SoC01 Kipato duni na Ugonjwa wa UVIKO - 19 (COVID-19)

Stories of Change - 2021 Competition

TechTino

Member
Oct 16, 2016
71
25
wBJVA_bJ6XjhRsU4gmtZLLS9kh8QJ4xXzkRDeKVU76zRygeFspSDCb2Fc9MWbmOzdGmZmFPJSxzyP8MsCMzGWZQlbq8eIrCq2VWWtVwoNI1mqyWjvPQ9TxSisBDq6mQfkPlR7RxY

UMASKINI NA UVIKO-19 (COVID -19)

Athari za janga hili kwa umaskini hutegemea kwa sababu kadhaa. Kuongeza usawa na kupungua zaidi kwa ukuaji wa uchumi inaweza kusukuma watu zaidi katika umaskini. Janga hili pia linatoa changamoto kwa serikali , uwezo wa kifedha ambao ulikuwa tayari umebana kabla ya janga na kama idadi ya kuongezeka kwa maambukizi na kubaki kufungiwa, kwa maskini na watu hali ya chini itazidi kuwa magumu . Bila mapato na ajira, ikiwa hali ya janga inaendelea, kuna uwezekano mkubwa kwa watu wa hali ya chini kuendelea kuambukizwa kwasababu hutafuta mapato la kujikimu kwa kila siku .

  • Pamoja na hatari kubwa ya kiafya inayosababishwa na janga la gonjwa hili, hatua za kuzuiwa kutoka nje hasa kwa baadhi ya inchi za Afrika Mashariki zilizo wekwa na serikali kupunguza maambukizi zimekuwa na madhara ya kupitiliza kwa watu , kuongeza umaskini, chuki dhidi ya wageni na kusababisha masuala mapya ya ulinzi wa kibinadamu. Katika hizo inchi za Afrika Tanzania ni moja wapo japo katazo la kutoka inje halipo lakini bado kuna changamoto nyingi ikiwemo ndani ya inchi na mipakani ikiwemo wafanyabiashara na madereva kukaa muda mrefu mipakani kusubili vipimo huku baadhi ya bidhaa zikiharibika.

MADHARA KUTOKANA NA MLIPUKO WA UVIKO 19 KWA MASKINI

  • Upotevu wa kipato kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19 (COVID-19) unaweza kuwaweka watu wanaokimbia makazi yao ambao wanaishi kwenye nyumba za kukodi katika hatari kubwa ya kufukuzwa na uwezekano watu hao wakalazimika kusafiri au kuhama pamoja na watu wengine, na kuzidisha hatari ya maambukizi.

  • Kwa ugonjwa unao ambukiza kama UVIKO-19, kufuata mapendekezo ya kujikinga, ikiwemo kunawa mikono kila mara, kutosogelena na mtu, na kukaa nyumbani ukiwa mgonjwa, inaweza kuwa vigumu kwa baadhi ya watu kutokana na maisha ya kutafuta pesa ya kula kila siku.Pia gharama ya vipukusu ni changamoto kwa watu wa hari ya chini kiuchumi.

  • Kutokana na muktadha huu wa mzigo mdogo wa visa vya UVIKO-19 lakini kutumika nguvu kubwa za hatua za uzuiaji, mazingira makuu hatarishi yaliyopo hadi hivi leo yametokana na kufungwa mipaka, makatazo ya kusafiri, uvurugaji wa biashara na masomo shuleni, makatazo ya mikusanyiko mikubwa, amri ya kukaa ndani na kutotoka nje,mjumuisho wa hatua zinazozuia kutembea na zinazorejelewa kwa pamoja kama ‘marufuku ya kutoka nje’ (lockdown).

  • Duniani kote, watu wenye umri mkubwa na wale wenye matatizo mengine ya kiafya kama ugonjwa wa moyo, kisukari, matatizo sugu ya mfumo wa upumuaji, na saratani wana uwezekano zaidi wa kuwa na maradhi makali yatokanayo na UVIKO-19 na kufa kwa ugonjwa huo. Wengi wa watu wanaoishi hasa maeneo ya mijini hasa vijana wanaishi katika nyumba za kupanga na wengi huwa na mtindo wa kuhamahama kutokana na kutafuta maisha bora hivyo, wanakabiliwa na hatari za ziada za ugonjwa mkali kwa sababu ya mwingiliano wa UVIKO-19 na magonjwa mengine yanayosababisha vifo. Haya yanajumuisha magonjwa yasiyoambukiza kwa njia ya hewa kama vile shinikizo la juu la damu na kisukari ambayo mara nyingi yanaathiri watu wa kipato cha chini kuliko wa kipato cha juu, huku kukiwa na fursa ndogo ya matibabu, pamoja na lishe duni, kifua kikuu na VVU. Utapiamlo na lishe duni, ambao umeenea zaidi miongoni mwa vijana na watu wazima.
  • Ugumu wa kufikia na kufungwa kwa vituo vya afya hasa kwa maeneo ya vijiji kumekuwa na changamoto ya miundombini ya kufikika kwenye vituo vya afya.
  • Afya ya Akili , Athari za kisaikolojia kutokana na kutofanya kazi, kuto kwenda shule au kutofikia huduma za afya kwa sababu ya UVIKO-19, kuhisi kutengwa na wengine, vizuizi vya kutembea pamoja na unyanyapaa na ukatili unaohusiana na kutii amri zinaweza kuongeza hofu, huzuni na aina nyingine za fadhaa ambazo watu waliokatika maisha magumu yaweza kuwa hatari kubwa zaidi na kupata msongo wa mawazo.

  • Hatari kwa watoto katika mazingira ya vituo vya malezi ni kufungwa ghafla kwa makao na watoto kurudishwa kwenye familia na katika jamii zao bila maandalizi ya kutosha. Hatari zinaweza pia kusababishwa kwa watoto kubaki katika makao ambapo mazingira ya watu wengi yanaweza kurahisisha kuenea kwa ugonjwa na kuwaathiri watoto wanaoishi humo huku wakiwa katika hatari kubwa ya unyanyasaji, kupuuzwa na unyonyaji. Hii ni hatari kubwa hasa kwa watoto wenye ulemavu, ambao wana uwezekano mkubwa wa kuwa katika makao na katika hali zingine wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa UVIKO-19 na kuathirika zaidi.

  • Katika maeneo mengi ya Tanzaniai, watu wa vijijini wakiwemo huwa wanahofia wageni wakiwemo wafanyakazi wa mashirika ya misaada na watu kutoka miji mikuu wakiwemo wanasiasa kama waambukizaji sugu wa UVIKO-19. Kwa watu hawa wanaotoka katika daraja la watu wenye uwezo mkubwa na hata nyadhifa za mamlaka katika mwitikio dhidi ya UVIKO-19, hawako katika hatari sana ya kunyanyapaliwa na kutengwa na jamii. Badala yake, hofu ya watu wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa katika mazingira haya inaweza zaidi kuchukua taswira ya kugomea hatua za afya ya umma na jumbe za kisiasa, kwa kuendeleza malalamiko ya siku nyingi kuhusu walio nacho na wasio nacho, kukosekana kwa usawa wa kimapato na kutoshirikishwa katika maamuzi ya kitaifa.

  • Vijana wengi wa Tanzania wanategemea ajira isiyo na uhakika na isiyo rasmi kuliko watu ambao wako katika ajira lasmi, wanategemea ujira wa kila siku ili kujikimu, ili kupata akiba kidogo, Ugonjwa huu umeleta changamoto kubwa kwenye kipato cha kila siku na kupunguza mzunguko wa kifedha pia hata ambao wako katika ajira lasmi bado hawako salama kwakuwa baadhi ya Kampuni zimekuwa zikipunguza idadi wa ya wafanyakazi kutokana na mdololo wa kiuchumi.

  • Machafuko yanayosababishwa na UVIKO-19 pamoja na hatua zinazochukuliwa kuzuia ugonjwa huo huathiri watoto, familia na mazingira kwa ujumla. Hatua za dharura za kukabiliana na ugonjwa huu hupelekea kufungwa kwa baadhi ya huduma za kijamii na kusababisha utegemezi kwa kiasi kikubwa hasa kwa wale ambao ni tegemezi tayari. Familia zenye mazingira yanayoainishwa na hali ya umaskini au rasilimali duni zitalemewa zaidi na mikakati inayochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huu kama vile zuio la kutembea na matumizi ya usafiri wa umma na hivyo kusababisha watu kukosa ajira au kuwa na kipato duni, kufungwa kwa shule, upatikanaji duni wa huduma na msaada wa kijamii, janga la njaa na hali ya kutengwa na jamii. Mazingira ya nyumbani yenye msongo wa mawazo yanaongeza uwezekano wa unyanyasaji wa kijinsia majumbani, pamoja na migogoro ya kifamilia, unyanyasaji na machafuko baina ya watu.

