ndiyomkuusana
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 668
- 426
hawajatoa picha yake?
Siwashukuru polisi kwa kumtangaza huyo shetani kwamba ni kinara wa vurugu za kidini hapa nchini ila nataka kuanza kuwaelewa kwamba sasa walau wanadalili za kuamka kwa kumwagiwa maji na kupigwa nyundo kwenye magoti...Lakini wamejiuliza yafuatayo kuhusu hawa jamaa wawili?hawajatoa mkuu
Ni rahisí tu kulambà hiyó Bingo, ni kiasí tu chá kujitokezà kwenyé kituô chá Polisi na kuwajulishà kuwa mtuhumiwa waó Sheikh Isso Bungó unafahanú alipojifichà kwã hiyiô waulizé maafande, utakapowaonyesha huyó mtu waó waó watakupà bei ganí?!Shs ngapi nikiwatajia alipo?
kweli polisi imeishiwa mbinu
nafikili wanajamvimeeanza tabia mbaya ya kuajadili watu. tanzania haina udini mimi naamini hivyo tatizo ni selikali hii kuegemea na kulipa kanisa nguvu ya dola. ukiachilia kushidwa kusimamia haki kwa wanajamii wote. waislamu wamekuwa wakitaka uwepo mjadala wa kitaifa kujadili hali hii. ungekuwa ni udini leomie nisingewza hata kupanda daladala na mkristo. tatizo ni selikali. hivi inaingia vipi akililini msafara wa shekh ponda unaoaskari zaidiya themanini kwa nini wengine waisende kuyalinda makanisa huko zenji. selikali hii imejikita katika kuwadunisha waislamu. kwanini waziri anaagizauchunguzi wakati ameshajiridhisha kwamba kumuua padri ni ugaidi ila kumuua kamanda wa polisi wa mkoa wa mwanza ulikuwa ni uhalifu. tuache kuchochea huo udini selikali ikubali kusikiliza wanachokitaka waislamu na wakristo badala ya mawaziri wanaoongea kwa hisia za chuki wakidai kuwa ni kauli ya selikari. je leo waumini wa kiislamu wakiamuua kuibua kashifa za kanisa katoliki na maaskofu wake tena tukachochea kuwa kuwa hayo ndo mafundisho ya ukatoliki. jamani yatosha sasa selikali ijifunze uadilifu.
:nimekataa
Sasa bila picha tutamjuaje huyu Sheikh???
Siwashukuru polisi kwa kumtangaza huyo shetani kwamba ni kinara wa vurugu za kidini hapa nchini ila nataka kuanza kuwaelewa kwamba sasa walau wanadalili za kuamka kwa kumwagiwa maji na kupigwa nyundo kwenye magoti...Lakini wamejiuliza yafuatayo kuhusu hawa jamaa wawili?
1.SHEHE BUNGO 2.UST.ILUNGA
Amechochea vurugu ili ponda awekewe dhamana Anahimiza mapadri kuuwawa bila sababu zozote
Amechoma kanisa kwa msahafu kukojolewa Amesababisha mauaji ya viongozi wa kikristo wawili
Amesababisha hofu Dar Es Salaam Wafuasi wake wanaendelea kuwawinda wakristo mpaka sasa
Amechochea wafuasi wa ponda kuvamia kiwanja Anasababifu hofu kwa taifa zima.
Anatafutwa kwakuwa hana makazi maalumu Anaishi Mwanza mtaa wa bugarika nyumba no.157
Lengo ni kuonyesha jinsi gani polisi wasivyokuwa makini na walivo na Double standard kwa wahalifu wa aina moja.
