Kipaji ni silaha tosha kutoka kimaisha,usiichezee!

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Maisha ya binadamu yana njia nying sana ya kumtoa kimaisha.Tunapaswa kujua ni wapi pakutokea na sio kukalili tu mafundisho ya wazazi kuwa soma mwanangu kwa bidii upate alama za juu uwe wa kwanza darasani.

Maisha hayapo hivyo,na sipo hapa kukosoa mafundisho ya wazazi la hasha!

Binadamu anaweza tumia KIPAJI chake na kufanikiwa kuwa mtu maarufu na mwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yake na akawa msaada mkubwa sana kwa wenzake.

Kipaji ni kitu ambacho kinapaswa kuendelezwa na sio kukandamizwa kwa kisingizio cha shule.Vipaji na shule vinapaswa viende pamoja.

Ikitokea kwa namna moja au nyingine isiyozuilika kuendeleza kipaji na shule pamoja ni uamuzi wa busara kabisa unapaswa kuchukuliwa kuendelea na kimoja.

Ni kweli elimu ni ufunguo wa maisha ila ni maisha gani hayo hufunguliwa na elimu?

Je ni elimu ya namna gani inatosha kabisa kutambulika kama ni ufunguo wa maisha?Form 4?Form 6? Bachelor? Masters? PHD?

Dunia imepitia hatua kadhaa mpaka kufika hapa ilipo sasa na kwa namna moja ama nyingine tunaweza sema michango ya wasomi na wasio wasomi(ndio wengi) imetufikisha hapa tulipo leo hivyo ambao hawajasoma wasibezwe kabisa.

Kipaji ni kipawa ambacho mtu hupewa na mungu wake.Kipaji ni silaha tosha kabisa katika kufanikiwa kimaisha.Unapaswa kama kijana kutambua kipaji chako ni kipi ukiendeleze maana ndio silaha yako tosha kabisa

Ni wangapi tumewasikia hawajasoma ila wametoka kimaisha kwa kuimba tu? Ni wangapi wapo ulaya wanacheza mpira na wanapata kipato kikubwa ila walifeli shule?

Kipaji huanza kutambulika mapema kabisa mtu akiwa bado mtoto mdogo.Ila ni wangapi leo hii ni mashuhuda kuwa wazazi wanawakataza watoto wasicheze mpira wasome ? Ni wangapi wanashuhudia vikundi vya kuziki shule wakichukuliwa kama ni wahuni?

Maisha yana njia nyingi ya kufanikiwa ila njia kubwa ni kipaji!

Usikibeze kipaji chako ulichonacho

HAWA NI WASANII WA MAREKANI WALIOENDELEA KIMAISHA KUTOKANA NA MUZIKI TU


1. Herb Alpert
Huyu ndio msanii tajiri zaidi duniani.

Herb-Alpert-Richest-American-Musicians-2017.jpg

Herbert Alpert alizaliwa 31st March 1935,ni raia wa USA.Anaeleza kuwa alianza kujishughulisha na muziki akiwa na miaka 8.Anautajiri wa Dollar Million 900 ambazo ni sawa na Tsh Trillion 2 na billion 7 na million 240.

Si kingine bali ni kipaji tu ndio kimemuweka hapo alipo.

Sasa endelea kumlazimisha mwanao aende shule na akirudi aende tuition kwa kuamini kipaji kinalazimishwa


2. Dr. Dre

Dr.-Dre-Richest-American-Musicians-2016.jpg

Anashikilia namba mbili akiwa na utajili wa dollar $650 Million mpaka $800 ambazo ni sawa na Tsh trillion 1 na billion 784 na uchafu achafu wa million 210

Endelea tu kuamkataza mwanao asijiunge na makundi ya hiphop kwa kumwambia ni uhuni.


3. Madonna
Madonna-Richest-American-Musicians-2016.jpg


Madonna anashikilia record ya kuwa msanii wa kike tajiri zaidi duniani.Pia ni muimbaji,dancer,mjasilia mali na muigizaji.Vyote hivyo ni vipaji vyake.Madonna pia anajulikana kama "Queen of pops" na mfalme wake ni Michael Jackson RIP
Anakadiliwa kuwa na utajiri wa $520 -$800 Million

Sasa wee mzazi endelea kumkataza mtoto wako wa kike asijiingize kwenye makundi ya wanaume wanaoimba ukiamini wata...

4. Sean Combs

Sean-Combs-Richest-American-Musicians-2017.jpg


PUFF DADY,Puff Daddy, Puffy, Diddy, na P. Diddy yote haya ni majina yake
Anakadiliwa kuwa na utajiri wa $640 million mpaka $700 million.

