Kipanya aibuka na Mawaziri baada ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan kuanza kazi

Mama kaanza vizuri sana. Ila kwa wanaomjua Mama hawakuwa na shaka tangu yalipotokea ya kutokea kuwa sasa Mungu ametupendelea hasa. Kwa kweli tunamshkuru Mungu sana kwa huyu Mama. Ni kwa neema zake tu aliye juu.
Mungu ana ukuu wake pia, kila kitu hutokea kwa sababu. Tuliwaza sana ataweza kuliendeleza vyema Taifa, hatimaye IMANI thabiti inarudi kwa bashasha. RIP hayati Magufuli karibu Mama Samia.
 
Ila watanzania hatuna tofauti na vinyonga bila kusahau nyumbu. Kila awamu huwa ainakuja kasi mno mnashangilia weeee baadae ikianza kupoa au kutotimiza kiu yenu mnakumbuka ndo mnaanza kukumbuka uwepo wa CCM
Kwisha habari zenu MATAGA
 
Hakika leo hii imekuwa ni Jumapili njema maishani tangu mwaka 2015 sijawahi kupata siku mzuri na njema na yenye matumaini kama leo.

Hapa chini ni picha iliyo tolewa na Kipanya akionesha mitazamo ya baadhi ya mawaziri wetu wa baraza lililokuwa chini ya marehemu Magufuli.


Hongera sana mama yetu mh Samia tupo nawe kwenye mapambano ya kusafisha nchi yetu.
Huyu kashapaki mabegi...mamaee..
 
Na Jafo naye aende kabisa kariakoo atafute kabisa begi maana kwa yale maneno ya busara ya mama yetu lazima ajiulize

Binafsi jaffo nampenda kwa uchapaji wa kazi ila alikuja nitibua alipoanza ku rap matibabu ya kujifukiza nyungu. Pilipili, limao , vitunguu saumu utafikiri wote tunatoka mzenga?
 
MATAGA mlitupigia sana kelele....
Zikaneni wenyewe sasa.
 
Da! Maisha bana siamini macho yangu leo hii nasoma humu JF nakuta tunamuongelea Rais Magufuli a.k.a Jiwe kama Marehemu

Maisha ya mwanadamu siku zote unapokwenda ni pafupi kuliko ulipotoka tusijisahau kujitambua kwanini Mungu alituumba, tukumbuke maisha yetu ni mafupi sana
Kuna watu walitamka kuwa mwendazake atake asitake lazima wamuongezee 5tena walisahau uwepo.wa Mungu
 
Binafsi jaffo nampenda kwa uchapaji wa kazi ila alikuja nitibua alipoanza ku rap matibabu ya kujifukiza nyungu. Pilipili, limao , vitunguu saumu utafikiri wote tunatoka mzenga?
Mkuu pale alikuwa anapiga zumari kwa mteuzi wake hivyo nakuwa na jinsi.
 
😀😀😀😀

Waongo mna maneno nimecheka hii mipasho yenu humu dah.
 
Back
Top Bottom