Shehe Ilunga ni mtu anayetokea kijiji kimoja na mke wa rais hivyo wanaukaribu na yeye hutumia ukaribu huu kuamini kwamba hawezi kukamatwa maana anamaslahi na mwenyeji wa Ikulu na ndicho kinachofanyika mpaka sasa kwamba ukilinganisha makosa huyu anayetafutwa Shehe Bungo na huyu Ilunga utagundua kwamba Ilunga in zaidi ya haini kwa mahubiri yake na Kanda nyingi za uchochezi zilizosambaa karibu nchi nzima.Kama wangekuwa wapo huru Ilunga alipaswa kukamatwa mapema sana kabla ya Bungo maana hata anapoishi panafahamika,ni maarufu kuliko Bungo anapatikana kirahisi kuliko...Polisi hamtamaliza uhalifu kwa Kumwacha Huyu Gaidi ambaye ameanzisha Chuo cha Ugaidi pale Ukerewe.
Polisi watangaza bingo atakayesaidia kumpata
na Farida Ramadhani
KINARA wa vurugu za kidini zinazoibuka kila siku ya Ijumaa jijini Dar es Salaam, amejulikana. Kinara huyo ametajwa kuwa ni Sheikh Issa Kondo Bungo ambaye amekuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu bila mafanikio. Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, zilisema kuwa Sheikh Bungo anadaiwa kuhusika na matukio kadhaa makubwa ya vurugu za kidini, zilizotokea kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam.
Duru za kipolisi zilitaja baadhi ya matukio ambayo Sheikh Bungo anadaiwa kuhusika nayo kuwa ni pamoja na tukio la kuchoma moto kanisa la TAG la Mbagala, baada ya mtoto (jina limehifadhiwa), kukojolea Quran. Tukio la kukojolea kitabu hicho lilitokea Oktoba 10 katika eneo la Chamazi saa 10 jioni wakati watoto hao wakiwa katika kijiwe chao cha kuchezea mpira.
Vurugu hizo zilisababisha kuvunjwa kwa vioo vya magari, madirisha ya makanisa pamoja na kuibwa kwa vifaa vya kwaya katika makanisa hayo ambayo ni ya Anglikana, Wasabato na Pentekoste. Kutokana na tukio hilo ambalo liliibua vurugu kubwa kutoka kwa baadhi ya waumini wa Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali, Sheikh Bungo anatajwa kuhusika kushawishi wenzake kuchoma kanisa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Jeshi la Polisi limekuwa likimsaka kwa muda mrefu, lakini halijafanikiwa kumtia mbaroni kutokana na staili yake ya kuishi kwani hana makazi maalumu. Shekh huyo pia anahusika kushawishi wafuasi wa Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Ponda Issa Ponda kuandamana kila siku ya Ijumaa ili kushinikiza mahakama itoe dhamana kwa Ponda ambaye kwa sasa yuko rumande akikabiliwa na kesi ya uchochezi, kilisema chanzo chetu cha habari.
Kwa mujibu wa habari hizo, tangu tukio la vurugu za Mbagala lilipotokea, Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata wafuasi wa sheikh huyo na wengine wako mahakamani, lakini yeye hajapatikana. Tayari Sheikh Bungo pamoja na wenzake wamefunguliwa kesi namba THA/ IR/ 7794/ 2012 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mwaka huu tumeshamfungulia jalada lingine namba CHA/ RB/ 10652013 katika kituo cha polisi cha Changombe, hivyo tunawaomba wananachi wanaopenda amani watoe taarifa katika kituo chochote cha polisi endapo ataonekana, alisema mtoa habari wetu.
Hadi sasa polisi imemfikisha mahakamani Shekh Ponda pamoja na wenzake 49 ambao kesi zao zinaendelea kusikilizwa huku wakiendelea kukamata wengine kila vurugu hizo zinapotokea. Vurugu hizo ambazo zimekuwa zikiwatia hofu wakazi wengi jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla, zimekuwa na tabia ya kuibuka kila siku ya Ijumaa na siku ambazo kesi ya Sheikh Ponda inapotajwa. Hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya shughuli za kimaendeleo katika jiji hilo kusimama kwa muda, huku polisi wakilazimika kutumia nguvu kubwa kuweka ulinzi.