Nadhani vioo vya gari vyako ni All auto AU cha dereva ndio auto. Vioo vya auto huna haja ya kushikilia switch ili kipande mpaka juu. Vinakuwa na ngazi mbili, ya kupandisha kawaida na kupandisha automatically.
Sasa hivi vioo vilitengenezwa hivyo ili kuepuka kubana vidole, mkono au chochote kinachoweza kupelekea either kumuumiza mtu au kuvunja kioo. Hivyo sasa huwa vikiona kuna kikwazo kwenye upandaji wake vinajishusha vyenyewe.
Safisha rubber ya kioo na kama una mafuta ya kuspray kama wd40 pulizia kwenye ule ufito wa reli ya rubber kwenye kioo na hili tatizo litaisha kabisa.
Karibu