KIPAJI CHANGU KIMEPOTEA

KIPAJI CHANGU KIMEPOTEA

dullydon

Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
81
Reaction score
31
Kipindi nilipokuwa mdogo miaka ya 90 na something, baba yangu mdogo alinichukua nikaanze shule ya msingi mkoani Iringa. Ilikuwa vijijini ambapo yeye aliku mratibu wa elimu kata.
Katika kijiji hicho nilikuwa rahisi kufahamika kwa sababu ndio mtoto pekee niliyekuwa natokea Dar es salaam. Hapakuwa na mtu kwenda au kutoka dar kwa kipindi kile.
Nilikuwa na vipaji kama vitatu, ambavyo ni uchoraji, uchekeshaji na mpira wa miguu.kati ya hiv mpira ndio ulinitawala ikafika kipindi sasa ikawa kero kwa mshua, walimu shuleni wakaniweka kwenye kundi la watoro sababu kama mwalimu hayupo basi na sisi darasani hatupo, ukichungulia dirishani unatuona waleeee tunakipiga. Ikawa easy kuwa identified darasani maana mwalimu akiingia tu naanza kuulizwa mimi.
Waliniita mbabe wa mpira na ikafika kipindi bila mimi basi darasa letu haliingizi timu. Nikawa nabebewa begi la shule nikiwa kwenye pitch la vumbi nafanya yangu na tena nilikuwa nguzo imara katika sehemu zote nne nikiwa na maana ya kipa, beki, kiungo kati, na mshambuliaji.nilishawahi kufunga magoli mengi mechi moja. Nilifunga goli 36 peke yangu katika ushindi wa goli 42 kwa 11 yaani kama rede vile.mechi hii tulicheza kwa muda wa masaa matatu bila refa.
Nadhani tulikuwa na mapafu zaidi ya mbwa. Bila shaka ni mimi pekee duniani niliyeweka rekodi hii ya mechi moja.nilishiriki umitashumta nikiwa darasa la tatu kwa fani ya hati ( mwandiko) lakini darasa la nne nikawa timu ya kata kwenye football.

Kufika tarafa nikakatwa jina la football sababu ya umri mdogo nikabaki kwenye uchoraji maana nilikuwa nacheza na minjemba enzi hizo kwa hatua hiyo.mwalimu mmoja ambae alikuwa kiongozi kwa tarafa yetu alinambia tumekukata sababu ya usalama wako kwa vile umri wako mdogo. Miaka akenda bado nikiwa shule ya msingi nikawa miongoni mwa wachezaji wa timu ya kijiji.
Secondry school nikarudi home dar nikasoma huku mpira ukawa chaguo la kwanza ambapo nilipokuwa form one nikawa kiongozi wa michezo ambapo kwenye shule hiyo ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza mambo ya mpira. Form two tulishiriki vyema kwenye ligi ya shule ambapo tuliingia final na form three. Siku hiyo nilikuwa hatari sana maana maana nje niliambiwa na demu wangu mtoto wa tanga kwamba baby piga mpira mwingi nipate kuchonga kwa hawa mashoga zangu huku nje na siku hiyo alikuwa kagombana na mwenzie. Vile vile kulikuwa na wanajeshi walikuwa wanatusubiri tumalize waingie wao wafanye mazoezi yao ya mpira huo wa miguu.
Mechi ilikuwa u/taifa b zamani kule nyuma. Tulishinda ushindi wa 2-1 goli la kwanza likiwekwa kimiani na chinga mmoja wa kuitwa Abdulrahmani na la pili nilipiga mie. Goli la chinga alipiga nyuzi zetu zile 90° ila la pili lilitoka mido ya kati ngoma ikapelekwa wing ya kulia kwa muha mmoja namkumbuka kwa jina la Lutale gilagiza nikamwambia kimbiza then imwage hapa kati, alichokifanya yeye sasa alikokota mara moja tu kisha akamwaga maji (cross) sasa ile klosi yake haikwenda juu kama nilivyotegemea, akaipiga usawa wa mapaja ikabidi nipige stop ya kwenda mbele sababu alidrible mara moja.
Wakati ngoma ipo njiani, beki wao nae akastop akawa anakuja mbele yangu. Kabla hajanifikia ile ngoma (mpira) ikafika na mimi nikanyanyua mguu usawa wa paja huku nikiangalia inapotoka nikaipress mbele ya beki huyu ambae kwa wakati huo alikuwa kashanifikia, so akapishana na mpira.
Nikachomoka huku nikisikia akitukana ," ah ......" Nilidrible moja ili kuuweka sawa mpira halafu nikaachia umeme mmoja mtakatifu sana wa chini chini ngoma kimiani nikasikia kelele za ajabu nje zikanipagawisha nikavua flana (jersey) nikawa naizungusha then jamaa mmoja anaitwa Kabanda akasema njoo hukuuuuu kundi likawa linanifata la timu yangu nikatupa jersey jukwaani wakanirukia ikawa shangwe na hapo hapo nikasikia sauti ya mtoto mzuri inawaka akaja kwenye vurugu pale akanirukia tukakumbatiana dah shida sana asee. Baada ya hapo nikamaliza form four shule nyingine nikazamia kuingia south afrika 2007 nikiwa na dream ya kukipiga kule. Safari ilikuwa kafiri kwasabu haikuwa na vibali tulizamia tukiwa 11 lakini mpaka sauzi tukafika watatu (3) wengine wote waliishia njiani na tulitumia takribani wiki mbili. Haikuwa rahisi kupata team kama nilivyokuwa nikidhania au jinsi bongo ilivyo. Kule kila kitu kiko kwenye utaratibu japo nilitaka nikakipige ajax cape town ya watoto. Life likachenji nikawa napiga issue tu za mtaani.
Kuna siku wabongo wa mtaan walikuwa wanacheza wenyewe kwa wenyewe.
Ilikuwa pretoria hiyo ngoma. Wabongo wa kutoka sunnyside na kutoka central pretoria. Hapo central kulikuwa na best angu mmoja ananijua balaa langu tangu Tz akanambia njoo nitakupa namba maana yeye alisema hawawezi kumwambia kitu. Ila yeye hakuwa mchezaji alikuwa kama katibu wa kizushi si unajua timu za masela tena?
Muda ukafika tukawa viwanja vya belle ombre ila katika first 11 yao sikuwepo na wala reserve hawakuniweka kisa eti sio mtu wa central so ushkaji pembeni. Jamaa yangu akashindwa kunitete wengi walimpinga. Mpira ukapigwa sana nikiwa jukwaani naangalia mpaka kufikia kama dk 30 tushapigwa 2-0. Ndani ya hizo dakika substution zilifanyika nne maana jamaa upepo wachezaji ulikata (mabishoo).
Second half dk ya 60 zikafanyika sub 4 nyingine na watu wa reserve wakaisha. Dk ya 62 ubao ukasomeka 3-0 nikaona yule aliyekuwa anachonga sana kwa timu yetu analalamika kutoka upepo nae unakata afu kaona ishakuwa 'isambe'.
Nikasikia akisema "oyaa hakuna mwingine aingie?wakasema sub imeisha akasema hata kama kuna mshabiki anaweza avae viatu aingie ndipo best angu akasema mzazi ingia huyu pimbi kashachemsha nikakataa. Timu ikacheza pungufu ndio nikasema poa nipe viatu kwa yule (mduanzi)jamaa. nikacheza wing ya kushoto nikapata mpira wa kwanza nikapoteza ila wapili nilifanya ile tail crockdile style afu nikatoa assist moja muruwa jamaa simjui akaweka kimiani ngoma refa akasema offside. zikabaki dk kama10 mpira kuisha nikatoa assist nyngine kwa yule yule no 9 akaweka nyavuni. Wakati tunarudi kati akanambia dah mwanangu hivyo hivyo. Tukacheza wee nikajikuta mpira upo kwangu uso kwa macho na kipa nikatia nyavuni nikasikia jamaa yangu nje anaongea yeye sasa.alikuwa anawapa shit wale wenzake.nikaja kufunga nyengine mbili zikakataliwa mpaka mwisho tukafungwa 3-2.
Wapo walionipongeza wengine wakauchuna na aibu. Sikucheza mpira tena wa ushindani hadi leo
 
