Kipi bora kati ya kununua nyumba au kujenga nyumba?

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,302
23,020
Habari JF, GT

Kama ilivyo ndoto za watu wengi kumiliki makazi ya kuishi kwa muda mchache tuliopo hapa duniani, basi naomba nilete huu mtanziko ambao umekua mjadala kati yangu na Mjomba wangu.

Katika michango yenu, yawezekana nikapata mawazo mapya pengine kuliko niliyokuwa nikimshauri Uncle.

Uncle wangu ni Mstaafu na karibuni anategemea kupata mafao yake. Tangu katika utumishi wake hakuwahi kujenga na kumiliki nyumba. Fedha anayotegemea kupokea kwa makadirio ni 80M.

Baada ya kunieleza mpango wa matumizi ya mafao yake, cha kwanza alichosisitiza ni kuwa na nyumba ya kuishi kumalizia uzee wake yeye na mkewe. Watoto tayari wanajitegemea. Bajeti aliyoitenga kwa nyumba ni 60m tu.

Kwa upande wangu nilimshauri ni vema akanunua nyumba kwa fedha hiyo aliyoitengea bajeti. Ujenzi sio kazi ndogo, inahitaji uzoefu na usimamizi. Vilevile ukizingatia hana kiwanja, kwenye hiyo 60m ukiweka na kiwanja hawezi kujenga nyumba nzuri.

Ukiachana na shughuli ya ujenzi, pia kuna suala la sehem utakayo jenga. Kiukweli kupata kiwanja cha maana ni lazima uende nje ya mji sana, almost 30km from city center. Na mara nyingi maeneo hayo huduma za msingi zinakuwa hazija fika.

Lakini akitulia kwa utulivu, hapo Kimara, Kigamboni, Kinyerezi nyumba za 50-60m zipo za kumwaga.

Pamona na ushauri wangu, kuna wengine ambao aliwashirikisha lakini walikuwa tofauti na mimi, wao walimshauri ajenge kwani ataweza jenga nyumba anayoipenda kwa ubora na kuchagua ramani anayoitaka.

Natambua JF kuna watu wenye uzoefu na hizi mambo, nawashirikisha nipate mawili matatu....
 
Nadhani anunue, nie nimjenga nyumba ya mita 10.5 kwa 15 lakini imekula 90 m na siweka fensi. Mwanzoni nilijua itakula labda 70. Lakni unawezakununua kwani kunawatu wanauza kwa sababu ya madeni ya benk au kutaka kupata pesa za ziada ili maoisha yaende. Cha mhimu atangaze facebook sifa za nyumba nayaotaka na maeneo na size za kiwanja.
 
Uncle wangu ni Mstaafu na karibuni anategemea kupata mafao yake. Tangu katika utumishi wake hakuwahi kujenga na kumiliki nyumba. Fedha anayotegemea kupokea kwa makadirio ni 80M.

Kwanza, Mwambie aaache hizo akili za kutegemea hela ambayo haipo mfukoni mwake mkuu. It's to risk.

Pili, kwanini hakujenga miaka hiyo yote anataka kujenga sasa akiwa mzee?

Tatu, anunue tu nyumba maana akisema ajenge itakula kwake kwa sababu hakuna anayejua kesho yake mfano wakati wa kujenga anaumwa ugonjwa ambao unahitaji pesa nyingi huoni itabidi achukue ile ile iliyopo kwenye bajeti ya ujenzi? akishaitumia atapata wapi ya kuendeleza ujenzi?
 
Kuna nyumba zinauzwa nzuri sana kwa bei ya kawaida kwa hapa dar sijajua huyo ndugu yako yupo wapi ila ubaya wa nyumba nyingi zinazouzwa ni hazijajengwa kwa standard inayotakiwa,kila eneo huwa wanapunguza materials au wananunua ya bei ndogo,hawa wajenzi wa nyumba hizi wanaitwa Jenga uza yani hii ndio biashara yao,anajenga kwa 30 milioni anauza kwa 45 milioni faida anapata nyingi, nyingine huwa zinauzwa kutokana na watu kushindwa kulipa madeni waliyokopa,hivyo mabenki yanalazimika kuuza na kufidia hela zao,nyumba zingine watu wanauza nyumba zao kwasababu ya kiuchumi hivyo mtu anaona ajiokoe kwa kuuza tu apate hela mambo yaende ila ubaya wa nyumba hizi nyingi watu huwa wanafuga madudu yao humo na mazindiko ya kila aina kwahyo mtu unaponunua ujiandae kisaikolojia either uwe mtu wa maombi sana na dua au ushinde kwa waganga.Nyumba za kujenga faida yake utakuwa unajenga kwa quality inayotakiwa,unauwezo wa kuwasimamia mafundi,ila hela inaenda nyingi kwa sababu ukitaka kitu kizuri lazima ugharamike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kumshauri naomba kwanza nimlaumu(samahan lakin)

1.Haingii akilini mpaka anafikisha Miaka 60 kazini Hajasimamisha ata chumba kimoja. Huu Ni uzembe wa Ali ya juu na haitakiwi kufumbiwa macho.

