Kingwendu ndio chaguo la Kisarawe

Kingwendu ndio chaguo la Kisarawe

Km kweli elimu yake ndogo basi itakuwa shida sana, alafu inauma sana. Kile kigezo cha kujua kusoma na kuandika naomba kingeongezwa cha "elimu ya mgombea ubunge iwe atleast bachelor degree". Ni aibu sana kwa mtu asiyesoma anakwenda KUTUNGA SHERIA alafu anakwenda KUZISIMAMIA, anaowatungia ni wananchi ambao wamemzidi kielimu, naomba kigezo cha elimu nacho kipewe kipaumbele, ndio maana WASOMI miaka hii wanazidi kudharaulika. KIGEZO cha AJUE KUSOMA na KUANDIKA kilikuwa ENZI ya NYERERE maana zamani kujua hivyo ilkuwa shida, miaka hii ni tofauti na zamani. Umuhimu wa elimu haupewi kipaumbele, elimu sio kipaji ila nilazima usome. Watu wanapropaganda sana, mara utasikia naongozwa na Roho Mtakatifu hata kwenye mambo ya kiutaalamu!, tubadilike wagombea wasome waelimike na co umaarufu wao

Rejea rasimu ya pili ya Tume ya Warioba, ilikuwa imependekeza mgombea ubunge awe na elimu angalau ya Form IV; lakini baada ya wana UKAWA kujitoa, waliobaki walikiondoa hiki kipengele na kurudisha angalau ajue kusoma na kuandika (darasa la saba kwenda chini) kama ilivyo kwenye katiba ya sasa toleo la mwaka 1977. Kwa hiyo Kingwendu kateuliwa kwa mujibu wa sharia na kanuni.
 
Kingwendu ana elimu ya diploma ya uhasibu aliyoipata chua cha TIA
 
hatari mno. nyie mnajiita wasomi mnaishia kupiga kelele tu sasa hawa jamaa (wasioenda shule) ndio wanaenda kututungia sera bungeni kisha mnakuja kulalamika ooh sheria kandamizi. WASOMI BADILIKENI


Kwani uwoya, lusinde na nape wamesoma wapi
 
Bunge la kutunga sheria na kuisimamia serkali wakiingia wachekeshaji kama hawa sijui
 
Kigwendu, kingwendulileeeeeee, ingia njengoni kama yatakushinda yamjengoni tupia komedi maisha yaendelee
 
mmmh.mtu anayelalamikia elimu ya kingwendu hasemi. uwoya, nape,lusinde na sanga wamesoma wapi au lwakatare kasoma wapi?
 
Kingwendu hongera sana, umeshapita hatua ya kwanza.

Ufanikiwe na hatua ya pili ili uwe mbunge
 
Ha ha ha! Hiyo combination ya Babu Duni & Kingwendu ni hatari ... Maana hawa wote ni watu wa masikhara. I can't imagine speech zao zilikuwaje! Ila huchoki kuwasikiliza.
 
Kingwendu ndio chaguo letu wana Kisarawe
 
Ha ha ha! Hiyo combination ya Babu Duni & Kingwendu ni hatari ... Maana hawa wote ni watu wa masikhara. I can't imagine speech zao zilikuwaje! Ila huchoki kuwasikiliza.
Piga picha Mzee Duni akiwa Rais wa TZ halafu Kingwendu Waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom