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,301
- 23,023
Habari JF, GT
Kama ilivyo ndoto za watu wengi kumiliki makazi ya kuishi kwa muda mchache tuliopo hapa duniani, basi naomba nilete huu mtanziko ambao umekua mjadala kati yangu na Mjomba wangu.
Katika michango yenu, yawezekana nikapata mawazo mapya pengine kuliko niliyokuwa nikimshauri Uncle.
Uncle wangu ni Mstaafu na karibuni anategemea kupata mafao yake. Tangu katika utumishi wake hakuwahi kujenga na kumiliki nyumba. Fedha anayotegemea kupokea kwa makadirio ni 80M.
Baada ya kunieleza mpango wa matumizi ya mafao yake, cha kwanza alichosisitiza ni kuwa na nyumba ya kuishi kumalizia uzee wake yeye na mkewe. Watoto tayari wanajitegemea. Bajeti aliyoitenga kwa nyumba ni 60m tu.
Kwa upande wangu nilimshauri ni vema akanunua nyumba kwa fedha hiyo aliyoitengea bajeti. Ujenzi sio kazi ndogo, inahitaji uzoefu na usimamizi. Vilevile ukizingatia hana kiwanja, kwenye hiyo 60m ukiweka na kiwanja hawezi kujenga nyumba nzuri.
Ukiachana na shughuli ya ujenzi, pia kuna suala la sehem utakayo jenga. Kiukweli kupata kiwanja cha maana ni lazima uende nje ya mji sana, almost 30km from city center. Na mara nyingi maeneo hayo huduma za msingi zinakuwa hazija fika.
Lakini akitulia kwa utulivu, hapo Kimara, Kigamboni, Kinyerezi nyumba za 50-60m zipo za kumwaga.
Pamona na ushauri wangu, kuna wengine ambao aliwashirikisha lakini walikuwa tofauti na mimi, wao walimshauri ajenge kwani ataweza jenga nyumba anayoipenda kwa ubora na kuchagua ramani anayoitaka.
Natambua JF kuna watu wenye uzoefu na hizi mambo, nawashirikisha nipate mawili matatu....