KERO Lini Serikali itaondoa changamoto ya kivuko Ferry?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

imekuaje

Member
Jan 28, 2024
34
46
Habari za mchana.

Je, serikali imejipanga vipi na ina mpango upi wa muda mrefu kwa wakazi wa Kigamboni ambao wakuwa wakipata hadha ya kuhangaika na usafiri wa kivuko Ferry takribani mwezi mmoja sasa, kivuko kinachofanya kazi ni kimoja tu MV kazi.

Ambacho kuvuka upande mmoja kwenda mwingine kinatumia takribani lisaa limoja na zaidi.

Hali ambayo inapelekea kuchelewesha shughuli za kila siku za uzalishaji mali kwa wakazi wa Kigamboni wanaofanya shughuli zao mjini.

Nikiwa kama mwananchi wa kawaida ninaomba serikali itupe jibu imejiandaaje na ina mpango gani na shughuli za uvukaji Kigamboni A.

Ahsante.
 
Hivi vivuko kama vile vya Azam Sea Tax kinagharimu bei gani kimoja? Je serikali haina uwezo wa kununua hivyo?
 
Hii seemu kama hakuna Mbunge kabisa yaaan au sijui kajikatia tamaa. Wakazi wa Kigamboni ndio watumiaji wakubwa Kwa stendi ile iliyokua pale ferry ingawa ni jimbo jingine lkn imeondolewa shida wanaopata ni wakazi wa Kigamboni maana wakivuka wanajikuta wanatembea mpk Ohio kule.
 
Hapo Magogoni palitakiwa kujengwa daraja refu ambalo lingeruhusu meli kubwa kupita chini.

Daraja hili lilihitajika zaidi ya daraja la Tanzanite au lile la Nyerere.

Ila, nchi yetu ina tabia ya kuwa na vipaumbele vibaya.
 
Inasikitisha sana

And they don't even care!

Kuna wakati unaweza kumaliza masaa mawili hapo hasa nyakati za jioni
 
Habari za mchana.

Je, serikali imejipanga vipi na ina mpango upi wa muda mrefu kwa wakazi wa Kigamboni ambao wakuwa wakipata hadha ya kuhangaika na usafiri wa kivuko Ferry takribani mwezi mmoja sasa, kivuko kinachofanya kazi ni kimoja tu MV kazi...
Serikali imejenga daraja....umesahau ?
 
Lile daraja limekaa kushoto sana.

Mtu anataka kuja mjini, daraja linampeleka Kurasini karibu na Sabasaba huko.

Yani daraja badala ya kufupisha safari, linarefusha safari zaidi.
Serikali imejenga daraja....umesahau ?.....ipo siku watasitisha mambo ferry pale..nadhani unaelewa hilo
 
Hivi vivuko kama vile vya Azam Sea Tax kinagharimu bei gani kimoja? Je serikali haina uwezo wa kununua hivyo?
Mkuu hivi vivuko navyo ni kama treni ambapo siwezi kununua na kufanya biashara badala ya kuwasubiri hao wapogaji?
 
Mkuu hivi vivuko navyo ni kama treni ambapo siwezi kununua na kufanya biashara badala ya kuwasubiri hao wapogaji?
Sijajua mkuu kuhusu hiyo fursa

Ila ningefahamu bei ya zile sea tax ningefurahi sana

Huku Kigamboni shida kubwa tuliyonayo ni hapo kwenye kuvuka tunapoteza muda mwingi sana
 
Serikali imejenga daraja....umesahau ?.....ipo siku watasitisha mambo ferry pale..nadhani unaelewa hilo
Hakuna uwezekano wa kujenga daraja linaloweza kuwa linarudi nyuma kama kuna meli inataka kupita na baadaye linarudi tena kuendelea kutoa huduma?

Kwanini waafrika hawana utamaduni wa kujali muda?
 
Jibu la hoja hii ni simple, siku ambayo wana kigamboni watafunga Ferry kwa kufanya service protest, ndio siku ambayo mtaiona serikali yote imehamia Ferry,kuanzia rpc rso,rc,hadi minister, kwa sasa endeleeni kulalama humu JF, wakati hakuna majibu humu push back ndio njia pekee
 
Hakuna uwezekano wa kujenga daraja linaloweza kuwa linarudi nyuma kama kuna meli inataka kupita na baadaye linarudi tena kuendelea kutoa huduma?

Kwanini waafrika hawana utamaduni wa kujali muda?
Subiri soon watampa Azam awe anavusha kwa bei zake kila kitu kwake yeye atalipa kodi tu....
 
Yaani unashindwa kuelewa Viongozi wetu,tena wengi WASOMI wanashindwa nini kutatua TATIZO dogo kama hili la KIVUKO cha Kivukoni...haingii AKILiNI kabisaa...

Tunashauri tena,hapo WAPEWE SEKTA binafsi wapaendeshe..tangazeni ZABUNI waje watu wenye uwezo,ziletwe pantoni kubwa na za kisasa zenye KASI,tatizo litabaki historia..serikali ikusanye KODI+ kuboresha hiyo gati

Kama suala ni BEI kubwa,kwa maana Wawekezaji wanaweza kutoza nauli kubwa, Serikali inaweza kuona namna ya kuwapunguzia hao wawekazaji KODI ili gharama(nauli) isiwe kubwa,AU serikali inaweza ikawa inatoa RUZUKU kidogo ..mbona Kamanga ferry imefanikiwa

Labda niseme hivi,CCM mnakwenda kupoteza MAJIMBO ya uchaguzi Kigamboni na Mbagala,2025 kwa KERO ya KIVUKO,labda mnaweza ELEWA na KUSIKIA maana kwenu ninyi KUSHINDA uchaguzi ndio kitu ambacho mnaona cha MUHIMU na sio KUTATUA matatizo ya Wananchi..
 
Sijajua mkuu kuhusu hiyo fursa

Ila ningefahamu bei ya zile sea tax ningefurahi sana

Huku Kigamboni shida kubwa tuliyonayo ni hapo kwenye kuvuka tunapoteza muda mwingi sana
Ni changamoto kubwa sana kwa kweli
Hizo water taxi zipo hapo mkuu ila ni 12 passengers tena ya 2016 kwa £25,000
Ila kwa mchina zipo wasafiri 100 kwa 30m tsh kabla ya usafiri wala ushuru ila hiyo itafaa kama unapata kibali na 30m is nothing
Hii hapa ya 100 passengers unaendesha mwenyewe
Screenshot_20240212_140502_Chrome~2.png
 
Ni changamoto kubwa sana kwa kweli
Hizo water taxi zipo hapo mkuu ila ni 12 passengers tena ya 2016 kwa £25,000
Ila kwa mchina zipo wasafiri 100 kwa 30m tsh kabla ya usafiri wala ushuru ila hiyo itafaa kama unapata kibali na 30m is nothing
Hii hapa ya 100 passengers unaendesha mwenyewe View attachment 2901878
Mbona bei rahisi sana? Sikuwahi kufikiri kitu kama hicho
 
Lile daraja limekaa kushoto sana.

Mtu anataka kuja mjini, daraja linampeleka Kurasini karibu na Sabasaba huko.

Yani daraja badala ya kufupisha safari, linarefusha safari zaidi.
Ukiamua kutumia daraja badala ya pantoni unaongeza 5 au 6km mpakq Posta. Umbali huo na muda unaookoa hapo feri ni afadhali mara 1000!
Nilishaachana na kupita feri, hapo ni jambo la muda tu pantoni itazama na watu.
 
Back
Top Bottom