Kipandauso (migraine): Chanzo, Dalili, Tiba na jinsi ya kujikinga na tatizo hili

Nashukuru kwa ufafanuzi ndugu, mimi ninachelewa kupata usingizi, kwa hiyo ninalala masaa 6-7, umri wangu ni miaka 28, maji nina kunywa lita 1.5 kwa siku, choo ninapata vizuri, lakini wakati mwingine nahisi ganzi ubongo wa nyuma hivyo napoteza kumbukumbu na kukosa hisia au mguso wa matikio na kuchelewa sana kuhisi uhalisia wa tukio lolote mfano kams ninapata taarifa ya kuhuzunisha au kufurahisha nachelewa sana kupata mguso huo, wakati mwingine ni kama sina nerve senses
 
Nashukuru kwa ufafanuzi ndugu, mimi ninachelewa kupata usingizi, kwa hiyo ninalala masaa 6-7, umri wangu ni miaka 28, maji nina kunywa lita 1.5 kwa siku, choo ninapata vizuri, lakini wakati mwingine nahisi ganzi ubongo wa nyuma hivyo napoteza kumbukumbu na kukosa hisia au mguso wa matikio na kuchelewa sana kuhisi uhalisia wa tukio lolote mfano kams ninapata taarifa ya kuhuzunisha au kufurahisha nachelewa sana kupata mguso huo, wakati mwingine ni kama sina nerve senses
Kuto kulala masaa 8 ndio kunako sababisha wewe upate maradhi yako ya kichwa jitahidi ulale mapema ndio kichwa kitapona deezekiels
 
Last edited by a moderator:
Huu ugonjwa upo sana na utambuzi wake ni mgumu. Naomba kupata empirical data na evidence kuhusu kipandauso pamoja na dawa (za kienyeji na kisasa) pamoja na wapi matibabu yanapatikana. Kuna mdau anahisi anacho.





====== Majibu kutoka kwa Mzizi Mkavu ======


Dah me mwenyewe nnalo hilo tatizo
 
Kama tatizo ni kipanda uso dawa ni mafuta ya habasoda wengi yamewasaidia.kwa watu wa kigoma kuna majan yanatambaa jina siyajui mizizi yake inafikichwa unainusa hutaumwa tena kipanda uso.
 
Habari wana JF wenzangu,

Nasumbuliwa sana na kichwa (kipandauso). Kiauma sanaa hadi nashindwa kutoka kitandani wiki ya 3 sasa inaisha. Kinauma hasa upande wa kulia hadi jicho linauma mno. Nilienda hsptl nikapewa dawa nimemaliza dozi wapii,naamka vizuri ikifika jioni kinaanza kuuma. Nisaidieni nini dawa yake?
 
Habari wana JF wenzangu, nasumbuliwa sana na kichwa (kipandauso). Kiauma sanaa hadi nashindwa kutoka kitandani wiki ya 3 sasa inaisha. Kinauma hasa upande wa kulia hadi jicho linauma mno. Nilienda hsptl nikapewa dawa nimemaliza dozi wapii, naamka vizuri ikifika jioni kinaanza kuuma. Nisaidieni nini dawa yake?

Tumia tangawizi mimi ilinisaidia sana, chukua kipande cha tangawizi twanga chemsha na maji. Kunywa. Fanya asubui mchana na usiku kabla hujaenda kulala.. Na kuhakikishia baada ya siku mbili kitakuwa kimeacha kabisa..

Ila tahadhari usizidishe sana tangawizi,, isiwe kali sana mpaka kuumiza utumbo wako. Hakikisha wastani wa tangawizi na maji unaendana.

Vitunguu swaumu pia ni dawa nzuri,, chukua vipunge kama vitatu au vinne vimenye vitafune au katakata vipande vidogo na kunywa na maji mengi.. Mimi hufanya hivyo na imenisaidia sana. Fanya hivi mara mbili asubui na jioni wakati unaenda kulala. Au kama unaogopa harufu tumia usiku tuu wakti unaenda kulala. Bila kusahau kunywa maji kwa wingi.
 
Mimi ninaifahamu dawa ya kipanda uso ila niyakienyeji nimesha watibu wengi na wamepona alinionesha bibi yangu na nikajaribu kwa watu kama kumi ikawasaidia ni mmea fulan unapatikana mbinga mkoani ruvuma ila kwa sasa ninaishi dodoma na kwa kule kwetu mbinga hilo ni tatizo dogo maana linatibika vizuri na wengi wanazijua dawa tofauti ila za miti shamba kwa dodoma niliko sasa limekua ni tatizo jaribu kuwasiliana na watu wa mbinga
 
Jamani nimesumbuliwa na hili TATIZO wengine wanasema NI kawaida kwa watu tuliozaliwa October wengine wanasema nawaza sana wengine nimerogwa dawa HAMNA naishia Kunywa vidonge vya kupunguza maumivu tu..vasograin,toka olevo 2006 mpk saiv kwa Mwaka lazima nipate attack ,kuna dawa ya KUDUMU jamani,sio za kishirikina LKN mm NI mtu wa imani
 
Epuka kula vyakula vinavyopelekea blood pressure kushuka eg ndizi za kuchemsha, madafu nk. pia usipendelee kukaa maeneo yenye joto kali.
 
Kapime kipimo cha kichwa kinaitwa EEG PCMC clinic upanga karibu na Muhimbili watakusaidia
 
Kichwa kinaumaje? Sonona (depression); anxiety na hasa PTSD ni matatizo ya kisaikologia yanayosababisha kichwa kuuma na bila tatizo la kimwili kuwepo! Muone psychiatrist au clinical psychologist hao watu wanaweza saidia!pole sana
 
Hata dada yng ana miaka 10 anaumwa kichwa mpaka analia machozi!! tumemaliza hispital zote mpaka muhimbili hana tatizo lililoonekana.
 
Pole bro. Ila tembelea kanisa la kisabato lilikaribu nao waeleze watakusaidia kupata ufumbuz wa tatizo
 
Back
Top Bottom