Kipele sehemu za ndani za siri

Susy

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
1,431
221
Nawasalimuni nyote!!

Wapendwa nina zaidi ya miaka nane nina kipele kidogo sana mfano wa chunusi ambacho mpaka nijishike mwenyewe ndio nijue kama kuna kipele. Kipele hicho nimekaanacho takribani ss miaka 8, hapo awali sikudhani kama ni shida na niliona ni hali tu ya kawaida, ila kwa ss nasikia kama kinavuta, nimekwenda hospitali nimepewa dawa mbali mbali, mpk ss nimechoka maana kila niikieenda hospitali mpaka nimtanulie dr. anitie vidole naye aangalie.

Naombeni msaada wenu.
 
Pole Susy,nenda kafanye uchunguzi,yaweza kuwa warts,wanakata tu na kuchoma,mzigo unakuondoka.Kama uko dar nenda Tumaini Hospital!
 
Thanks Dyslexia

You are welcome! Hilo ndo tatizo,haichukui muda,warts mara nyindi haziumi ila zinakukoseha raha,inakuwa kama ka mchele fulani,wanakata muda mfupi sana na kuchoma,unapewa dawa ya kusafisha,baada ya muda siku tatu,uko ok!
 
Kipele chenyewe ukigusa kinauma? na je kipo upande wa ndani wa labia (lips)?
Kama ndio inaweza ikawa bartholin's cyst. Hii cyst itatikiwa ichanwe kuwa wazi, utapewa antibiotics, na ili isirudie, inabidi upunguze kuoshaosha. Zinawapata sana watu wanaokuwa wanaosha sana-yaani usafi uliokithiri kiasi cha kuondoa benefical microorganims.

Nawasalimuni nyote!!

Wapendwa nina zaidi ya miaka nane nina kipele kidogo sana mfano wa chunusi ambacho mpaka nijishike mwenyewe ndio nijue kama kuna kipele. Kipele hicho nimekaanacho takribani ss miaka 8, hapo awali sikudhani kama ni shida na niliona ni hali tu ya kawaida, ila kwa ss nasikia kama kinavuta, nimekwenda hospitali nimepewa dawa mbali mbali, mpk ss nimechoka maana kila niikieenda hospitali mpaka nimtanulie dr. anitie vidole naye aangalie.

Naombeni msaada wenu.
 
Nanren
Ni ndani kabisa ya uke, na mpaka uingize kidole cha kati kiingie nusu ndio unaweza kukikuta, na kilinipata miaka 8 iliyopita ambapo sikujua maana hata ya kujisafisha sanaa kama ss nilivyo, hakiumi hata kidogo, hata siwezi wakati mwingine kuhisi kama ninakipele mpaka wakati nanawa, ila ss nimeanza kukisikia kama kinavuta mara moja moja kama vile ni ganzi fulani, yaani sijui nikueleezee vipi unielewe, lakini natumai umenisoma.

Zaidi ya yote nashukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi, be blessed
 
Poa, nimekusoma kinamna.
Ina maana hiyo sio bartholin cyst.
Lakini pia nahisi haiwezi kuwa Genital wart- especially kwa kuwa ipo miaka mingi na haikupi tabu, na ninaamini hujawahi kuambukizwa STD.

Labda uendelee kukaa nayo inaweza kutoweka yenyewe taratibu. Ngoja pia tusikilize na wataalam wengine.

Cheers

Nanren
Ni ndani kabisa ya uke, na mpaka uingize kidole cha kati kiingie nusu ndio unaweza kukikuta, na kilinipata miaka 8 iliyopita ambapo sikujua maana hata ya kujisafisha sanaa kama ss nilivyo, hakiumi hata kidogo, hata siwezi wakati mwingine kuhisi kama ninakipele mpaka wakati nanawa, ila ss nimeanza kukisikia kama kinavuta mara moja moja kama vile ni ganzi fulani, yaani sijui nikueleezee vipi unielewe, lakini natumai umenisoma.

