Kingunge awafyatukia wanaotamka ufisadi

Duh kweli Mzee Kingunge kachoka kiakili.
Hebu mkumbusheni alivyotuibia pale Ubungo Bus Terminal!

Alitaka hata akiiba viongozi wa dini wamsifie?

Nyerere alikwisha sema ukingia tabia ya kula nyama ya watu huiachi tabia hiyo,Kingunge anakwenda mbali zaidi n kuta kuihalalisha.

Mzee Kingunge ushindwe,uchoke,uzeeke na ulegee!

Baba Mungu ni kwa nini unamchukua kanumba unaacha wazee ambao ubongo wao unaenda reverse kama huyu hapa? E baba lete mauti kwa huyu dunia iondokane na uchafu huu
 
Huyo Mzee amesahau huu ni wakati kuita koleo koleo na siyo kijiko kikubwa!?Au anahofia nini?
 
..wameshasahau maneno kama wanyonyaji, makabaila, mabeberu, mirija,etc etc.

..tatizo CCM walijisahau. sasa muda umekwenda, hakuna walichokifanya, na wananchi wameanza kuwakataa.
 
Mwanasiasa mkongwe nchini
Kingunge Ngombale Mwiru
Mwanasiasa mkongwe nchini
Kingunge Ngombale Mwiru
amesema kuwa viongozi wa dini
na wanasiasa wanaowaita
wenzao mafisadi ni aina ya
viongozi waliochoka na kufilisika.
Akizungumza katika mkutano
maalum ulioandaliwa na CCM
Wilaya ya Bagamoyo, Kingunge
alisema kuwa viongozi hao wa
dini na wanasiasa wanadhani
kuwapo kwa mfumo wa vyama
vingi na uhuru wa kutoa maoni
ni kuruhusu watu kutokua na
adabu kwa wenzao.
Alisema kuwa imekuwa ni tabia
hivi sasa kwa baadhi ya viongozi
wa dini na wanasiasa kutumia
majukwaa yao kuwavunjia
heshima viongozi waliopo
madarakani.
“Hili ni jambo lisilowezekana hata
kidogo kiongozi anachaguliwa
na wananchi halafu kuna watu
wanamvunjia adabu kiongozi
huyo huku ni kuwatukana
wananchi na hakukubaliki
mahala popote,” alisema
Kingunge.
Akuzungumzia suala la ufisadi
Kingunge alisema kuwa neno
ufisadi maana yake si kama
inavyofikiriwa na watu
wanaoneza neno hilo bali lina
maana mbaya kuliko
wanavyolisema baadhi ya watu
wakilitumia kuwachafua wenzao.
“Tuache kupakaziana maneno
mabaya kama ufisadi kwani
neno hilo lina maana mbaya
kuliko inavyodhaniwa na iwapo
kuna mtu ana ushahidi na
matendo ya ufisadi ya mtu ni
bora ayatoe hadharani na kutoa
ushahidi kuliko kuendelea
kuchafuana,” alisema Kingunge
Akizungumzia masuala ya udini
Kingunge alisema kuwa
Watanzania wanapaswa kuacha
kuendekeza udini kwani baadhi
ya wanasiasa na viongozi wa
dini ambao wamefilisika
kimawazo wamekuwa
wakitumia udini kutaka
kuwagawa Watanzania.
CHANZO: NIPASHE
my take;kama haya ndo mawazo ya wazee wetu!?,basi vijana tunakazi ya ziada.
 
Baba Mungu ni kwa nini unamchukua kanumba unaacha wazee ambao ubongo wao unaenda reverse kama huyu hapa? E baba lete mauti kwa huyu dunia iondokane na uchafu huu
inabidi umwombe mola wako msamaha,unampangia kazi,unaomba awe mbaguzi,yaani baya li mkute kisa maoni yake ambayo huyaafiki. n then u call urself great thinker
 
kama ni kingunge hategemewi kufurahia mafisadi kusemwa, na hana haki ya kimaadili kuzungumzia kuhusu ufisadi kwa namna yoyote,kinachoshangaza ni kwamba hajui kwamba hana mvuto isipokuwa ndani ya chama chake ambao hata hivyo hakuna anayepinga ufisadi
 
hiki kizee,hakina dini wala mchango wowote katika nchi hii ninawasiwasi hata kod akilipi zaidi ya kutumia mali za wananchi,yeye pia ni fisadi.wanakufa watu muhimu kinabaki hiki kisiki
 
Inasemekana Mzee Kingunge ni supporter mkubwa wa EL kuwa Rais 2015; ndio maana yumo kwenye harakati za kumsafisha!
 
Mlitegemea asemenini after receiving easter package toka kwa wamiliki wa jina hilo? Kwani kijana wake na mkewe walikuwa wanafanya nini pale ubungo bus terminal na kule mitaa ya posta na kariakoo wanafanya nini kwenye suala zima la parking? Je wanachokusanya kinaendana na wanachoilipa serikali na watumishi wao? Je huo tuuiteje, ujasiriamali au..................?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom