Kiongozi wa mapinduzi Mali aongozewa miaka mitano madarakani

Kiongozi wa mapinduzi Mali aongozewa miaka mitano madarakani

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Jenerali Assimi Goïta amepewa muhula wa urais wa miaka mitano na bunge la mpito, ambao anaweza kupewa tena bila kufanyika kwa uchaguzi.

Kiongozi huyo wa kijeshi, ambaye ametwaa utawala kwa nguvu mara mbili, aliahidi kurejea kwa demokrasia mwaka jana, lakini hilo halikufanyika.

Mswada unaotoa hakikisho kwa mamlaka yake mapya ulisema muda wake madarakani unaweza kurejelewa "mara nyingi inavyohitajika" hadi Mali "iwe na utulivu".

Mswada huo unamhakikishia jenerali Goïta kuiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi hadi angalau mwaka 2030, huku wengi wakihofia kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha ukandamizaji wa upinzani au wale wanaompinga.

Kiongozi huyo wa kijeshi mwenye umri wa miaka 41 aliteuliwa kuwa rais wa mpito baada ya mapinduzi yake ya mwisho mwaka 2021.

Wakati huo aliahidi kufanya uchaguzi mwaka unaofuata - lakini tangu wakati huo amekuwa akiendelea kuongoza, ikiwa pigo kwa juhudi za kurejesha utawala wa vyama vingi.

Mswada huo wa mpito uliidhinishwa siku ya Alhamisi kwa kauli moja na wanachama 131 wa Baraza la Kitaifa la Mpito, ambalo linaundwa na wabunge 147.

Baraza lilikuwa tayari limepitisha hatua hiyo mwezi Aprili.

Mswada huo unaruhusu rais wa mpito, serikali na wabunge kugombea urais na uchaguzi mkuu.

Mwezi Mei, serikali ya kijeshi ilipiga marufuku vyama vyote vya kisiasa nchini humo huku kukiwa na ongezeko la msako mkali dhidi ya wapinzani tangu jeshi kuchukua uongozi.

Serikali ya kijeshi imekuwa ikijaribu kuzima ghasia za wanajihadi zilizoanzishwa na makundi yenye uhusiano na Islamic State (IS) na al-Qaeda.

Tangu kuchukua madaraka, kiongozi huyo wa kijeshi ameunda muungano na viongozi wa mapinduzi katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger, wakiimarisha uhusiano na Urusi baada ya kukata ushirikiano na mkoloni wa zamani Ufaransa.

Jenerali Goïta pia ameiondoa Mali katika kundi la kikanda la Ecowas kutokana na madai yake ya kutaka nchi hiyo kurejesha utawala wa kidemokrasia.

Burkina Faso na Niger pia wameondoka kwenye kundi muungano huo.
 
Safi Bora kuongozwa kijeshi

Kuliko wahuni Kama Tanzania kutawala watu kihuni hivi!!
 
Atakuwa mpuuzi sana na msaliti mkubwa kama atarudisha huo Upuuzi uitwao Demokrasia.
Akichoka, amuandae mwingine mwenye falsafa zake kuendeleza Taifa.
 
Africa my Africa, siasa hatuiwezi.

Sio demokrasia wala hizo tawala za kijeshi, vyote sawa tu.
 
Back
Top Bottom