Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U20) ya Azam FC, Iddy Salim, amefariki dunia baada ya kupata ajali ya bodaboda.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC leo Ijumaa Septemba 11, 2026, kipa huyo alifariki dunia jana katika ajali hiyo.
“Tunasikitika kutangaza kifo cha kipa wetu wa timu ya vijana ‘U20’, Iddy Salim, aliyefariki dunia kwa ajali ya pikipiki jana Alhamisi,” imesema sehemu ya taarifa ya klabu hiyo.
Klabu hiyo imesema mwili wa Iddy kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Dar es Salaam, ambako unaendelea kufanyiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tanga kwa ajili ya mazishi.
“Kwa sasa mwili wa marehemu upo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, kwa ajili ya kufanyiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa nyumbani kwao Tanga kwa ajili ya maziko,” taarifa hiyo imeeleza.
Klabu hiyo imeungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu, huku ikitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Iddy Salim.