Kingunge Ngombale Mwiru avuliwa ukamanda UV-CCM Taifa

Kingunge Ngombale Mwiru avuliwa ukamanda UV-CCM Taifa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,677
Reaction score
870,404
Habari za hivi punde kuhusiana na kikao kinachoendelea kwenye ukumbi wa Mwalimu nyerere zinasema mzee Kingunge Ngombale Mwilu ametimuliwa rasmi kuwa kamanda wa uvccm Taifa kwa kushindwa kutimiza majukumu yake na kwenda nje ya mstari.

========================

BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), limemvua ukamanda wa umoja huo mwanasiasa mkongwe na kada wa chama hicho Kingunge-Ngombale Mwilu.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda, alisema uamuzi huo umefikiwa juzi usiku, baada ya baraza kuu la umoja huo lilipokutana, pamoja na mambo mengine waliamua kumvua ukamanda Kingunge.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza hilo, naye alitumia nafasi hiyo kuelezea nafasi ya vijana hao kuelekea uchaguzi mkuu, huku pia akiweka wazi kwamba, wanaoondoka CCM wanatoka kwa mapenzi yao wenyewe.

Kuhusu kuvuliwa ukamanda mkuu, Kingunge, Mapunda alisema "Baraza letu lilimvua ukamanda mkuu, Kingunge Ngombale Mwilu. Uamuzi huu ulitolewa kutokana na tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kwenda tofauti na maadili na taratibu za CCM."

Aidha, kikao kimetoa mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.

Mapunda alisema pia, baraza la umoja huo kupitia kikao chake cha juzi, kimeunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi na kamati ya utekelezaji kuhakikisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.

"Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo," alisema.

Kingunge ni mmoja kati ya makada wa CCM ambaye alionesha hadharani kutoridhishwa na mchakato wa chama hicho katika kumpata mgombea urais kwa maelezo kuwa, taratibu zilikiukwa.

Kada huyo wa CCM wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho, alikuwa upande wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo ndani ya chama, lakini jina lake lilienguliwa.

Baada ya jina la Lowassa kuenguliwa, Kingunge hakusita kuelezea masikitiko yake dhidi ya chama chake, ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho walikuwa na wagombea wao mfuko na sehemu kubwa, utaribu wa kumpata mgombea urais wao si wa haki.

Rais Kikwete akizungumza na baraza hilo, alisema anayetoka CCM kwa sasa anatoka kwa hiari na mapenzi yake mwenyewe kwa sababu uamuzi wa nani agombee urais kupitia chama hicho ulifanyika kwa pamoja.

Aidha, Rais Kikwete alisema uamuzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya CCM na kuwa, ilipigwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa, baada ya mjadala mrefu, ambapo uamuzi ulichukuliwa kwa pamoja.

Pia, alisema hakuna haki iliyovunjwa katika mchakato wa kutafuta mgombea urais wa CCM, kwa sababu taratibu zote zinajulikana wazi na ni zile zile na ukweli ni kwamba, baadhi ya watu waliamua kutoka CCM, hata kabla ya vikao vya Dodoma kuanza.

Rais Kikwete aliwaambia vijana hao: "Aliyetoka, katoka mwenyewe kwa uamuzi wake mwenyewe, lakini pale tuliamua wote. Maana pale tulipokubaliana kupiga kura, tulikubaliana kupiga kura kwa majina yale matano, si uamuzi wangu pekee yangu, bali ulikuwa uamuzi wa sote. Maana tulijadiliana na kukubaliana kwa mujibu wa Katiba yetu, majina ni haya haya. Tukapiga na kura yakaisha."

Alisisitiza :"Hivyo, anayetoka, anatoka kwa hiari yake mwenyewe kwa sababu pale Dodoma wote tulikubaliana, tuliamua wote kwa mujibu wa Katiba yetu na kwa kweli wote wanaotaka kutoka ndani ya CCM wanatoka kwa hiari yao wenyewe na wala si kwa sababu ya kunyimwa haki."

Aliongeza, sasa mchakato umekwisha na aliyepata kapata na aliyesokosa kakosa. Mchakato huo haurudiwi tena na hawawezi kuitisha tena mkutano mkuu. Lililobaki sasa wanasubiri Dk.John Magufuli arudishe fomu na baada ya hapo ni Ihynae Ihyena na mambo yanakwenda.

" Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Katika mchakato huo wa Dodoma, CCM ilimteua Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli kuwa mgombea urais


Chanzo: Jambo leo
 
Hakika chama sasa kimeoza na hakina msimamizi tunaishi kama kambale.
Yuko wapi mzee nassoro moyo na sasa mnataka kufanya nini kwa kingunge,kadi zao na namba zao tutamkabidhi nani?
Hii ni hatari kwa maisha mafupi ya chama chetu tuliyonayo yaani tungeishi miaka kumi leo makada/walinda maslahi wameamua kutuulia chama na kukizika october/25/2015 ??
Hivi ni kweli uvccm nlo limekuwa genge la vijana watumikishwa wasio na dira wala mwelekeo ndani ya chama?
-hakika hili la kumuengua mzee kingunge ukamanda wa vijana ni zaidi ya maasi kwa chama,inawezekana hakuwa na mbinu za kuwa fikisha huko muendako ninyi vijana lakini huu siyo mida mwafaka kwa ujinga kama huu mlioufanya.
Naamini sasa kweli october /25 ushindi tutaushuhudia kwenye luninga tukiwa mafichoni.



"ndimi mwana tanu & ccm mwenye kuijua kweli fitina kwangu mwiko"
 
Kingunge anafanya nini huko ccm wata mchochoa bure mzee wawatu atoke tu kwa amani
 
asante kijana maana hujui ulitendalo...
Kiufupi tuu unajua maana ya kumvua ukamanda wa vijana uvccm en' what next after nyerere convetion center..!

Aondoke zake amfuate yule jamaa mwenye mamvi...na wewe ukitaka ungana nae mwende zenu
 
Huyu mzee nae apumzike sasa umri huo anatakiwa awe anacheza na wajukuu nyumbani sio kuhangaika na siasa.

Awaachie vijana nao wakamate nafasi hizo wapige posho.
 
Kakatwa tamko la vijana au Makonda liko wapi? au kakatwa kwenye keyboard?
 
Kngng ni injini ya train iliyochoka.hana jipya.heko vijana wa ccm.amfuate el alikokwenda akampigie debe na huko nako ili ukawa iparaganyike zaidi.hivi ni nani jamani asiye wajua wazee mslahi kama akina kingng? Hao ni wazee wa biashara zao.wanakanyagia vijana wa ccm ili wafike waendako.alitukana maaskofu sasa moto unamchoma hapahapa.
 
hata gazeti letu la uhuru liliwaita waliomsindikiza lowassa kuchukua fomu ya uraisi 'vibaka'!

Mkuu bandiko lako limekuwa kama kumwaga almasi penye kuku, wataishia kuzichakura na kuzimwaga. Watachotaka ni punje ya mtama wajaze tumbo.

Kizazi cha sasa hakijui tena thamani ya mzee katika maisha yao. Wanashindwa kuelewa kuwa Jando bila Mzee ni sawa na jahazi bila nahodha.
 
Hawa jamaa wasipobadilika, watatufikisha pabaya,washapanga mbinu zote za kurudi madarakani, nashangaa naona jeshi lishaanza shirikishwa, nina wasiwasi yale ya kenya yatafika kwetu, kwani hayo mabavu yao watu hawatakubali, ndo hapo machafuko yatakapotokea, na ukizingatia elimu zero, miundo mbinu zero, usafiri wa anga ni tetra 0, yani tunaishi kwa kudra ya allah tu, kuna mambo ambayo ndo yanaharibu jamii haya ndo yapo juu, mf. Sembe, pembe za ndovu manake tumekuwa vinara, mambo muhimu ya kunyanyua uchumi wetu vishauwawa vyote, lakini tulivyorogwa na kurogeka cubically, watu bado tunao hao hao na kuwapigia vigelegele, sisi ni wa kuzidiwa na msumbiji, rwanda kweli, aibu sana, na kutokana na mfumo wao ulivyo hata akija huyu jm bado hatafanya lolote, mamilioni yatapotea zaidi ya escrow, yatakuja zaidi ya escrow etc na hakuna atakayefanywa lolote
 
Huyu Mzee Kingunge angejipumzikia siasa tu, kama Nape na Baba Riz1 walimpuuza alipowashauri kabla Lowasa hajahama chama, itakuwa huyo Riz1 na wenzie? Hii ni aibu kubwa si kwa Mzee Kingunge tu, bali kwa wanahistoria wote pamoja nasisi sote tulio onja manufaa ya TANU na ile CCM ya 1977. SASA NI HAKIKA YA KUWA, CCM IMEAMUA KUJIKAANGA KWA MAFUTA YAKE YENYEWE.
 
Inaelekea mzee Kingunge amekwisha amua kuwa asizikwe na bendera ya ccm kama walivyozikwa wenzie waliomtangulia!!
 
Breaking news.
Baraza kuu uvccm taifa linaolloendelea muda huu ktk ukumbi wa mwl nyerere convention centre mjini dar es salaam lamfukuza ukamanda wa taifa ndg kingunge ngombale mwiru kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake vizuri na kuwa nje ya mstari wa ccm.
 
Back
Top Bottom