Zaidi ya yote nashukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi, be blessed
 
Hiyo yaweza kuwa warts, mara nyingi warts haziumi ila ukiwa unashikashika kinaweza uma kwa mbali sana. Sasa naomba ukiache tu forget it, think like your normal haitasumbua afta all hakionekani. Usiwe na obssesiòn ya kukishika kitakupa shida. Kuna mtu kashauri kuwa waweza kata sasa warts ukikata sometime zaweza geuka cancer. Nilikuwa na mama yangu mkubwa alikuwa na wart begani kilikuwa hakina shida, aliamua kukata baadaye alidevelop skin cancer. Warts zinasababishwa na human papiloma virus sometime zinaweza sababisha cancer. Google human papiloma virus jifunze zaidi.
 
Thanks Dr G, ingawa umeniogopesha sana!! nilikua nakula nimeshindwa kuendelea kula!!
 
Usiogope susy, we just take it easy na forget it if you have anything abnormal ukiendelea kushika kinaweza kuwa infected. Lakin kama kinakuletea shida au kinakua haraka na kuwa kikubwa usisite kwenda hospitali au ni PM.
 
Kwa niaba ya Susy nasema ahsante kwa nyote mnaojitahidi kutoa ushauri mbalimbali na kuelimisha. Hata sisi wengine tunajifunza humuhumu... kweli elimu haina mwisho.. Thanks guys!
 
Nawasalimuni nyote!!

Wapendwa nina zaidi ya miaka nane nina kipele kidogo sana mfano wa chunusi ambacho mpaka nijishike mwenyewe ndio nijue kama kuna kipele. Kipele hicho nimekaanacho takribani ss miaka 8, hapo awali sikudhani kama ni shida na niliona ni hali tu ya kawaida, ila kwa ss nasikia kama kinavuta, nimekwenda hospitali nimepewa dawa mbali mbali, mpk ss nimechoka maana kila niikieenda hospitali mpaka nimtanulie dr. anitie vidole naye aangalie.

Naombeni msaada wenu.

Duh!
 
Dr G, nashukuru kwa kunitia moyo!! ubarikiwe sana!!

SUWI tupo pamoja!!
 
Susy nenda umuone Gynaecologist kama ulivyoshauriwa pale Tumaini Hospital. Hiyo ni cyst na tiba yake ni kukipasua na kuondoa kilicho ndani, . ukiamua kunywa dawa utakunywa nyingi bila mafanikio.
 
Hi susy ulisha solve problem! mwenzawangu naona anatatizo kama lako; nitashukuru kama utatupa feedback hapa!
 
Suzy Pole, nimesoma ushauri wa watu mbali mbali, kila mtu anafikiri kivyake na hiyo ndio medicine, u can have a lot of differential diagnoses.

Mimi sidhani sana kama ni Bartholin's cyst kwa kuwa yenyewe usingekaa nayo for 8 years, lazima ingekusumbua na pia hiyo cyst huwa haiko ndani sana huwa kama 0.5 to 1cm inside the vagina from the introitus, na ile huwa inakuwa with time, na huweza kukua na hata kuonekana imevimbe kwa nje kwenye labium majus.

Umewahi kushika Cervix yako? Nimeshawahi kupata complaint ya mtu akidai ana uvimbe ndani ukeni lakini ilikuwa ni cervix, alipoigusa kwa mara ya kwanza akajua ni uvimbe. Jaribu kujichunguza vizuri some people do confuse the cervix with a mass or a nodule na utajicheka ukigundua hicho unachodhani ni kijipele kikajakuwa ni maumbile yako ya kawaida.

Sidhani pia kama ni warts kwani zenyewe mara nyingi huwa zinakuwa nje zaidi kwenye perineum kuliko ndani unless ziwe very extensive. Na huwa zinakuwa na feel fulani rough unapokashika sijui zako zikoje. Ni kweli Warts zinasababishwa na virusi aina ya HPV type 6 and 11 in 90% of patients, virusi hivi havisababishi cancer, vinavyosababisha cancer ni virusi vya HPV type 16 and 18 and others ambavyo vinasababisha cervical cancer, kwa hiyo hata kama ni warts usihofu haiwezi kuwa cancer baadaaye.

Daktari aliyekupa dawa alikwambia shida ni nini? Kama unawasiwasi sana u better see a gynaecologist atakutoa huo wasiwasi
 
Follow this advice!
This is purely an advice from a health personnel, not from a person surfing from the internet. Fuata ushauri huu, labda kama unataka kuendeleza mada.
 
Back
Top Bottom