Ilikuwa pretoria hiyo ngoma. Wabongo wa kutoka sunnyside na kutoka central pretoria. Hapo central kulikuwa na best angu mmoja ananijua balaa langu tangu Tz akanambia njoo nitakupa namba maana yeye alisema hawezi kumwambia kitu. Ila yeye hakuwa mchezaji alikuwa kama katibu wankizushi si unajua timu za masela tena?
Muda ukafika tukawa viwanja vya belle ombre ila katika first 11 yao sikuwepo na wala reserve hawakuniweka kisa eti sio mtu wa central so ushkaji pembeni. Jamaa yangu akashindwa kunitete wengi walimpinga. Mpira ukapigwa sana nikiwa jukwaani naangalia mpaka kufikia kama dk 30 tushapigwa 2-0. Ndani ya hizo dakika substution zilifanyika nne maana jamaa upepo wachezaji ulikata (mabishoo).
Second half dk ya 60 zikafanyika sub 4 nyingine na watu wa reserve wakaisha. Dk ya 62 ubao ukasomeka 3-0 nikaona yule aliyekuwa anachonga sana kwa timu yetu analalamika kutoka upepo nae unakata afu kaona ishakuwa 'isambe'.
Nikasikia akisema "oyaa hakuna mwingine aingie?wakasema sub imeisha akasema hata kama kuna mshabiki anaweza avae viatu aingie ndipo best angu akasema mzazi ingia huyu pimbi kashachemsha nikakataa. Timu ikacheza pungufu ndio nikasema poa nipe viatu kwa yule (mduanzi)jamaa. nikacheza wing ya kushoto nikapata mpira wa kwanza nikapoteza ila wapili nilifanya ile tail crockdile style afu nikatoa assist moja muruwa jamaa simjui akaweka kimiani ngoma refa akasema offside. zikabaki dk kama10 mpira kuisha nikatoa assist nyngine kwa yule yule no 9 akaweka nyavuni. Wakati tunarudi kati akanambia dah mwanangu hivyo hivyo. Tukacheza wee nikajikuta mpira upo kwangu uso kwa macho na kipa nikatia nyavuni nikasikia jamaa yangu nje anaongea yeye sasa.alikuwa anawapa shit wale wenzake.nikaja kufunga nyengine mbili zikakataliwa mpaka mwisho tukafungwa 3-2.
Wapo walionipongeza wengine wakauchuna na aibu. Sikucheza mpira tena wa ushindani hadi leo
 
Wengi hufa masikini kwa kutotanbua vipaji vyao,wao wenyewe au wazazi wao,...wqnamichezo maarufu na matajiri duniani akina Mayweather Jr,Messi,Ronardo na wengineo wamefika hapo kwa watu wao WA karibu kutambua vipaji walivyo navyo..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom