Kinana acharuka: Adai kampuni ni yake lakini meno ya Tembo si yake!

8D6U9156king+maker.JPG
14.JPG
NECKikao.jpg
 
kinana aache utoto.kitendo cha kuhusishwa tuu kwa namna yoyote na kampuni inayohujumu uchumi ni cha aibu kubwa na kilitosha kwa yeye kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya ccm.kuikubali kampuni na kuyakana yanayofanywa na kampuni kwa maelezo dhaifu eti sihusiki na uendeshaji haitoshi kumuondolea kinana wingu zito la ufisadi.
 
acha uongo,,hiyo kampuni haikagui mizigo,,lazima uwe muelewa ebu toa ushahidi wa hiyo kampuni ya Malekani
Punguza jazba, Malekani ndio wapi ndugu, hata hivyo ukiwa kiongozi, kampuni yako ikitajwa kwenye kashfa, hata kama haina uhusiano wa moja kwa moja na shughuli unavyofanya, unaachia ofisi. Waungwana wanafanya hivyo, ndio maana kwa wenzetu waliostaarabika, kashfa yoyote mtu anaachia madaraka.

Na unakuwaje wakala usijue kinachosafirishwa, hawezi kukwepa kashfa hii kinana.
 
huu ni mwanzo tu jamani huyu mtu aliwekwa kando miaka ya nyuma hapa kwa kashfa za chini kwa chini like that,,lkn tabia ya ccm ya kulindana ndo utamaduni wao.cku moja historia itawahukum,,

 
I'm convinced kabisa huyu jamaa anahusika na huwa wanajua nini kinasafirishwa maana wanasiasa hawapendi kuchafuliwa na magazeti au kukumbwa na kashfa so ni lazima ajue kampuni hii na zingine zote anazomiliki zinafanya nini all the time.Hizi dili wanapiga sana tu,wao wanadhani sisi hatujui,wanauza meno na wanyama hai wengi sana nje ya nchi na hata vigogo wa MALIASILI wanahusika pia.Inatia hasira sana,Then wakihojiwa wanatoa majibu mepesi mepesi mnooo,na cha ajabu hakuna atakayewajibishwa katika hili maana ni upepo tu nalo pia litapita................TILL ONE DAY WHEN SONS OF MEN DECIDE TO RECLAIM THEIR COUNTRY.
 
Contena zingekuwa zimebeba madawa ya kulevya wangesema hawajui kilichomo? Acheni kuwafanya watu na akili ni punguwani. Kinana alikuwa anafaham ni nini kinasafirishwa.
 
JK ni jembe la Magamba. Kumweka Kinana hapo ni kuficha uozo wa CCM na Serikali kwa kuwa anafahamu Kinana ni Wakala wa CCM na JK kujilimbikizia mali kupitia mauzo ya maliasili za nchi yetu. Nchi yetu imeshauzwa.
 
Rafiki wa mwizi akiwa polisi unategemea usalama gani?...huyo ndio katibu mkuu wa chama cha magamba.
 
Kinana kwa nini ulifungua kampuni ya uwakala wa meli?ukijibu swali hilo basi tutaelewa!msomali na nyara=ccm na rushwa
 
WANA JF mnaikumbuka kampuni AMI ilisafirisha drugs nje?ilifungiwa baadae ikasajiliwa SDV TRANSAM.ya kinana vipi?
 
tulisema huyu jamaa kama ninavyowaita ni mshomali ...haya sasa .... hawa jamaa sijui wanayapendea nini meno ya tembo?

huyu si ndiye mmiliki wa Trans Africa Logistics Limited (TALL) moja ya ICD (bandari za nchi kavu) sumbufu sana
 
hapa ndipo huwa inanipelekea niamin kuwa ccm wamekuwa wanaendesha hiz biashara ili wapate fedha za kuendeshea chama, haiingii akilini kila siku maliasilizetu zinakamatwa nchi za nje inamaana china wanauchungu na malisili zetu kuliko hapa kwetu zinapo pakiwa.kwanin hiz nyara zisikamatiwe hapa Tanzania inamaana hapa kunawakaguzi wa madawa ya kulevya na si wa nyara zetu? HII BIASHARA UPO MKONO WA MKUU WA KAYA VASCO DAGAMA SI BURE HUO UOVU UWE UNAENDELEA KWA KASI NAMNA HIYO.
 
Ccm kweli ni janga, yaani serikali yake ina maana haikuweza kugundua UJANGILI kwenye hifadhi, haikuishia hapo hizo pembe zikasafirishwa hadi bandarini still serikali haikugundua, package inafanyika kwenye makontena jamaa hawajui kinachowekwa, mpaka meli inaondoka bado hawakujua! Kufika China tu jama wakabaini mapema! Hapa haya mambo yanafanyika kukiwa na ngao zinazolinda hii mizigo wala tusidanganye mfano mzuri sasa hv biashara kubwa za mkaa zinafanywa na makada wa Ccm kwa kutumia ngao zao!
 
Mkuu KEIKEI,kuna mambo mengine hayahitaji ufahamu mkubwa wa sheria,Kinana kwa jinsi alivyozoea kubwabwaja majukwaani kuombea wanaume kura anafikiri kila kitu ni siasa,kifupi yeye ndo anapaswa kuwajibika kwa sababu ndiye mmiliki wa kampuni,hao anaodai kuwa ni mamlaka inayohusika na ukaguzi hata wakifikishwa mahakamani Charge yao ni rahisi sana kuliko anavyodhani,ni bora akae kimya kuliko kupoteza muda kutoa utetezi wa kitoto namna hiyo kwa sababu naamini ana ufahamu mdogo sana wa sheria.
 
Back
Top Bottom