Kiooo kiooo

Cataliyya

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
781
371
Kiooo kiooo alikivunja nani, simjui simjui wa mwisho akamatwe atiwe gerezani.....
Huu mti gani wa mchongoma, nikiukata haukatiki, hata kwa shoka haukatiki, hata kwa panga haukatiki, hata kwa jembe haukatiki...........endelea
 
Siku hizi watoto wapo na PEs games Tv

Sio muda wote mkuu, sisi wengine tunawafundisha nyimbo za enzi za utoto wetu.

-"Sisimizi mwaenda wapi, twaenda msibani, aliyekufa ni nani, aliyekufa mkubwa wetu, kidege zunguruka ukitaka inama inuka".

-Sikiliza mama wee nikwambie hadithi, mikono yangu midogo weee haiwezi kufanya kazi, sikiliza mama wee nitakuwa mkubwa, nitafanya kazi zote nawe (na wewe) upumzike!

-Baba naomba hela, niende Sinza, na Sinza sitaki! nataka mdundiko mdundiko mdundikooo.......!

-NK.......
 
Ukuti ukuti, wa mnazi wa mnazi, mwenzetu mwenzetu, kagongwa kagongwa, na gari na gari, tumpeleke mnazi mmoja acje kusema kwa mama yake pyeee pyepye Pye..... Mambo badoooo.......
 
Dah... umenikumbusha mbali. miaka hiyoo ya zilipendwa

Deke deke maleeenga
mkono tindi aende tanga
akachukue fungu la upanga
kuku simba kalegea
kalegea koongwe, kongwe la mwana mzee
kila mtu mchaka mchaka
 
Yai bovu yai bovu
Linanuka linanuka
linanukaje linanukaje
uuuff uuuff kageraa

Nina ndoo yangu weee
yakuchota maji wee
maji ya barafu wee

watoto msitizame nyuma... yai linapiiita
 
Back
Top Bottom