Kinana aivua nguo Serikali ya CCM!

Kinana aivua nguo Serikali ya CCM!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Duniani kuna vituko sana. Ni jana tu,Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana ameivua nguo Serikali ya chama cha Mapinduzi.

Akiwa ziarani mkoani Njombe,Kinana ameitaka Serikali izungungumze na wananchi wake kabla ya kuanzishwa kwa miradi ya maendeleo.Amedai kuwa Serikali ( tena ya CCM) haina utaratibu wa kuzungumza na wananchi wake na kusababisha kutokea kama yale ya Mtwara.

Waungwana,haya kweli ni maneno ya Kinana kuzungumza mbele ya wananchi? Alilenga kuwalaghai au kuidhalilisha Serikali? Nani atamwamini Kinana,mtu mwenye nafasi mujarabu wa kushauri vikaoni mambo kama haya kwa kuimarisha chama na Serikali ya chama chake?

The next Hollace Kolimba in speech?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Huwa magamba hawaeleweki leo anaongea hiv kesho vile.
 
itakuwa amerishwa ayo maneno, si yake. kama anajua tatizo ni ccm na bado wana shupaza shino, basi ajue itakatwa tu.
 
Huwa siwaelewi viongozi wetu.wapo kama vinyonga
Akiwa kama katibu amechukua hatua gani kukishauri chama?
 
...hakusema chochote kuhusu serikali kushughulikia majangili? na vipi kuhusu wang'oa kucha, meno na macho? vipi kuhusu wauaji wa Mwangosi?.
Aseme yote asichaguechague.
 
Mi naona kama Kinana anashurutishwa tu kufanya hiyo kazi, hotuba zake zote huwa haziendani na matendo ya viongozi wote wa serikali ya ccm kuanzia kwa wafagiaji mahofisini mpaka kwa Rais.

Kazi yenyewe hii inamsababishia watu kuvuatilia biashara zake na kutoa matamko ya ajabu ajabu yanayomchafulia jina na sifa yake ndani na nje ya nchi.

Utendaji kazi wake wote unatoa picha kwamba kuna uwezekano mkubwa yuko blackmailed, anafanya kazi ambayo anajua hailipi, laiti mngejua ni maneno gani aliyasema akiwa kwenye kikao fulani hivi karibuni, mngebaki mdomo wazi.
 
Hauwezi kuongoza kwa kufuata upepo, unachokoza mada kisha unasikilizia...hii ndiyo maana ya kukosa dira
 
Aliyasema hayo kumfurahisha Deo Filikunjombe. Kumbuka alikuwa Ludewa na Ludewa kuna mgodi wa makaa ya mawe. Filkunjombe huwa hana huo "UPOPO" wa CCM aliogopa angeweza kumlipua hapo jukwaani LIVE.

Kama anajua hivyo kwanini basi asiishauri SERIKALI ikae na Wananchi wa Mtwara kuhusu suala la gesi?
 
Duniani kuna vituko sana. Ni jana tu,Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana ameivua nguo Serikali ya chama cha Mapinduzi.

Akiwa ziarani mkoani Njombe,Kinana ameitaka Serikali izungungumze na wananchi wake kabla ya kuanzishwa kwa miradi ya maendeleo.Amedai kuwa Serikali ( tena ya CCM) haina utaratibu wa kuzungumza na wananchi wake na kusababisha kutokea kama yale ya Mtwara.

Waungwana,haya kweli ni maneno ya Kinana kuzungumza mbele ya wananchi? Alilenga kuwalaghai au kuidhalilisha Serikali? Nani atamwamini Kinana,mtu mwenye nafasi mujarabu wa kushauri vikaoni mambo kama haya kwa kuimarisha chama na Serikali ya chama chake?

The next Hollace Kolimba in speech? Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Atoke vipi sasa? na atmosphere ndo hiyo imebana kotekote. Advance party watakuwa wamemwambia pengine akisema hivyo ingalau watu watakaa na japo wamsikilize kwa dakika kadhaa mkutanoni. Tutarajie hotuba za namna hiyo zaidi ikiwa njia ya kuwafanya watu japo wakae mkutanoni. Meseji hasa kutoka CCM watakuwa wananyunyiza kwa mbaaaaali, katikati ya lugha za namna hii. That is politics
 
Ndo zao kile chama, yaani huwa wanatiririka tu kama wamekatwa vichwa...
 
Sangarara hembu tuambie maneno gani hayo aloyasema, hata kama tukibaki midomo wazi, sawa tu, maana sana sana inzi wataingia midomo ikiwa wazi, ila tutakuwa tumejifunza kitu.
 
...hakusema chochote kuhusu serikali kushughulikia majangili? na vipi kuhusu wang'oa kucha, meno na macho? vipi kuhusu wauaji wa Mwangosi?.
Aseme yote asichaguechague.

mmoja ni Lakatare ana nyea debe
 
Kama serikali haifanyi kazi kwa akili maana yake ccm ni boga!...anatakiwa yeye aanze kujiuzulu!
 
hiyo ni kwa Tanzania mzima,kuna miradi ya maji ,barabara inapita kwenye maeneo ya watu,kasisitiza washauriane nalenngwa sasa ubaya upo wapi???kusema nawananchi kwanza!!!!
 
Back
Top Bottom