Kingunge Ngombale Mwiru avuliwa ukamanda UV-CCM Taifa

Utawala umefitinishwa. Goodbye CCM.Kapumzike salama tutaonana ahera ya tarehe 25.10.2020 kama utakua bado una pumzi.
 
Hawa jamaa wasipobadilika, watatufikisha pabaya,washapanga mbinu zote za kurudi madarakani, nashangaa naona jeshi lishaanza shirikishwa, nina wasiwasi yale ya kenya yatafika kwetu, kwani hayo mabavu yao watu hawatakubali, ndo hapo machafuko yatakapotokea, na ukizingatia elimu zero, miundo mbinu zero, usafiri wa anga ni tetra 0, yani tunaishi kwa kudra ya allah tu, kuna mambo ambayo ndo yanaharibu jamii haya ndo yapo juu, mf. Sembe, pembe za ndovu manake tumekuwa vinara, mambo muhimu ya kunyanyua uchumi wetu vishauwawa vyote, lakini tulivyorogwa na kurogeka cubically, watu bado tunao hao hao na kuwapigia vigelegele, sisi ni wa kuzidiwa na msumbiji, rwanda kweli, aibu sana, na kutokana na mfumo wao ulivyo hata akija huyu jm bado hatafanya lolote, mamilioni yatapotea zaidi ya escrow, yatakuja zaidi ya escrow etc na hakuna atakayefanywa lolote


Mkuu bado miezi miwili kiama chao kimeshafika huu sio wakati wa kulalamika. Wahimize walio karibu nawe tuikamilishe kazi tuliyioanza miaka ya 90. Hata familia inayomiliki chama cha CCM inalijua hilo
 
Kwa kumtimua Mzee kingunge ngombale mwiru huko bado wanajiita kuwa ccm bado ipo pamoja na haina makundi?wakawadanganye watoto wao huko
 
Kwani Ukamanda wa vijana ni issue, Ninahakika kuwa Kingungwe hategemei posho za vikao za Ukamanda wa vijana. Isitoshe wameshastaafu au kuachishwa makamanda wa majeshi itakuwa kamanda wa umoja wa vijana tena wa CCM?

Kuna vichekesho!
 
Aondoke huko mzee wa watu keshazeeka,siasa ya sasa si ya miaka ile,ooohoo hiki ni kizazi cha twita facebok..ni kizazi korofi mwishowe watamkata mtama bureee!

Kama walivyo mkata mtama mgombea urais karokola
 
eti kamanda mwe!! sasa huyu babu ukamanda alikuwa ana uperform vipi ... mtu unamiaka 100?
 
Yaani watu hawalali kisa ukawa??? Mzee huyo tunamuitaji sana najua atasaidia kitu fulan
 
Nyerere alivyosema CCM si Baba yangu wala Mama yangu, Mapunda angekewepo angemfukuza kwenye Chama. Hawa vijana wa mtandao Dotcom hawana adabu. Kingunge, Wazee wa Tanu na waasisi wa CCM waliobaki mnamfukuza!? Nasubiri nimsikie JK atasema nini. UVCCM mnavuka mipaka.
 
Mmemnyima number mwenye mpira hiyo mechi itachezeka kweli?
Kingunge ndio mchawi wenu wa miaka na mikaka sasa kasema kweli darubini zake zinaonyesha giza mmembwaga ngoja sasa mtaona cha mtema kuni OCTOBER.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom