MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Katibu Mkuu, Kinana akiingia Hanang, Mkoa wa Manyara
Mapokezi ya Kinana Kijiji cha Gehandu, Hanang Manyara
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Vijana wa UVCCM, wakati wa mapokezi yake, Kijiji cha Gehandu, Hanang Manyara
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mapokezi yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, wakati Kinana alipowasili katika Wilaya ya Hanang, akitokea mkoani Singida, kwenda kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na njia ya kuzitatua katika mkoa wa Manyara
Waziri Mkuu msaafu, Sumaye akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika mapokezi ya Kinana yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, Wilaya ya Hanang, Manyara. Kushoto Mkuu wa wilata hiyo Mndeme
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu wakati wa mapokezi hayo
Nape akisalimiana na Mbunge wa Babati Vijijini, Jeetuson Patel wakati wa mapokezi kuingia wilaya hiyo Hanang
Vijana wa Kibarbaig wakionyesha ushupavu wao wa kuruka wakati wakimburudisha Kinana wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Gehandu, wilayani Hanang
Katibu Mkuu, Kinana na Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye wakicheza ngoma ya asili ya watu wa Hanang
=========================================================
Katibu Mkuu baadaye alianza kazi za kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga misumari kwenye kenchi kwenye jengo la maabara ya shule ya Sekondari ya Mwahu Kata ya Kihandu, wilayani Hanang
Katibu Mkuu, Kinana akiwatubia wananchi kwa maelfu katika viwanja vya ofisi ya CCM, Wilaya ya Hanang kwenye mji wa Katesh.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape akihutubia wananchi kwa maelfu waliojitokeza katika mkutano kwenye viwanja vya CCM, mjini Katesh, Hanang.
Mh. Dkt. Mary Nagu ambaye ni mbunge wa Jimbo la Hanang, akiwatubia wapiga kura wake.
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu wakijadili jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Katesh mkoani Manyara,
Picha juu:Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hanang, Agustino Mayumba akiuliza swali kuhusu mapato ya mnara wa simu uliojengwa katika eneo la soko Kata ya Basotu.
Picha chini: Katibu Mkuu, Kinana akimwelekeza Mwenyekiti wa CHADEMA, nini cha kufanya baada ya kubainika kuwa ni yeye aliyesaini Mkataba wa mnara wa Vodacom.