Habari wakuu,
Kama kichwa kinavyojieleza,naomba tuambiane kipengere kilichokuwa kigumu kwako wakati unajifunza programming language yoyote ile.
Kwa upande wangu kutokana na research niliyofanya na kutambua lugha gani nianze nayo kwa ajili ya projects zangu,niliamua kuanza na Python.Kama kawa nilianza vizuri nikafika hadi kwenye functions, hadi kufikia hiyo point sikusumbuka kiasi hicho japo nilihaso kidogo.
Tatizo lilianzia pale kwenye OOP.Kusema kweli hii point nilistruggle sana.Nasoma maelezo kisha nacopy code inarun vizuri na kutoa output ila sasa nikiicheki code ili kujua why output imekuja hii nachoka.Ila nashukuru nilivuka.
Ningependa kusikia uzoefu kutoka kwenu pia,Karibuni.