Mkuu haya aliyoyatoa Mzee Kingunge sio mapya, alishayatoa kwenye programu ya chama cha ccm iliyotoka 1987, enzi za chama kimoja, katika kuujenga uchumi wa kijamaa kisayansi kwa kuanzisha mapinduzi ya viwanda,ikijumuisha uwekezaji wa viwanda mama na vya kati. Kuanzisha mashamba makubwa ya kilimo cha kisasa na utumiaji wa zana za kisasa za kilimo na kuondokana na kilimo kidogo kidogo cha kutumia jembe la Adam na Hawa, pamoja na matumizi ya ng'ombe. Kama ile programu ingewekewa maanani na kutekelezwa leo tungekuwa mbali sana kiuchumi. Cha ajabu hakuna ndani ya ccm aliye ijali kabisa na chapisho la programu hiyo nadhani inaoza tu kwenye maktaba za ccm. Hii ni mara ya pili Mzee kingunge ana introduce hiyo sera. Hope fully hao wana ccm wenzake wataikubali na kuitekeleza, kama itakuja kuingia kwenye hii katiba ya mzee sita na walio wengi au katiba itakayokuja kupatikan ya wananchi, whichever. Ni vizuri sera hiyo ikaingizwa kwenye katiba iwe dira ya taifa lakini utekelezaji wake unahitaji dedication and commitment to the nation, lakini kama tutaendelea kuwa na aina hii ya viongozi wa leo wachumia tumbo, mafisadi, wanaoendeleza utawala wa ki imla wa kupachika vizazi vyao madarakani sera hii itakuwa ndoto. Neverless kwenye hili bunge maalum la kutunga katiba ya wajumbe walio wengi, Mzee kingunge ingalau kazungumza ya maana.
..unajua sisi wengine tulikulia ktk CCM ile ya mkutano wa Kizota.
..kutokana na experience hiyo ndiyo maana tunaamini kwamba hiki chama kilichoko sasa hivi siyo CCM, bali ni kitu tofauti kabisa.
..CCM ile ya kina Kingunge ilikuwa chama au movement for ideas. Hii ya sasa hivi hata sijui niseme ni dubwana gani, may be it is a campaign machine. Kila tapeli nchi hii yumo CCM. Chama hakina sera na watendaji wake wamebaki kuwa watu wa kauli mbiu na mipasho ya "niseme...nisisemeeeeee"
cc Kasheshe, Mtu wa Pwani, Mchambuzi, chama
Last edited by a moderator: