Kioo cha Tv Samsung inch 55

Kioo cha Tv Samsung inch 55

Eli24

Senior Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
165
Reaction score
365
Habari ndugu zangu JF

Kioo cha tv yangu kimepasuka. Naomba kuuliza hvi hapa mjini Dar wapi naweza pata kioo cha tv inch 55??

Naomba Msaada ndugu zangu kama kuna mtu anajua wapi nitapata. Ahsante
 
Chief nunua TV mpya tu kwani huwezi pata kioo original kitachoendana sawa na TV yako.
 
TV ikishakufa kioo hata ukiuziwa elfu 3,000 usikubali maana bei ya kioo original ni sawa na kununua TV mpya
 
Pole mkuu, nunua TV mpya tu, binafsi change kilipasuka kilikuwa nch 49 curve hotpoint..ulikuwa ni balaa haina hata mwaka na nilinunua ghali kinoma, kuuliza kiooo, ni bei sawa na TV!

Mpaka leo sijanunua TV, najikusanya. Ha ha ha haaaa.. .labda mwaka 2022.
 
Habari ndugu zangu JF

Kioo cha tv yangu kimepasuka. Naomba kuuliza hvi hapa mjini Dar wapi naweza pata kioo cha tv inch 55??

Naomba Msaada ndugu zangu km kuna mtu anajua wapi nitapata. Ahsante
Mkuu ukipata nitag, sema ni expensive sana, mimi nnayo TV kwangu mpya kabisa watoto wamegonga kioo, nimeiweka tu hata sijui pa kuanzia, imebidi nivute myingine.
 
Mkuu hebu jaribu kwenda pale Samsung Kkoo uone watakwambiaje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom