Kipi bora jamani?

Emecka

Member
Jul 17, 2012
75
27
Heshima mbele wana MMU

Naomba kuuliza, Hivi kipi bora kati ya hivi viwili.

Kuolewa mke wa pili au kuwa nyumba ndogo. Toa sababu za kukubaliana na mojawapo kati ya hayo.
 
bora nyumba ndogo,,akikufumania hana haki ya kukushtaki! tena akizingua unamtema muda wowote.
 
bora nyumba ndogo,,akikufumania hana haki ya kukushtaki! tena akizingua unamtema muda wowote.

Mkuu, huoni kwamba kuwa nyumba ndogo unakosa amani na pia ni risk? Kuna dada mmoja alinusurika kuuwawa kwa kupigwa risasi na NYUMBA kubwa. Bahati nzuri ikampata mkononi mpaka sasa ana ulemavu wa mkono kisa mume wa mtu.
 
shosti kula uhondo kwataka vitendo,kuolewa ukimkuta mke mkubwa sio muelewa kisa cha kupigwa juju nini,na pia kuna uwezekano akatafuta nyumba ndogo au akaongeza mke mwingine,ukiwa nyumba ndogo heshimu ndoa ya mwenzio,usitake kujionyesha kua nawe wammiliki mheshimiwa,jilie vitu vyako polepole bila pupa mbona utayafurahia mahabat tu!!
 
Heshima mbele wana MMU

Naomba kuuliza, Hivi kipi bora kati ya hivi viwili.

Kuolewa mke wa pili au kuwa nyumba ndogo. Toa sababu za kukubaliana na mojawapo kati ya hayo.

ngoja nisogee hapo kwa maria roza maana duu..
 
shosti kula uhondo kwataka vitendo,kuolewa ukimkuta mke mkubwa sio muelewa kisa cha kupigwa juju nini,na pia kuna uwezekano akatafuta nyumba ndogo au akaongeza mke mwingine,ukiwa nyumba ndogo heshimu ndoa ya mwenzio,usitake kujionyesha kua nawe wammiliki mheshimiwa,jilie vitu vyako polepole bila pupa mbona utayafurahia mahabat tu!!

Sasa hiyo nyumba kubwa ikishakugundua si ndio itakupiga juju mara mbili zaidi?
 
Mwenzenu mie umri umeanza kunitupa mkono, niko.kwenye 30+ menopause ileeee naiona imefika Kibamba yaja kwa kasi. Ni either nibaki kuwa nyumba ndogo au niolewe mke wa pili. Nikisema nisubiri huyo mume wangu peke yangu naweza kujikuta menopause inafika sina mtoto hata wa dawa.

Nifanyejeeeeeeeeee?
 
ulikuwa selective sana wakati wa uschana wako na huenda ulipata wanaume wenye lengo zuri nawewe kwa wakati huo ukawatafutia sababu, na hayo ndio huwa ni madhara yake lakini pole sababu hata wewe ipo siku utakuwa nyumba kubwa kwa hiyo nyumba ndogo itayo fuata ,unafikiri kama kashindwa kubaki na nyumba kubwa ndo hiyo ndogo ataiweza ni lazima na wewe utafika mahali atakuona wa kawaida na atatafuta nyumba ndogo zaid tulia utampata mume wako peke yako, jaman kina natasha si hao wanaolewa na miaka 46??? katika mambo ambayo huwa yanawaingiza kidada katika majanga makubwa ni pamoja na kuwa na hofu ya kuolewa hivyo kujikuta wame nunua matatizo zaidi, kama haja ni mtoto si shida ilimradi uwe na uwezo wa kumtunza wanaume wa kukupa mtoto wala si wakuhangaika ilimradi tu utunze mwenyewe lakini hilo unalo taka fanya nahisi litakuwa na raha mwanzo lakini lina shubiri mbeleni kwanza kwa huyo bibie mkubwa na pili hata huyo bwana kwani hadi hapo tu si mwaminifu katika ndoa hivo na wewe ukisha ifikia saba ya pili lazima utaanza kuona tofauti , kwa sasa huwezi iona hiyo tofauti sababu ndo kwanza mpo saba ya kwanza.
 
