King'amuzi cha ting

King'amuzi cha ting

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
282
Ndugu wapendwa, katika harakati za kukimbizana na muda ili TV yangu iendelee kufanya kazi nimejikuta nimenunua king'amuzi cha TING AAL - 002 kwa bei ya 99,000/=. Kwa yeyote anayefahamu uzuri au matatizo ya aina hii ya king'amuzi naomba anijulishe. (Msaada Tafadhali).
 
Hapo mkuu kama ni mtu wa dini sawa lakini kwa burudani hamna kitu.wako kidini zaidi, nilinunua hicho nimeishi kukitupa.
 
hamna bhana mbona cha ukwel xana 2...sema wako katika mchakato wa kufunga steshen zingine 42...xo just wait ma friend .....
 
hamna bhana mbona cha ukwel xana 2...sema wako katika mchakato wa kufunga steshen zingine 42...xo just wait ma friend .....


Hawana lolote hao Ting.
Huo mkakati ndio wimbo wao wa kila siku utekelezaji ni zeroo.
 
Hapo mkuu kama ni mtu wa dini sawa lakini kwa burudani hamna kitu.wako kidini zaidi, nilinunua hicho nimeishi kukitupa.

Kweli mkuu,kama anapenda kusikiliza kwaya achukue
 
Ting ni mabingwa wa matamko, mikakati na michakato... utadhani inamilikiwa na CCM!!! imekula kwako mkuu kwa dini tu utawapenda na lazima uokoke mwaka huu
 
wivu mwingi..ne bwana,yaani nafikiri unafikiri ki masaburi

Default

Quote By AlP0L0 View Post
Hapo mkuu kama ni mtu wa dini sawa lakini kwa burudani hamna kitu.wako kidini zaidi, nilinunua hicho nimeishi kukitupa.
Kweli mkuu,kama anapenda kusikiliza kwaya achukue

haya na huyo je!
 
Aisee hapo hamna kitu. Ungefanya michakato ya kupata labda DSTV ila hao bei kubwa. huku Arusha tunatumia Milan cable ina kila kitu halafu wana bei nafuu mno
 
Aisee hapo hamna kitu. Ungefanya michakato ya kupata labda DSTV ila hao bei kubwa. huku Arusha tunatumia Milan cable ina kila kitu halafu wana bei nafuu mno[/Q
UOTE]

Aisee watu wa Arusha na Moshi.mnaenjoy kwa saana kupitia Milan Cable
 
Ting ni mabingwa wa matamko, mikakati na michakato... utadhani inamilikiwa na CCM!!! imekula kwako mkuu kwa dini tu utawapenda na lazima uokoke mwaka huu


Hahahahah. Ting hawana ishu kabisa
 
Ting wao wanatangaza DINI tu hamana lolote, hamana movie hamna mpira yaani wamejaza machannel ya DINI.
 
Mkuu naomba unijuze upatikanaji wa hii milan cable(Please)
 
Mimi naipenda sana, ila wananiboa saaaaaana ukiongeza salio, inaweza kukata kama masaa hata 5 au zaidi hata kama umeongeza salio wakati salio la kwanza halijaisha, yaani hapo ndipo sipendi, ila kwa watoto wangu ni nzuri sana kwani hawaangalii mambo ya ajabu kama ya startimes, wakirekebisha hilo mimi nipo pamoja nao hadi king'amuzi kibadilishwe sijui kitaitwaje?
 
hamna bhana mbona cha ukwel xana 2...sema wako katika mchakato wa kufunga steshen zingine 42...xo just wait ma friend .....

Una ubia nao???!!! Ving'amuzi vyote viko sawa!!, ukijumuisha na hicho cha dstv. Tatizo liko katika pakeji. Ukitaka chanel nyingi na nzuri zaidi ni lazima ulipie pesa nyingi zaid.
 
Inategemeana na unapenda nini kama unapenda tamthilia na picha za kichina nemda Startimes,na kama unapenda picha za kimagharibi,makala,maisha na mpira kidogo nenda Zuku,lakini hao hizo free channels wana TBC na Channel Ten ,tu ila upande wa radio kuna Clouds FM,na radio mbalimbali,pia nimesikia wataleta kifurushi kitakachokuwa na simu na intaneti,kama ilvyo Kenya.Na kama unazo fweza nunua Dstv huyo ndio baba wa ving'amuzi hata jina la ving'amuzi ndipo lilipo zaliwa ,na aliyebuni hilo neno ni ndugu Nsekela mtoto wa aliyekuwa kigogo wa NBC alikuwa Multi Choice enzi za mwanzo wake hapa TZ
 
Ndugu wapendwa, katika harakati za kukimbizana nu muda ili TV yangu iendelee kufanya kazi nimejikuta nimenunua king'amuzi cha TING AAL - 002 kwa bei ya 99,000/=. Kwa yeyote anayefahamu uzuri au matatizo ya aina hii ya king'amuzi naomba anijulishe. (Msaada Tafadhali).

Hujajuta kuomba msaada?
 
Back
Top Bottom