Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Abdulrahman Kinana amesema hana mpango wa kuwahoji Wajumbe wa Bunge Maalumu laKatiba wanaotokana na chama hicho kwa sababu ya misimamo yao inayokinzana namiongozo ya chama, kwa kuwa anawafahamu wote kwa majina na idadi yao haizidikumi. Kauli hiyo yaKinana inafuatia taarifa zilizoripotiwa na gazeti hili hivi karibuni kuwa, CCMkimeanza kuwahoji baadhi ya wabunge wake, ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu laKatiba kwa sababu ya kupingana na maelekezo ya chama hicho kuhusu Muundo waSerikali mbili. Sisi (CCM)hatuhoji mtu kwa sababu ya kuwa na msimamo tofauti, kwani hawa wenye msimamotofauti na chama hawazidi kumi ama siyo zaidi ya 15, alisema Kinana nakuongeza; Hawa watu miminawajua kwa majina, mmoja (jina tunalo) ni hatari zaidi kwa sababu anawezakuwakusanya wengine na kuwashawishi wafuate msimamo wake, lakini waliobakiwote, hawatishi kwa kuwa wanabaki na misimamo yao wenyewe. Kwa mujibu wahabari hiyo, wajumbe waliohojiwa ni wale wanaotokana na Ubunge wa Jamhuri yaMuungano na ambao wanataka Muundo wa Serikali tatu. Ni kweli hata miminiliitwa na akaniambia (mwakilishi wa chama) ametumwa aniletee ujumbe kuwa nikokwenye orodha ya watu 90 na nikiendelea na msimamo wangu nitachukuliwa hatua,alieleza mmoja wa wajumbe waliodai kuwa wamehojiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu yaCCM.
Kura ya wazi na Serikali mbiliKatika hatuanyingine, Kinana alizungumzia msimamo wa chama hicho wa kura ya siri na muundowa Serikali mbili, akieleza kuwa siyo jambo la ajabu, kwani katika mchakato wakutunga katiba, kila kundi lina maoni na mtazamo wake na kuutetea kwenyemijadala. Wanaosema kunavyama havina msimamo pale bungeni ni waongo. Siyo vyama tu, kila kikundi kinamsimamo unaotokana na uchambuzi wao wa hali ya siasa nchini na wanachofikirikina masilahi kwa nchi na watu wanaofuata mtazamo wao. Hawawezi kuniambia kamaLipumba (Profesa Ibrahim) na Mbowe (Freeman), hawana wanachosimamia kwenyemjadala huo wa Bunge Maalumu, alisema na kusisitiza: Watanzaniawasitarajie miujiza, lazima mivutano ya aina hiyo iwepo, kwani kila kundilinajitahidi kupenyeza mawazo yake na wanaoitetea misimamo hiyo ni watu.Kikubwa hapa sasa ni uvumilivu, watu wavumiliane na wazungumze kwa hoja namwisho wa yote wafikie mwafaka. Alipoulizwa kamani kweli CCM imekuwa ikiwashinikiza wajumbe wake kusimamia matakwa ya chamahicho, alijibu Siyo CCM tu, CUF wanakutana na Chadema wanakutana, tena kilasiku. Hili ni jambo la kawaida. Anasema tatizosiyo chama kuwa na msimamo, bali chama kutokukubali kubadili misimamo yake hatakama haikuwa sawa. Unaweza kuwa na msimamo wako, lakini ukaja mbele ya wenzako,ukagundua kuwa hauko sahihi, ikifikia hapo unapaswa kulegeza kamba ili uingizemawazo ya wenzako pia kwenye hoja zako, alisema. Wito kwa Wajumbe wa Bunge la KatibaKinana ametoa witokwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba akiwataka watambue kuwa Tanzania siyonchi ya kwanza kutengeneza katiba. Alisema zipo nchinyingi duniani, ikiwamo India, Indonesia, Columbia, Kenya na Pakistan ambazozilitumia muda mrefu zaidi kutunga katiba zao. Sisi kutumiamajuma matatu kutengeneza kanuni za kuongoza Bunge Maalumu la Katiba, ni hatuanzuri tunayopaswa kujivunia, alisema. Kinana aliendeleakueleza kuwa pamoja na tofauti zinazojitokeza katika mijadala ya Bunge hiloMaalumu, makundi yanayounda Bunge hilo yanapaswa kutambua utaifa na uzalendo naikilazimika waache tofauti zao ili wawe na mwelekeo wa pamoja katika kufikiamwafaka unaokusudiwa. Kwa hali hiyopamoja na tofauti zetu, tusiondoke kwenye lengo. Mimi naamini katibatunayoitaka itapatikana ila safari ya kuipata ni ndefu na ngumu.
chanzo: mwananchi