  • Kuzolota kwa uhusiano wa kidiplomasia hasa kwa inchi masikini na zinazoenda na inchi za bala la ulaya, kama tunavyoshuhudia mpaka sasa ni baadhi tu ya inchi za afrika ambazo tayari zimepatiwa dozi ya chanjo ya kutosha ili kukinga na kudhibiti kuenea kwa maambukizo ya ugonjwa huu , hili limeleta mgawanyo na upendeleo wa mataifa baadhi kutokuwa na nguvu na uwezo wa kupata dawa au kutengeneza chanjo kwa viwanda vya ndani vya inchi hasa za kiafrika.

WAJIBU WA JAMII NA SERIKALI KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA HUU WA UVIKO-19

  • Uimarishaji na upanuzi wa miundombinu ya maji, usafi wa mazingira na usafi binafsi , ujengaji wa vituo vya kunawia mikono kwenye maeneo ya jumuiya (sokoni, vituo vya afya, malango ya makazi) na kuongeza usambazaji wa maji na sabuni kwenye masoko na hospitari au mahali penye mikunyaniyiko ya watu mara kwa mara kama nyumba za ibada.

  • Unaweza kuwa salama kwa kupunguza idadi ya watu unaotangamana nao usioishi nao na kwa kuzingatia mikakati muhimu ya usafi kila inapowezekana ili kupunguza kuenea kwa virusi vya korona. Wakiwemo watu wa umri mbalimbali, hata ikiwa huna dalili zozote au mamatizo mengine ya afya.

  • Kutumia usafiri wa umma , Usitumie usafiri wa umma kila inapowezekana na ujaribu kusafiri kwa baiskeli, kutembea au kwa gari lako. Ikiwa unahitaji kutumia usafiri wa umma, usisafiri wakati kuna wasafiri wengi na ukae mbali na watu wengine. Sharti uvae barakoa unapotumia usafiri wa umma.

  • Kuendelea na kazi , Unapaswa kuendelea kufanyia kazi nyumbani ikiwezekana. Ikiwa ungependa kwenda kazini, sharti kwanza uhakikishe kuwa wewe na wanafamilia wako hamna dalili za maambukizi. Ikiwa hakuna yeyote aliye na dalili, unaweza kwenda kazini mradi udumishe umbali wa mita 2 kati yako na watu wengine na kunawa mikono au kutumia kipukusi mara kwa mara.

  • Polisi na wanajeshi wanaweza kuhusika katika kutekeleza mikakati ya afya ya umma na pia kuhakikisha kuwa chakula na bidhaa nyingine muhimu zimewafikia watu wanaothirika pakubwa.

  • Ikiwa unaonesha kuwa unadalili za maambukizi , jitenge kaa nyumbani kwa muda wa angalau siku 14 na uzingatie mwongozo wa kujitenga wa familia zilizo na uwezekano wa kuambukizwa virusi vya korona. Mwanafamilia au yeyote aliyetangamana nawe kwa karibu sharti ajitenge kwa muda wa siku 14 huku taratibu za kupimwa virusi vya UVIKO-19 ndani ya siku tano za kwanza za kuonyesha dalili.

  • Kohoa au piga chafya kwa usahihi , funika pua na mdomo kwa kutumia tishu au kohoa na kupiga chafya ndani ya kiwiko cha mkono.

  • Nawa mikono kwa sabuni na maji tiririka , Safisha katikati ya kiganja, vidole na kucha, hadi kwenye kiungio cha mkono.

  • Epuka kugusa mdomo, pua na macho yako , usiguse uso kwa kutumia kiganja, kwa maana virusi vya UVIKO-19 huingia kupitia kinywa, pua na macho.

  • Epuka maeneo yenye watu wengi, na punguza mawasiliano ya kimwili , Hata walio athirika ambao wanahisi wana afya njema, wanaweza kuambukiza wengine , epuka kukumbatiana, kubusiana na kushikana mikono.
 
Back
Top Bottom