Kingunge: Wagombea urais CCM hakuna msafi

Kingunge: Wagombea urais CCM hakuna msafi

Kati ya watu wanaoheshimika ndani ya CCM ni Kingunge Ngombare Mwiru. Leo katika mahojiano na mwandishi wa habari ITV amezungumza jambo ambalo wananchi hawana budi kuyazingatia.

Tuchague viongozi bora na si bora kiongozi. Pia kwa kauli ya kwamba hao wanaojitembeza sasa hivi siyo wasafi,Sasa je CCM imejiandaa vipi kupata mtu msafi?

Je, nani aliyemsafi ndani ya CCM?
Ccm linajifanya takatifu no jambo baa sana kutaka update urais kwa kuipinda demokrasia kama MTU anaona anauwezo shindana usitake kubebwa.Napenda Ifweero hapendi wanaobebwa
Kuna kundi
 
Huyu mzee vipi? Kashasema hakuna msafi halafu tena utendaji?

Huyu mzee ni opportunist wa hali ya juu; hapo ujue kisha shikishwa kibunda cha kutosha na Lowassa!! Kumbukeni kuwa huyu huyu mzee ndio aliyempigia debe sana Kikwete 2005 mpaka ripoti ya kamati ya maadili iliyoorodhesha udhaifu wa Kikwete kiuongozi na kimaadili haikujadiliwa kikaoni!! Sio mtu wa kumuamini kabisa kwa mustakabali wa Taifa letu; siku hizi he is senile so the country will listen to his advice at its own peril!!
 
Kati ya watu wanaoheshimika ndani ya CCM ni Kingunge Ngombare Mwiru. Leo katika mahojiano na mwandishi wa habari ITV amezungumza jambo ambalo wananchi hawana budi kuyazingatia.

Tuchague viongozi bora na si bora kiongozi. Pia kwa kauli ya kwamba hao wanaojitembeza sasa hivi siyo wasafi,Sasa je CCM imejiandaa vipi kupata mtu msafi?

Je, nani aliyemsafi ndani ya CCM?
Hivi huyu ana usafi gani??Mtoto wake tu ni janga
 
Kwa kweli CCM mmeanza kuchanganyikiwa. Kama mnaanza kutukana hata wazee wenu laana inawakula vizuri.

Hebu tueleze Mzee kingunge ameanza lini kunywa viroba?

LAANA IMEWAKAMATA MAPEMA KUPITA MAELEZO...

Huyu mzee kwa wale wanaomjua ni muumini wa KONYAGI; muulizeni mzee Malecela!!
 
Mzee kingunge yuko sahii 100% hakuna aliye msafi na Matumizi ya Fedha hayakwepeki kipindi cha chaguzi wote ni mashuuda wa jinsi kulivyokuwa na Matumizi makubwa ya Fedha kwenye chaguzi za serikali za mitaa mwezi Dec last year

Wagombea wote wa CCM wanatumia Fedha wanachotofautiana ni Amount na hata oposition Nao wanatumia Fedha kwenye chaguzi.Rais wa Marekani Barack Obama kwenye chaguzi zote mbili alitumia Fedha, Rais wa Kenya uhuru Kenya ta alitumia Fedha, Dr Sla uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alishinda ijapokuwa aliporw alitumia Fedha (kukodisha Helkopta) si Fedha haba,Mhe mbowe uchaguzi mkuu wa 2010 alishinda ubunge wa Hai kwa kutumia fedha,Seif sharif Hamad chaguzi zote alishinda za mwak 1995,2000,2005,2010 alitumia fedha

Ni nan hatumii fedha kwenye uchaguzi? Kingunge anauliza ni nani aliyemsafi?
 
Ndani ya CCM wachafu wanaonekana wasafi kiasi cha kuwachafua wasafi... eti wasafi wa CCM wanataka kumvua lowassa uwanachama kwa kisingizio eti ni mchafu!!! Wezi wa fedha za Umma waliojibebea mifweza kibao kwenye mifuko ya Sandarusi nao wanagombea Urais, wamenogewa hadi wanajiona wanahati miliki ya nchi yetu... PINDA? MEMBE? WASSIRA? NGELEJA? NCHEMBA? SITTA?... Hao wote ni mafisadi wakutisha... wote wamelamba fedha za ESCROW...
 
Harakati za kuwania urais ndani ya CCM zimeingia katika hatua mpya baada ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale - Mwiru kuibuka na kudai kuwa wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha kutaka kuingia Ikulu.

“Kiukweli tukiangalia wote wanaojitangaza hakuna msafi hata mmoja... hatuwezi kuchagua rais kama vile tunachagua wachezaji wa mpira, haiwezekani. Tunataka kupata mgombea wa urais ambaye atakuwa na uwezo wa kushughulikia kwa vitendo kero na umaskini wa Watanzania,” alisema Kingunge.

Gazeti la Mwananchi.
 
Mzee Kingunge anamzungumzia nani sasa mwenye sifa alizoziainisha? Hakuna hata mmoja.Kwahiyo tusisimamishe mgombea?

Mzee Tupatupa
 
hawakawii kumwambia mzee kaanza kupoteza kumbukumbu baada ya kuwapa za uso.
 
wasafi bado wapo wengi tu, hata Mungu (kwa mujibu wa maandiko) alipotaka kuiangamiza Sodoma, Nabii Lutu alikuwapo kama mwaminifu pekee na alibaki na kuendeleza kizazi.
..tena Lutu(Loti) aliendeleza kizazi kwa kuzaa na mabinti zake aliowazaa...This quote from the holy scripture amazes me a lot....
 
kwani hili Kingunge ndio nani? yeye katoa maoni yake tu hana mamlaka wala madaraka wala nguvu ya ya uteuzi ama kumchagua wenye sifa ya urais. cc, nec na mkutano mkuu ndio yenye mamlaka hayo na hasa mkutano mkuu ampao unaweza na uwezo wa kuitisha jina lolote kwa kupiga kura hata kama lilichujwa na cc ama nec!
 
wasafi bado wapo wengi tu, hata Mungu (kwa mujibu wa maandiko) alipotaka kuiangamiza Sodoma, Nabii Lutu alikuwapo kama mwaminifu pekee na alibaki na kuendeleza kizazi.

Mwenyyewe namshangaa huyu mzee. Amekuwa too general. Hajiamini kiufupi.
 
wote ccm mafisadi tu, yani ukianza ufisadi ni kama umekula yama ya mtu hutoacha
 
huyu Kingunge mwenyewe mchafu ka nini .sijui haogi?
 
Kati ya watu wanaoheshimika ndani ya CCM ni Kingunge Ngombare Mwiru. Leo katika mahojiano na mwandishi wa habari ITV amezungumza jambo ambalo wananchi hawana budi kuyazingatia.

Tuchague viongozi bora na si bora kiongozi. Pia kwa kauli ya kwamba hao wanaojitembeza sasa hivi siyo wasafi,Sasa je CCM imejiandaa vipi kupata mtu msafi?

Je, nani aliyemsafi ndani ya CCM?

Kingunge hawezi kutamka neno 'MSAFI' kinywani mwake, kuelezea mtu anayefaa. Hii ni kwa sababu maisha yake yooote ameshiriki kufanya uchafu mwingi kupitia CCM na serikali yake.Yeye na genge lake ndio wameifikisha CCM na Tanzania katika hali hii mbaya na chafu.
sasa anapoibuka kutaka kusema anafahamu mtu msafi anafananaje, nadhani tunapaswa kumtilia mashaka makubwa na akili yake! He is ruthlessly mad!
 
Kingunge mnafiki don't waste your time listening to him
 
Back
Top Bottom