Kipengele cha kuhakiki vyeti kinakera sana

Tamu chungu

Member
Dec 20, 2015
85
64
Nachukia sana ninapoona kampuni inatangaza nafasi za kazi na moja ya masharti wanakwambia uende mahakamani kusetifai vyeti vyako kisha ndo utume maombi.

Wanashindwa kutambua kwamba vijana waliopo mtaani kuna wakati wanakosa hata pesa ya kutolea vyeti photocopy,kwakua waajiri wao wana uhakika na mshahara hawataki kufikiria mara mbili kuhusu usumbufu huu wanaotusababishia vijana tusakao ajira.

Point yangu hapa ni kwamba sipingi suala la kusetifai vyeti ila kinachotakiwa ni kwamba muhakikishie kwanza mtu ajira kisha ndo umpe hayo maelekezo na blabla zinginezo.Sio kijana anapoteza pesa yake mwisho wa siku hata ajira yenyewe hamumpi.

Ma HR jitahidini kuwa mnafikiria kwanza kabla hamjatoa tangazo la ajira,waiteni kwanza watu muwafanyie usaili na watakaopita ndo muwaelekeze chakufanya kuliko kuleta usumbufu kwa vijana kabla hata ajira zenyewe hamjawapa.

Ni hayo tu
 
me kipengele cha five years work experince ndio kinanichoshaga asee
 
Back
Top Bottom