Kingunge awafyatukia wanaotamka ufisadi

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Apr 18, 2009
1,195
232
Mwandishi wetu, Pwani

MWANASIASA mkongwe nchini Kingunge Ngombale - Mwiru ameibuka na kuwataka wenye ushahidi na watu wanaodaiwa kuwa mafisadi wautoe hadharani

"Tuache kupakaziana maneno mabaya kama ufisadi kwani neno hilo lina maana mbaya kuliko inavyodhaniwa na iwapo kuna mtu ana ushaidi na matendo ya ufisadi ya mtu ni bora ayatoe hadharani na kutoa ushahidi kulio kuendelea kuchafuana kwa kuitana kila kukicha mafisadi" alisema Kingunge.

Mwanasiasa huyo mkongwe hapa nchini alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano maalumu ulioandaliwa na CCM Wilaya ya Bagamoyo ambao pamoja na mambo mengine ulilenga kuimarishaji chama hicho wilayani humo.

Kingunge alisema hivi sasa imekuwa ni tabia kwa baadhi ya viongozi wakiwamo wa dini na wanasiasa kutumia majukwa yao kuwavunjia heshima viongozi waliopo madarakani kwa kuwaita mafisadi huku wakiwa hawajui hata maana halisi ya neno hilo.

Alisema viongozi hao wanadhani kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi na uhuru wa kutoa maoni hapa nchini ni kuruhusu watu kutokuwa na adabu kwa wenzao dhana ambayo alisema si sahihi na hivyo alishauri iachwe mara moja.

"Hili ni jambo lisilowezekana hata kidogo kiongozi anachaguliwa na wananchi halafu wanatokea baadhi ya watu wanamvunjia adabu kiongozi huyo, mimi nadhani huko ni kuwatukana wananchi na hakukubaliki katika mahala popote", alisema Kingunge na kuongeza:

Akizungumzia suala la udini lililoshika kasi hivi karibuni, Kingunge alisema Watanzania wanapaswa kusimamia maadili yao waliyozoea tangu enzi za mababu kwani wapo baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini ambao wamefilisika kimawazo na hivyo wamekuwa wakitumia udini kutaka kuwagawanya wananchi.


Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/21744-kingunge-awafyatukia-wanatamka-ufisadi

Fikra zangu:
Nadhani huyu mzee yupo ICU kiakili na mawazo. Na hii ndiyo inayopeleka CCM shimoni. Watu wanaushahidi wa wizi na uporaji wa rasilimali za serikali, wakienda mahakamani mahaka ni ya CCM, sasa kilichobaki ni hukumu ya wananchi. Wewe wasubiri 2015 moto utawaka!
 
Kwenye suala la udini yuko sahihi ila anatakiwa kukemea hilo kwenye chama chake maana ndicho kimeasisi UDINI Tz!
Hata yeye pia ni FISADI!!
 
Kwenye suala la udini yuko sahihi ila anatakiwa kukemea hilo kwenye chama chake maana ndicho kimeasisi UDINI Tz!
Hata yeye pia ni FISADI!!
Umenihappisha!! Kwamba na yeye ni FISADI!! Sijui CCM wafanyeje kujisafisha maana wote ni wachafu na kila anayekuja kuropoka anaropoka kama katoka kwenye mtungi, yaani anajifanaya hajui yale yanayoendelea hapa duniani. Na hakika waTz kama hatutakaa sawa kupigania haki, basi hata Mungu wa mbinguni atatulaani! 2015 ni jibu na kampeni zinatakiwa zianze mapema kabisa ili kujenga chama pinzani kitakachokuwa tayari kuchukua nchi, na pia kwa sasa panatakiwa pawe na kampeni za kukemea ufisadi ili 2015 isije kuwa nchi imebaki mifupa tu iwe kama Hispania, jamaa alishinda kwa kura nyingi lakini karithi serikali mifupa wananchi tena hawamtaki au kama vile Ugiriki jamaa aliondolewa kwenye nafasi yake ya Uwaziri mkuu wakaweka mwingine wakidhani ni suruhisho kumbe wapi leo kuna mzee wa miaka 70 kajipiga lisasi mbele ya jengo la bunge la Ugiriki maana hana kitu na alikuwa anaelekea kuanza kuokota chakula jalalani.
 
Ivi kingunge na vingunge Wapo nchi hii? Anauza maji ya kisima k'nyama sikuhizi icho kibabu.
 
Jamani huyu mzee vipi?hana wanashauri?mwambieni apumzike mambo ya siasa.ameisha poteza mvuto kwa kiasi kikubwa sana.
 
Kwenye suala la udini yuko sahihi ila anatakiwa kukemea hilo kwenye chama chake maana ndicho kimeasisi UDINI Tz!
Hata yeye pia ni FISADI!!

Hana dini halafu anajifanya kuwapinga viongozi wa dini wanaokemea maovu ikiwrmo ufisadi
 
Anatapata mzee wa watu, itakuwa ni hasira za kuchomolewa cc.... Naona ile 'mbinu' ya cdm ya kuishitaki serikali ya ccm kwa wananchi kwa kutowachukulia hatu mafisadi inazaa matunda.
Pia inampasa akamwambie maneno haya nape!
 
Mzee Kingunge amekuwa mzigo na anakichafua chama na kutuchefua wanachama.
Suala la ufisadi linapita uwezo wake wa kufikiri,kuuchambua na hata kuuchukulia hatua.
He is a spent force,akae kimya na kula pensheni yake tu.
 
nadhani haka kababu kalishirikiana na mk*wapa kumdedisha father of the nation. Just curious
 
Kesha choka mno, naona hata uwezo wa kufikiri umekwisha na hajui anayosema!!!
 
Awasiliane na Kainerugaba

Wakati nikiendelea kusoma nilitaka kuandika kama wewe, asante sana, aende kwa Faresh DPP ndiko kuna mafaili , na kwa kuwa mahakama ni ya CCM itawaosha tu na maji taka, hata hivyo Yeye ni FISADI MZEE kwani Ubungo Terminal , na Packing System za Mjini anatuumiza sana. Tena ukiangalia mali anazomiliki mwanae Kinje zinatisha wakati afanyi kazi wala bishara halali, huyu mzee ndio anamumwagia mipesa ya rushwa, yeye anaFISADi mabinti tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom