Elections 2010 Kiongozi Bora: Amua, Chagua

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Wanajanvi, nawasilisha


Wadau inaonyesha kweli mnataka mabadiliko ya dhati. Ujumbe huu uwasaidie kufikia maamuzi ya dhati 31 Oktoba 2010. Mimi siwaambii nani mumchague lakini ninyi mnajua nani wa kumchagua atakae saidia kuyapunguza haya makali ya maisha. With kind regards, Mpenda Mabadiliko.
KIONGOZI BWM Vs JK
MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima
ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa
kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo
250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500,
hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay
kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni
120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa
siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo
atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo
hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo
nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una
familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari
kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie
wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila
waalimu na wenzao.........! 3 years.

Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama
Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko
BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara
yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani.
Wewe je unae mpigia
kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata
baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea
wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.

Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko
busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah
wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia
mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je
zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa
wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye
mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza
kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni
KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI
kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona
hili wameamua kujichorea MIPAKA yao Mapema.

MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA KWA KODI ZENU.

 
Back
Top Bottom