5. Celine Dion
Celine-Dion-Richest-American-Musicians-2018.jpg


Anakadiliwa kuwa na utajiri wa $630 million.
Alianza kujulikana katika tasnia ya muziki akiwa na miaka 12 tu.

Endelea kuamini kuwa mafanikio kama haya yanaweza kupatikana kupitia shule.




6. Jay-Z
Jay-Z-Richest-American-Musicians-2018.jpg


Anatajwa kuwa na utajiri wa $510 million mpaka $560 million.

Endelea kumwambia mwanao asome kwa bidii

7. Britney Spears
Britney-Spears-Richest-American-Musicians-2017.jpg


Akiwa na miaka 18 aliweza kujulikana dunia nzima(Kasoma saa ngapi??)

Anakadiriwa kuwa na utajili wa $500 million.

Wewe kama mzazi endelea tu kumnyima mwanao nafasi ya kukuza kipaji chake kwa sababu ya elimu

8. Beyoncé
Beyonc%C3%A9-Richest-American-Musicians-2016.jpg


Anautajiri wa $450 million.
(Akiwa na miaka 16 walianzisha kundi maarufu zaidi la R n B linalojulikana kama Destiny Child )
-Kundi zima walikuwa na miaka 16 na ndio kundi bora kabisa la wanawake katika uso wa dunia kimziki mpaka leo

-Endelea tu kumfungia binti yako ndani asome

9. Mariah Carey
Mariah-Carey-Richest-American-Musicians-2017.jpg


Anakadiriwa kuwa na utajili wa $520 million
Ameweka record ya kuwa msanii wa kike aliyeweka aliyeuza albamu nyingi tangu kuundwa kwa ulimwengu.Kwa kingereza anajulikana kama " best-selling female artist of the millennium in 2000"

10. Master P
Master-P-Richest-American-Musicians-2018.jpg


Anautajiri wa $375 million

HAWA SHULE WALIENDA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU.SASA WEE KAMA MZAZI ENDELEA KUMLAZIMISHA MWANAO MAMBO AMBAYO HAYAPENDI ILI ATOKE KIMAISHA

 
F

hakihitajiki

Sasa kilichokushinda wewe ni nini mkuu!??

Hata hivyo, twashukuru kwa taarifa na kejeli kwetu wazazi. Shida ni kila nikisoma sentensi nakutana na huo mchanganyiko wa L na R unaharibu kabisa mvuto wa mada.
 
Sasa kilichokushinda wewe ni nini mkuu!??

Hata hivyo, twashukuru kwa taarifa na kejeli kwetu wazazi. Shida ni kila nikisoma sentensi nakutana na huo mchanganyiko wa L na R unaharibu kabisa mvuto wa mada.
Wapi umeona R na L zimechanganywa?
 
Sasa kilichokushinda wewe ni nini mkuu!??

Hata hivyo, twashukuru kwa taarifa na kejeli kwetu wazazi. Shida ni kila nikisoma sentensi nakutana na huo mchanganyiko wa L na R unaharibu kabisa mvuto wa mada.
Kama kakosea mkosoe usilazimishe vituambavyo mashiko yake ni madogo sana, pia matumizi ya rl kwake sio kipaumbele.
 
Halafu najaribu kumuuliza ni wapi pamekosewa nirekebishe hajibu
Mimi sioni sababu ya wote kuwa wahandishi mfano huyo dada celline hata lugha kwake nishida lakn katufanyia mazuri mengi tu, bongo hatakama unawazo zuri unaweza kushidwa kulitoa ukiofia kuchambuliwa vitu vidogo,mwishowe tunachelewa sana kufika.
 
Dah.... Kipaji siyo kwenye sanaa na michezo tu .... Kipaji ni uwezo wa MTU kufanya jambo fulani kwa ubunifu wa hali ya juu......unaweza kuwa na kipaji cha soka....hisabati... surgery nk..nk
Tofauti kubwa ya vipaji hivi ni kwamba vipaji vya sanaa vinahitaji media ili usonge mbele wakati hivi vingine unasonga tu huku ukuhudumia watu bila hata kuwajua wala wenyewe kukujua
 
Wapi umeona R na L zimechanganywa?

Sikuwa nimeona hili...


Kama kakosea mkosoe usilazimishe vituambavyo mashiko yake ni madogo sana, pia matumizi ya rl kwake sio kipaumbele.

Ni kipaumbele cha lugha na ufasaha wa uandishi wa Kiswahili.

Halafu najaribu kumuuliza ni wapi pamekosewa nirekebishe hajibu

Ni sehemu nyingi sana. Kwa kuanza tafuta sehemu zote zilizotakiwa kuandikwa 'utajiri' uone umeandikaje.
 
Back
Top Bottom