Kigamboni: Kwa takribani mwezi mmoja, kivuko kipo kimoja tu kinachotoa huduma na kingine kiikiwa kimepaki tu kwa madai kimeharibika

zunya

JF-Expert Member
Sep 2, 2014
1,484
991
Kwanza kabisa nianze kuwapa pole kwa wakaazi wa kigamboni kwa madhira na taabu wanazozipata kwa takribani mwezi mmoja sasa na wamekua wavumilivu.

Kwa takribani ya mwezi mmoja, kivuko kipo kimoja tu kinachotoa huduma, na kingine kiikiwa kimepaki tu kwa madai kimeharibika, huku kukiwa kunaonekana hakuna hata anaejali kuhusu ilo.

Pili, sehemu za kukalia wasafiri (waiting lounge), milango imeanza haribika mmoja baada ya mwingine, na hakuna matengezo. Ivi mpaka mwaka uishe huu ferry si itakua ishakufa kifo cha mende?

Hakuna uwajibika, watu kama watumwa ilihali kila siku watu tunalipa nauli na vivuko havitengenezwi. Kile kilichoenda Kenya kutengenezwa mpaka leo hakijarudi.

Eeeh Mungu sikia kilio cha wana Kigamboni.

#Eeimen
 
Mama si atoke hapo ndani magogoni ashuke chini kwenda kufanya ziara kivukoni uone kama kesho tu hakijawashwa hicho kivuko. Kiugupu ni kuwa watu wanapiga pesa kimyakimya. Trip moja serikalini ,moja nifichie
 
Mama Kizimkazi wanamchekea sana, hawamuoni kama katili, roho mbaya, wanaona ni kama mzee wa ruksa, na wapigaji wenyewe wanajua baada ya mama mambo yanaweza kuja kuwa magumu tena.
 
Kwanza sio kwa 'madai kimeharibika', kimeharibika kweli na mafundi wanaendelea na matengenezo afu we unaonekana sio mkazi wa Kigamboni
 
Mama si atoke hapo ndani magogoni ashuke chini kwenda kufanya ziara kivukoni uone kama kesho tu hakijawashwa hicho kivuko. Kiugupu ni kuwa watu wanapiga pesa kimyakimya. Trip moja serikalini ,moja nifichie
Kivuko cha Magogoni kilikwenda Kenya kutengenezwa mwezi tatu, tuliambiwa kitakamilika ndani ya miezi mitano! Sasa mwaka sasa unakaribia, Watanzania na Tanzania yangu Mwenyezi Mungu aendelee kutulinda! Mungu Ibariki Nchi Yangu Mungu Ibariki Afrika!!
 
Binafsi sitoi pole yeyote kwa wakazi wa kigamboni, uoga wao wa kizuzu wa kufanya push back ndio wanaovuna, why wasifanye service protest pale Ferry?,maana hii itamfanya RC na Waziri wakimbulie pale kwenda kuwasikiliza, humu JF hakuna solutions
 
Kwani Daraja la Nyerere (Kigamboni) lilijengwa kwa kazi gani?

Kwanini mpige mbizi hapo Ikulu wakati daraja lipo?
 
Hapo tu karibu na ikulu watu hawawajibiki hata hawaogopi mama anaweza fanya jogging akakuta huo uozo.Sasa jiulize walioko mikoani huko si ndo wanacheza mziki kabisa.Pale mpaka yatokee maafa ndo utasikia kelele za viongozi.Mkuu wa wilaya ya kiga yupo kimyaaa na mkuu wa mkoa yuko wapi sijui.
 
Kwanza kabisa nianze kuwapa pole kwa wakaazi wa kigamboni kwa madhira na taabu wanazozipata kwa takribani mwezi mmoja sasa na wamekua wavumilivu.

Kwa takribani ya mwezi mmoja, kivuko kipo kimoja tu kinachotoa huduma, na kingine kiikiwa kimepaki tu kwa madai kimeharibika, huku kukiwa kunaonekana hakuna hata anaejali kuhusu ilo.

Pili, sehemu za kukalia wasafiri (waiting lounge), milango imeanza haribika mmoja baada ya mwingine, na hakuna matengezo. Ivi mpaka mwaka uishe huu ferry si itakua ishakufa kifo cha mende?

Hakuna uwajibika, watu kama watumwa ilihali kila siku watu tunalipa nauli na vivuko havitengenezwi. Kile kilichoenda Kenya kutengenezwa mpaka leo hakijarudi.

Eeeh Mungu sikia kilio cha wana Kigamboni.

#Eeimen
Nimepewa habari na mmoja wa wafanyakazi hapo anasema kivuko kimoja kimekufa Gearbox na imetoka pesa milion KADHAA kununua Gearbox ingine ambayo IMEFANYA KAZI SIKU 3 TU na Kufa tena.

Wizi wa diesel na oil na vifaa vya kufanya service unafanyika wazi kabisa.
Nimeambiwa mkuu wa hapo Kivukoni kabadilishwa lkn Uozo ni ule ule.
Diesel na vifaa vingine vinaibiwa na kupakiwa kwenye vibajaj kila siku.
Mishahara ya wafanyakazi hapo Inachelewa mpk miezi miwili.

Hii hali wakati wa Magufuli haikuwepo.
Hawa watu Rais anatakiwa kuwashughulikia sana tena haraka.
Wanaiba mpk vifaa vya service za hizo feri hii nchi inarudi kule kule tulikotoka.

Mwendo kasi wameiba vifaa mpk sasa mabasi 144 yamekufa kabisaa.

Shida wanapata wananchi.
Wabunge na walioko serikalini wanatembea kwenye magari ya serikali.
Mafuta Bure, full Air conditioning.

HII DHULMA IKARIPIWE NA KILA MZALENDO.
Enyi mnaoiba Mali za wananchi Mungu awalaani .
Mnatesa wanyonge kwa tamaa zenu binafsi.
Mungu yupo.
Lzm mtakuja kujuta tu.
Wengi wenu Saratani za tumbo lzm ziwaondoe Duniani manake matumbo yenu yamejaa MALI ZA HARAMU TUPU.
maadui wa ummah msio na huruma hata kidogo.
 
Duh....

Ova
 
Back
Top Bottom