2.Kiinua mgongo hakiwekwa ili mtumishi akajenge, kile ni kwa ajili ya KULA TU matunda ya utumishi wake Miaka yote iyo aliyotumikia(kifuta jasho).
Maana yake ile ilitakiwa iwe pesa ya KULA mema ya nchi,utalii na vacation mbalimbali.

Ushauri:
1. Arudi Mkoani alikozaliwa akatafute Kiwanja Cha Bei nafuu, akajenge nyumba nafuu isiyozidi milioni 20-25

Kwanini nasema ivo: Akijitutumua kujenga hapa Mjini kwa mil. 60, atabakiwa na mil 20.
Sijajua ataifanyia nini ila Kama Ni kujiingiza katika utaftaji,
nakuapia atafeli vibaya mno maana purukushani za utaftaji kwa umri huo wa 60+ Ktk mji wetu huu hatoziweza kabisa, ATAKUFA KWA PRESHA BURE.

2. ASIWE NA WASHAURI WENGI WA FEDHA.
hapa wazee wa fursa washanusa mzee atashika mpunga mwingi mdA sio mrefu.

-Wazee wa MR. KUKU
(wekeza laki 7 upate milioni 70 kwa wiki 4)

-wazee wa FOREX
(wekeza Dola 1000 upate Dola 500,000 ndani ya nusu saa)

MSHAURI MZEE ARUDI BUSH ALIKOZALIWA, ALE MAISHA YAKE YALIOBAKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vyote bora, kutegemeana na mahali/muda nk

changamoto ya nyumba za kununua watakiwa utumie muda mwingi kujua kwa nini inauzwa, manake nyumba nyingi zina mauza uzaaaa na mazindikoooo
 
Mwambie aje kongowe,vikindu na kisemvule huku,gari ni moja tu hadi kufika city centre,kariakoo.
Huku kuna viwanja vya shilingi 1,500,000ts h hadi 3,000000 tu,
Nyumba inaweza kujengwa kwa milion 10 hadi 15 tu maana huku ghalama za ujenzi zipo chini,kwani ukinunua uwanja mchanga wa kujengea unachukua Hapo hapo uwanjani kwako,mabat huku kuna viwanda vya mabat ukienda kiwandani wanakuuzia kwa bei rahisi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kumshauri naomba kwanza nimlaumu(samahan lakin)

1.Haingii akilini mpaka anafikisha Miaka 60 kazini Hajasimamisha ata chumba kimoja. Huu Ni uzembe wa Ali ya juu na haitakiwi kufumbiwa macho.

2.Kiinua mgongo hakiwekwa ili mtumishi akajenge, kile ni kwa ajili ya KULA TU matunda ya utumishi wake Miaka yote iyo aliyotumikia(kifuta jasho).
Maana yake ile ilitakiwa iwe pesa ya KULA mema ya nchi,utalii na vacation mbalimbali.

Ushauri:
1. Arudi Mkoani alikozaliwa akatafute Kiwanja Cha Bei nafuu, akajenge nyumba nafuu isiyozidi milioni 20-25

Kwanini nasema ivo: Akijitutumua kujenga hapa Mjini kwa mil. 60, atabakiwa na mil 20.
Sijajua ataifanyia nini ila Kama Ni kujiingiza katika utaftaji,
nakuapia atafeli vibaya mno maana purukushani za utaftaji kwa umri huo wa 60+ Ktk mji wetu huu hatoziweza kabisa, ATAKUFA KWA PRESHA BURE.

2. ASIWE NA WASHAURI WENGI WA FEDHA.
hapa wazee wa fursa washanusa mzee atashika mpunga mwingi mdA sio mrefu.

-Wazee wa MR. KUKU
(wekeza laki 7 upate milioni 70 kwa wiki 4)

-wazee wa FOREX
(wekeza Dola 1000 upate Dola 500,000 ndani ya nusu saa)

MSHAURI MZEE ARUDI BUSH ALIKOZALIWA, ALE MAISHA YAKE YALIOBAKI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ushajenga ngapi mpaka sasa hivi? Ama kweli mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa!
 
Arudi bush , ajenge nyumba ndogo ya mil 20 hata kama ni chumba na sebure.. mil 60 atumie kuishi vizuri.

Mzee umefika 60 yrs hujajenga nyumba unategemea ujenge uzeeni ili aishi nani wkati watoto woote wanajitegemea..
Ajenge nyumba ndogo ya kumuhifadhi then ale maisha..

Btw pesa ya kiinua mgongo sio ya kujengea wala kununua gari (haya unatakiwa kuyafanya ujanani) hii ni pesa ya kukufanya ustaafu kwa amani bila kuwaza mambo ya chakula wala emergency ndogo ndogo.
 
Hiyo hela atumie kujenga nyumba yake,kununua nyumba sio nzuri kiusalama maana unaweza ukauziwa jumba la udongo lililopigwa plasta vizuri tu kumbe mbovu kama za jenga uza!!
 
Kama amestaafu tuseme ana miaka 60 hivi, anatarajia kuishi miaka mingapi mbele..? Jibu ni kwamba hatujui, tusimpangie.

Watoto wake tayari wanajitegemea, ni yeye na mkewe tu.... hiyo nyumba lengo lengo ni kumwachia nani..?

Aliweza kuishi kwa kupanga, alikotoka ni mbali kuliko aendako.... anaweza kumalizia safari yake bila ‘kumiliki’ nyumba.

Kuzika 60m kwa umri huo ni matumizi ya hovyo ya pesa, akule bata na mkewe na akiweza awasapoti watoto wake kama kuna sehemu wanahitaji ili safari ikiisha wamzike kwa heshima.

I moved your cheese, so what..!!
 
Mkuu kazi unayo.

Nasema hivo sababu 'mbwa mmoja kapigiwa miluzi mingi',atashindwa kudaka uelekeo sahihi.

Comments zote zinafanana ni za: jenga ama nunua!

Sasa hapo sijui lililo sahihi, ila nawe tupe mrejesho ni ushauri gani ambao unauona utamsaidia huyo ba'mdogo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama amestaafu tuseme ana miaka 60 hivi, anatarajia kuishi miaka mingapi mbele..? Jibu ni kwamba hatujui, tusimpangie.

Watoto wake tayari wanajitegemea, ni yeye na mkewe tu.... hiyo nyumba lengo lengo ni kumwachia nani..?

Aliweza kuishi kwa kupanga, alikotoka ni mbali kuliko aendako.... anaweza kumalizia safari yake bila ‘kumiliki’ nyumba.

Kuzika 60m kwa umri huo ni matumizi ya hovyo ya pesa, akule bata na mkewe na akiweza awasapoti watoto wake kama kuna sehemu wanahitaji ili safari ikiisha wamzike kwa heshima.

I moved your cheese, so what..!!
Aliweza kupanga kwasababu alikuwa na ajira(kipato endelevu). Sasa hivi hana hicho kipato ana kiinua mgongo tu.
Sasa kwa ushauri wako ale bata, alipe kodi kwa kiinua mgongo kisa una-assume hana muda mrefu wa kuishi?! Kuna watu wanaishi hadi 100yrs au hata 80yrs ni miaka 20 hio.
 
Wewe ushajenga ngapi mpaka sasa hivi? Ama kweli mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa!
Ndo maana nimeomba samahani kabla sijamlaumu.

Kwa sasa, mpaka bodaboda,mama ntilie unakuta wamejenga Tena wakiwa na umri mdogo.

Kwa fursa zilizoko serikalini, posho,mikopo n.k

Ukikuta mtu kashindwa kujenga hata kibanda Cha milioni 4 hata kwa mkopo Ni wakulaumiwa TU.

Hilo halina mjadala mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arudi bush , ajenge nyumba ndogo ya mil 20 hata kama ni chumba na sebure.. mil 60 atumie kuishi vizuri.

Mzee umefika 60 yrs hujajenga nyumba unategemea ujenge uzeeni ili aishi nani wkati watoto woote wanajitegemea..
Ajenge nyumba ndogo ya kumuhifadhi then ale maisha..

Btw pesa ya kiinua mgongo sio ya kujengea wala kununua gari (haya unatakiwa kuyafanya ujanani) hii ni pesa ya kukufanya ustaafu kwa amani bila kuwaza mambo ya chakula wala emergency ndogo ndogo.
Naungana na huu ushauri. Washauri wote wa maswala ya kustaafu duniani wanakushauri ukishastaafu, kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhama mjini!!!

Wewe mzee wa miaka 60 unataka kukaa katikati ya mji ukifanya nini? Huna kwenu? Hata kama huna kwenu, tafuta eneo nje ya mji huko ambapo unaweza kujenga nyumba nzuri ndogo ya kuishi kwa gharama ndogo. Kwa umri huo, hakuna tena ufahari unaoutafuta kusema unajenga nyumba kali. Fedha zinazobaki azitumie kuanzisha miradi midogo ya ufugaji ambayo itamkeep busy, kumpa mazoezi na kumuingizia kipato kidogo cha kusukuma siku.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom