Kinana na timu yake waanza ziara ya Mkoa wa Manyara, wahutubia maelfu ya wananchi Katesh, Hanang

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Katibu Mkuu, Kinana akiingia Hanang, Mkoa wa Manyara

Mapokezi ya Kinana Kijiji cha Gehandu, Hanang Manyara

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Vijana wa UVCCM, wakati wa mapokezi yake, Kijiji cha Gehandu, Hanang Manyara

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mapokezi yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, wakati Kinana alipowasili katika Wilaya ya Hanang, akitokea mkoani Singida, kwenda kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na njia ya kuzitatua katika mkoa wa Manyara

Waziri Mkuu msaafu, Sumaye akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika mapokezi ya Kinana yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, Wilaya ya Hanang, Manyara. Kushoto Mkuu wa wilata hiyo Mndeme

Kinana akisalimiana na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu wakati wa mapokezi hayo

Nape akisalimiana na Mbunge wa Babati Vijijini, Jeetuson Patel wakati wa mapokezi kuingia wilaya hiyo Hanang

Vijana wa Kibarbaig wakionyesha ushupavu wao wa kuruka wakati wakimburudisha Kinana wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Gehandu, wilayani Hanang

Katibu Mkuu, Kinana na Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye wakicheza ngoma ya asili ya watu wa Hanang
=========================================================

Katibu Mkuu baadaye alianza kazi za kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga misumari kwenye kenchi kwenye jengo la maabara ya shule ya Sekondari ya Mwahu Kata ya Kihandu, wilayani Hanang

Katibu Mkuu, Kinana akiwatubia wananchi kwa maelfu katika viwanja vya ofisi ya CCM, Wilaya ya Hanang kwenye mji wa Katesh.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape akihutubia wananchi kwa maelfu waliojitokeza katika mkutano kwenye viwanja vya CCM, mjini Katesh, Hanang.

Mh. Dkt. Mary Nagu ambaye ni mbunge wa Jimbo la Hanang, akiwatubia wapiga kura wake.

Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu wakijadili jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Katesh mkoani Manyara,

Picha juu:Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hanang, Agustino Mayumba akiuliza swali kuhusu mapato ya mnara wa simu uliojengwa katika eneo la soko Kata ya Basotu.
Picha chini: Katibu Mkuu, Kinana akimwelekeza Mwenyekiti wa CHADEMA, nini cha kufanya baada ya kubainika kuwa ni yeye aliyesaini Mkataba wa mnara wa Vodacom.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Ziara ya Kinana yamtoa kigogo Dar

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo ameanza ziara mkoani Tabora kukagua vituo vya afya vilivyotelekezwa.

Pallangyo amechukua hatua hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana kufanya ziara mkoani Tabora na kushuhudia namna vituo vya afya vilivyotelekezwa huku wananchi wakikosa huduma za afya.

Kinana alitishia kuwa atakabidhi majina ya mawaziri na watendaji wa Serikali wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanadaiwa kutoa zabuni yenye thamani ya sh. bilioni 7 kwa Kampuni ya Humphrey Contraction Ltd kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya
Hospitali ya Kitete yenye vituo vya afya lakini vimetekelezwa.

Inadaiwa kuwa mkandarasi huyo alipewa kazi ya kufanya ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Kitete na kujenga jengo la chuo cha uuguzi katika hospitali hiyo.

Ilielezwa kuwa mkataba kati ya Serikali na mkandarasi huo ulisainiwa Oktoba 28, 2009 ambapo alitakiwa kukamilisha kazi hiyo mwaka 2012 lakini ameshindwa kufanya kazi aliyopewa. Pia alipewa kazi ya kujenga vituo vya afya wilayani Sikonge kwa thamani ya sh. bilioni 2.5.

Kuhusiana na ziara ya katibu huyo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa alisema ni ya kweli. "Alhamisi kuna ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, atatembelea hospitali na vituo vya afya ambavyo vimetelekezwa na mkandarasi.

"Tuna matumani kwamba ziara hii itakuwa dira kwetu hasa katika kuimarisha huduma za afya kwa jamii na wananchi wa mkoa wa wetu wa Tabora," alisema Mwassa.
Chanzo: Nipashe.
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Hizi siyo picha za kutuonyesha baada ya miaka zaidi ya 50 ya utawala. Same old dirty tricks! Mwalimu Nyerere alipohojiwa juu ya kwa nini anaamua kung'atuka na kuacha Urais, alisema,"Kama kuna kitu nimeshindwa kukifanya katika muda wa kuiongoza nchi hii kwa miaka 24, basi siwezi tena kukifanya hata kwa miaka mingapi mingine, hivyo ni bora nikawapisha wengine." Ni wakati sasa kwa Chama kilichotawala nchi hii kwa zaidi ya miaka 50, nacho kujifunza kwa Nyerere, na kujua vivyo hivyo kwamba, kile ambacho mmeshindwa kukifanya kwa zaidi ya miaka 50, hamuwezi kukifanya hata mngepewa miaka mingine mingapi! You have reached the end of the road! Hamna tena mawazo na mbinu mpya za kuikwamua nchi hii kutoka katika umaskini wa kutupwa. Muwe waungwana, kwa faida ya Taifa hili, wapisheni wengine!!!!
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Kinana songa mbele watanzania wengi wako nyuma yako imani yao kwako ni kubwa sana watumikie watanzania pamoja na chama pendwa chenye kujali watu na maisha yao kwa ujumla.
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Hizi siyo picha za kutuonyesha baada ya miaka zaidi ya 50 ya utawala. Same old dirty tricks! Mwalimu Nyerere alipohojiwa juu ya kwa nini anaamua kung'atuka na kuacha Urais, alisema,"Kama kuna kitu nimeshindwa kukifanya katika muda wa kuiongoza nchi hii kwa miaka 24, basi siwezi tena kukifanya hata kwa miaka mingapi mingine, hivyo ni bora nikawapisha wengine." Ni wakati sasa kwa Chama kilichotawala nchi hii kwa zaidi ya miaka 50, nacho kujifunza kwa Nyerere, na kujua vivyo hivyo kwamba, kile ambacho mmeshindwa kukifanya kwa zaidi ya miaka 50, hamuwezi kukifanya hata mngepewa miaka mingine mingapi! You have reached the end of the road! Hamna tena mawazo na mbinu mpya za kuikwamua nchi hii kutoka katika umaskini wa kutupwa. Muwe waungwana, kwa faida ya Taifa hili, wapisheni wengine!!!!
Mkuu unataka kusema nini mambo yaliyofanywa na ccm ni zaidi ya unavyodhani kama shida yako ni picha siyo maendeleo waliyoletewa wananchi pengine unataka sifa kama hizi anazopiga kiongozi wako.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Hizi siyo picha za kutuonyesha baada ya miaka zaidi ya 50 ya utawala. Same old dirty tricks! Mwalimu Nyerere alipohojiwa juu ya kwa nini anaamua kung'atuka na kuacha Urais, alisema,"Kama kuna kitu nimeshindwa kukifanya katika muda wa kuiongoza nchi hii kwa miaka 24, basi siwezi tena kukifanya hata kwa miaka mingapi mingine, hivyo ni bora nikawapisha wengine." Ni wakati sasa kwa Chama kilichotawala nchi hii kwa zaidi ya miaka 50, nacho kujifunza kwa Nyerere, na kujua vivyo hivyo kwamba, kile ambacho mmeshindwa kukifanya kwa zaidi ya miaka 50, hamuwezi kukifanya hata mngepewa miaka mingine mingapi! You have reached the end of the road! Hamna tena mawazo na mbinu mpya za kuikwamua nchi hii kutoka katika umaskini wa kutupwa. Muwe waungwana, kwa faida ya Taifa hili, wapisheni wengine!!!!
Ndugu, Nani alikudanganya kama uungwana ni kukabidhi madaraka pekee?.

Kuna mchakato wa kukabidhi madaraka na katika mchakato huo, wananchi ndiyo wanaoamua nani wampatie hayo madaraka.

CCM inapokabidhiwa madaraka, kuna kuwa na makubaliano na wananchi walio wengi ya kuyashika, kuyatunza na kuyaenzi katika njia ya kimaendeleo mpaka baada ya miaka mitano.

Unapoona CCM inaendelea kukabidhiwa madaraka kila baada ya miaka mitano basi, huna budi uelewe kuwa, CCM bado inaaminiwa na wananchi walio wengi kwa sababu inafanya kile ambacho wanaitaka wananchi ikifanye kwa faida yao.
 
hans79

JF-Expert Member
May 4, 2011
3,802
1,225
Kweli maccm mmeishiwa yaani copy & paste toka M4C.

CHADEMA PAMOJA NA UKAWA VIDUMU DAIMA KWA UWEZO LA RAB .
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Kweli maccm mmeishiwa yaani copy & paste toka M4C.

CHADEMA PAMOJA NA UKAWA VIDUMU DAIMA KWA UWEZO LA RAB .
Ndugu, CCM wameishiwa kitu gani?.

M4C kwa sasa ni historia.

Viongozi wa CHADEMA wameyakimbia mapungufu yao na kujificha kwenye kikundi wanachikiita UKAWA.
 
kababu

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,593
2,000
KWELI CCM NI BABA WA VYAMA, MENYEKITI WA CHADEMA AKIWA ANAWAJIBIKA CHINI YA KATIBU MKUU WA CCM,
KUMBE CCM NDIO KILA KITU, VIVA CCM, AMAN KWENU NYOTE

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,386
2,000
Hapo ni haki akina Tambwe Hizza walalamike. Naona Nepi na mzee Wa tembo wameamua kupiga hela, hii mizunguko ya Tanzania nzima si watajenga maghorofa wakati wenzao wanapiga miayo tu? Kwa nini wasingeigawa nchi kwa makundi ili na wengine waende upande mwingine? Sasa hivi ni wale wale tu, wakiamua kwenda na akina Shonza na Stella Mwampamba labda wanaenda kuwavua nyupi. kazi kweli kweli!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Kinana kaba mpaka wasipumue tena, juzi nilikuomba uregeze kamba, nimefuta ile kauli yangu.

Nakuomba zidisha kukaba, hawa wasaliti hawafai hata kuwepo Tanzania, waende Rwanda.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
2,000
Maccm wote mapumbavu kabisa, eti mwenyekiti wa chadema wilaya kasaini mkataba wa vodacom duh!
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
2,000
Kinana kaba mpaka wasipumue tena, juzi nilikuomba uregeze kamba, nimefuta ile kauli yangu.

Nakuomba zidisha kukaba, hawa wasaliti hawafai hata kuwepo Tanzania, waende Rwanda.

Aibu yao maccm kwenye serikali za mitaa na 2015
 
daniel merengo

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
278
0
CCM baada ya kugundua kwamba hwakubaliki tena na hawapati watu kwenye mikutano yao wameona waanzishe hii style ya kukaa kwenye viti ili kuonyesha kwamba wanapata watu wengi kwenye mikutano.kama una akili timamu angalia hizo picha hapo juu uone ukweli ccm is dying.

Wewe bwana mdogo acha uvivu wa kufikiri nani amekwambia kinnana ataboresha huduma za afya? au ndio kusema kwamba kuwamwanaccm lazima uweke akili pembeni na kutumia makalio kufikiri?
 
cerxm

Member
Nov 14, 2013
56
95

Hata kama unakengeza lako limezidi hapo waliokaa ni kama mistar mitano tena hapo mbele yajukwaa ni wazee hao wa kijiji waliobak wote wamesimama
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom