Kinyozi asiyenyoa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kituko nimekiona, hapa kwetu kijijini,
Kuna mtu ni kijana, anaitwa bwana Joni,
Ana sifa ya aina, maana sijabaini,
Kinyozi asiyenyoa, huyo kinyozi wa nini?

Wanamuita kinyozi, apitapo mtaani,
Eti yeye ni mjuzi, wa fani ya kizamani,
Wala hakuanza juzi, alianzia mjini,
Kinyozi asiyenyoa, huyo kinyozi wa nini?

Na tena hana ofisi, kila siku yu nyumbani,
Kuna kitu ninahisi, kumuhusu bwana joni,
Sijauona mkasi, kaushika mkononi,
Kinyozi asiyenyoa, huyo kinyozi wa nini?

Madada wamsifia, eti ni fundi jamani,
Kila anapopitia, wanajigonga kwa joni,
Wakaka wamchukia, kinyozi kinyozi gani,
Kinyozi asiyenyoa, huyo kinyozi wa nini?

Beti zangu zimekoma, swali ninalo kichwani,
Isiwe natia noma, nifukuzwe kijijini,
Nilosema nimesema, mnijibuni watani,
Kinyozi asiyenyoa, huyo kinyozi wa nini?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Wa kijiji una mambo,kwa mzee wa makamo
Au niseme mtambo,wangu huu msimamo
Bwana Joni wa kitambo,si enzi tu za kilimo
Ukijua jina lake,waijua siri yake

Huna haja kuwazua,ukafanya mashindano
Huitaji pekechua,sikiza yake soprano
Wadada waigundua,hata katika maono
Mkasi wake mdomo,na kichwa chenye ujazo
 
Wa kijiji una mambo,kwa mzee wa makamo
Au niseme mtambo,wangu huu msimamo
Bwana Joni wa kitambo,si enzi tu za kilimo
Ukijua jina lake,waijua siri yake

Huna haja kuwazua,ukafanya mashindano
Huitaji pekechua,sikiza yake soprano
Wadada waigundua,hata katika maono
Mkasi wake mdomo,na kichwa chenye ujazo

Jibu nimelisikia, rafiki mpendwa Suki,
Bw. Joni atishia, utadhania fataki,
Wengine atutambia, ayeya kama hataki,
Kama jinale ni siri, si kinyozi, kinyonyozi!

Atufunze na wengine, hicho anachonyonyoa,
Kweupe tena saa nane, Joni ati ananyoa,
Fundi mwingine nene, mbona sina cha kunyoa!
kama jinale ni siri, si kinyozi, kinyonyozi!

Tuwashauri wa dada, wamejaa kijijini,
Vinyozi wasio ada, na mikasi mikononi,
Wananyoa na ziada, akili himo kichwani,
Kama jinale ni siri, si kinyozi, kinyonyozi!
 
Jinale hilo li wazi,mashakani sijiweke
Ni kama mfua nazi,kaziye ndi jina lake
Wadada wenye uchizi,wakubali changa lake
Ukinyozi hauwezi,ingawa vifaa tele

Umenipa mshawasha,wa kijiji kukupasha
Yaliyojiri kwa Asha,nywele kutaka ziosha
Hakuhitaji utasha,wala staili za kingosha
Amerudi ka mzuka,na nywele zimesinyaa

Aliitwa kaka Joni,kuelezea tukio
Wala haikuwa soni,iloleta uvutio
Ni sauti ya puani,na vidole vya kindio
Jambo limezua jambo,kinyozi awa tishio

Ingekuwa ni fundisho,kama wote wangekacha
Wangeepuka michosho,ilowapata mapacha
Walimegwa kiudosho,na nywele zikawachacha
Fanya hima weka biti,labda ujumbe tafika
 
Last edited:
Back
Top Bottom