Habari nilizozipata jioni hii kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa BTL kuna tetesi kuwa wataviweka sokoni rasmi na washafunga mitambo yao. Ni full kuenjoy kwani unatumia antena ya ndani (indoor antena) si kama startimes. Bei zake zitaendana na ubora wao ni full HD, MP4, Waweza kurekodi vipindi.
Kwa mwezi utalipia 6000 na vitauzwa kwa sh.140,000.
km unataka emmanuel tv funga dish la kawaida ujitanue
pls can smbdy enlighten me.
what does dishi la kawaida and some call it free to air means.
m lost...!
mengi hajakuibia ndugu, ndo maana kuna king'amuzi cha TBCCM kinaitwa startimes kinauzwa 39 elfu tu, ni uamuzi wako kutumia chapati au andazi.yaani wafanyabiashara kama akina mengi hawana hata aibu na wao kuamua kujiingiza kwenye biashara ya kuwaibia wananchi...140000 watatoa wapi...kuna watanzania wengi waliokua wapenzi wa ITV lakini hata 70000 hawajui imekaaje ndio waje kulipia 140K...acheni upuuzi...
King'amuzi cha Ukweli hapa Bongo ni "Easy Tv" pekee. Kina ubora wa Matangazo pia kina local channels karibuni zote kasor DTV na CTN na CEN. Ila hadi zenji TV imo Ndani. Na kama ww ni Mpenzi wa Movie kuna MBC 1 hadi 5. BalaA tupu. Ukinunua Digitek/Continental/BtL au Startimes Umeliwa. Labda Usubirie "Go TV" King'amuzi Dada cha Dstv kwa ajili ya Local and Entateinment Channels.
Hadi Kufikia Decemba mwaka huu kaya Moja itakuwa na wastani wa Ving'amuzi sita hadi 8.
MunGu tusaidie kwani ni wW pekee unajua Mifuko yetu inavyotobolewa kwa Mlolongo wa Matumizi kama Vile Digitale ya Ving'amuzi.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Channel gani zitaoneshwa?
Sent from my GT-P7500 using Tapatalk 2
mkuu hebu tufafanulie, free on air unaweza kukamata hizi channel zilizoingia kwenye digital?Mpango mzima ni ma dish ya free channel
Bongo ubabaishaji, watu wataanza biashara ya makabati ya kuwekea ving'amuzi. Kwangu kuna Receiver ya Dish la bure, GTV, DSTV, StarTimes, ZUKU, VCR ya zamani, na DVD Player.
Yale yale ya mtu kuwa nalaini 4 za simu. Vipi wakashirikiana tukawa na receiver moja na channel zote?
Mbona leo hakijaingia sokoni?
...Pole Mkuu, tatizo la wanaJF walio wengi sasa hivi ni kutaka kuonekana wa kwanza kuweka Breaking News. Kwa maana hiyo mtu anaweza akafikiria tu jambo kichwani mwake na akaja haka kulitundika kwa kianzia cha 'Kuna Taarifa desh desh, mwenye Taarifa kamili atuwekee hapa'!!
Ni Ajabu.
Huko ulikozitoa si ungetafuta ukamilifu wa habari hizo kisha ukatumwagia hapa jamvini?
Hii taarifa ya DigTek niliishasema mahali fulani huko nyuma. Tunaviharakishia nini kwa maneno ya mdomoni wakati mwenyewe bado anajipanga??
Si atakapokuwa tayari ataviingiza Sokoni na tutaviona? Kwa nini tunamuwahisha na Midomo yetu???
Hii taarifa aliyotundika mkuu siku ya Alhamisi kama sikosei kwamba 'Habari nilizopata jioni hii, DigTek kuanza Jumatatu!". ilipaswa wanaJF wala isitusumbue vichwa:
Hivi kwa Jinsi tunavyomfahamu Reginald Mengi, huyu huyu mfanyabiashara tunayemjua ambaye akitaka tu kuongeza Kipindi Kipya kwenye Tv ama Radio yake atakitangaa Mwezi Mzima kabla, Leo aingize jambo kuubwa kama King'amuzi chake awe hajatutangazia hata kwa Miezi mitatu Kabla????
Kama DigTek kipo basi kitakuja tu lakini hii isiwe sababu ya baadhi ya wanaJF kuwa Ma-sheikh Yahya' wa kutabiri ujio wake!!
Hapo kwenye red kaka ni kweli ila sasa tungengoja hadi lini wakati hawa TCRA wamemezeshwa ulimi na Dstv so wanashindwa kusema nao kuhusu kuongeza local channels? Maana wakati huo sie tunangoja hadi wafikie muafaka mambo mengi sana ya ndani yatatupita sasa that was the only way out