Mwenzenu mie umri umeanza kunitupa mkono, niko.kwenye 30+ menopause ileeee naiona imefika Kibamba yaja kwa kasi. Ni either nibaki kuwa nyumba ndogo au niolewe mke wa pili. Nikisema nisubiri huyo mume wangu peke yangu naweza kujikuta menopause inafika sina mtoto hata wa dawa.

Nifanyejeeeeeeeeee?

Ooooh so this is your worry!

pole sana... do what thou heart feeleth!
 
Kosa moja halisahihishi kosa la pili...
Kwangu mimi sioni uafadhali wa option yoyote kati ya hizo...
Ukifanywa nyumba ndogo bado utakosa mamlaka kamili kwa huyo aliyekuweka small house...
Ukiwa mke wa pili, hili litategemea na imani yako na mwenzako kama ni halali kufanya hivyo...
 
Naomba kukuuliza swali la kizushi, miaka yoooote hiyo ya nyuma 20+, na kwenye early 30's hivi hukuwahi kutongozwa na mwanaume mwenye nia ya kujenga familia nawe...?
Kama jibu ni ndio ilikuwaje ukaachana nae/nao?

Mwenzenu mie umri umeanza kunitupa mkono, niko.kwenye 30+ menopause ileeee naiona imefika Kibamba yaja kwa kasi. Ni either nibaki kuwa nyumba ndogo au niolewe mke wa pili. Nikisema nisubiri huyo mume wangu peke yangu naweza kujikuta menopause inafika sina mtoto hata wa dawa.

Nifanyejeeeeeeeeee?
 
Naomba kukuuliza swali la kizushi, miaka yoooote hiyo ya nyuma 20+, na kwenye early 30's hivi hukuwahi kutongozwa na mwanaume mwenye nia ya kujenga familia nawe...?
Kama jibu ni ndio ilikuwaje ukaachana nae/nao?

Ndugu yangu hapo nilipokuwa early 30's nilikuwa chuo baada ya hapo nikaenda nje ya nchi sasa nimerudi wale ambao walikuwa wananitongoza enzi hizo wamekwisha kuoa na wengine wapo katika mahusiano karibu wataoa. Nimebaki kwenye dilemma.
 
Kosa moja halisahihishi kosa la pili...
Kwangu mimi sioni uafadhali wa option yoyote kati ya hizo...
Ukifanywa nyumba ndogo bado utakosa mamlaka kamili kwa huyo aliyekuweka small house...
Ukiwa mke wa pili, hili litategemea na imani yako na mwenzako kama ni halali kufanya hivyo...

. Unakunywa kinywaji gani?????

Halafu mleta mada unataka kuolewa kwa kuwa umejiona unachina au kwa kuwa unampendA?

Unadhani akikuoa ndo amemaliza?
 
Heshima mbele wana MMU

Naomba kuuliza, Hivi kipi bora kati ya hivi viwili.

Kuolewa mke wa pili au kuwa nyumba ndogo. Toa sababu za kukubaliana na mojawapo kati ya hayo.

Kuwa nyumba ndogo, si halali ni kosa tu kama kosa lingine lolote la uzinifu. Kuwa mke wa pili, inaweza kuwa ni halali kama imani yako inaruhusu, maana ni mke ambaye anatambulika kila sehemu, tofauti ni kuwa unakuwa na boss ambaye ni mwanamke mwenzio ndani ya ndoa! Kwa wale wenye imani ya Kikristo, mke wa pili huwa hairuhusiwi na hivyo ni kosa tu sawa na kosa la nyumba ndogo.
option zote zina taabu, ila option ya kuwa mke wa pili ni less risk than kuwa nyumba ndogo. Kumbuka kuwa nyumba ndogo haina haki yoyote ile, si kwa huyo mke wala watoto wake!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom