Kinana acharuka: Adai kampuni ni yake lakini meno ya Tembo si yake!


SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2010
Messages
8,543
Points
2,000
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2010
8,543 2,000
KADA maarufu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema hahusiki na usafirishaji wa meno ya tembo nje ya nchi, ikiwa ni siku moja tu tangu gazeti moja la wiki, lichapishe habari iliyomuelezea kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyosafirisha meno hayo.

Hata hivyo, kada huyo amekiri kuwa mmiliki wa Kampuni ya uwakala wa meli ya Sharaf Shipping Agency, iliyohusika kusafirisha makontena yaliyokuwa na nyara hizo za serikali, kabla ya kukamatwa nchini China yakiwa safarini kupelekekwa Hong Kong.

Gazeti hilo lilimtaja Kinana kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa na hisa 7,500 kati ya 10,000 katika kampuni hiyo, huku hisa nyingine 2,500 zikiwa zinamilikiwa na mshirika mwenzake, Rahma Hussein. Thamani ya hisa hizo ni sh 1,000 kila moja.

Kinana alitoa ufafanuzi huo katika mahojiano maalum na Tanzania Daima.

“Nimeisoma habari hiyo na kwa bahati mbaya sioni anayenilaumu wala kitu ninacholaumiwa nacho. Kwamba nina hisa katika kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf ni kweli.

“Lakini mimi sina nafasi yoyote ya kiutendaji na wala sishughuliki na uendeshaji wa kampuni hiyo. Kwa kweli sikujua na wala sikuhusika kwa namna yoyote ile na usafirishaji wa makontena hayo na mengine yoyote,” alisema Kinana.

Alisema anachojua yeye ni kwamba, maofisa wa kampuni hiyo waliuliza na kuambiwa kuwa shehena iliyokuwa katika makontena hayo ni plastiki zilizotumika.

Alifafanua kuwa, wenye wajibu na mamlaka ya kukagua shehena zote zinazosafirishwa nje ya nchi ni mamlaka za serikali na si kampuni ya uwakala wa meli.

Alisisitiza kuwa, hana mamlaka kwa mujibu wa sheria kukagua mali inayosafirishwa japokuwa anaweza kuuliza bidhaa iliyopo katika makontena hayo.

“Ni dhahiri kabisa kwamba, habari hii imeandikwa na jina langu kutumika katika malengo ambayo siyajui. Nahisi kama jina langu limetumika kama pilipili katika kachumbari ili kunogesha habari.

“Kwa bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa kupasha habari, basi umma umedanganywa,” alisema Kinana.

Kwa mujibu wa habari hiyo, sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali liliibuliwa kwa mara ya kwanza na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, katika Bunge lililopita la bajeti.

Ilidaiwa kuwa, nyaraka hizo zilionyesha kuwa, kilichokuwa ndani ya makontena hayo ni plastiki zilizodurufishwa na baada ya ukaguzi kufanyika, iligundulika kuwa, kilichokuwemo ni pembe za ndovu.

Habari ya gazeti hilo hata hivyo, ilimnukuu ofisa mwandamizi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, akieleza wazi kuwa kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani, wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Source: Tanzania Daima
 
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
7,504
Points
2,000
Kichuguu

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
7,504 2,000
Ingekuwa Marekani huyu jamaa angeshaachia ofisi sababu tu ya kampuni yake ya uwakala kutumika kusafirishia magendo. Hilo ndio jembe la magamba.
General Patreas kaachia ngazi kwa ajili ya nyumba ndogo tu, wala siyo wizi au usafirishaji wa nyara za serikali. Lakini Tanzania sisi ni nchi maskini! hatuwezi kuruhusu maamuzi magumu ya namna hiyo!
 
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,003
Points
1,500
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,003 1,500
hawo ndio viongozi wa CCM
Mwenyekiti anayo Bilali lodge na katibu wake Sharaf Shipping Company. Hongereni
 
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
3,577
Points
1,195
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
3,577 1,195
ccm hata iweje wananhusika na pembe hizo maana haiwezekani kila wakati maneno na pembe za tembo zinakamatwa zinatoka tanzania ingekuwa kwenye nchi za wenzetu alitakiwa kujihudhuru pamoja na mawaziri wahusika wa mali asili. lakini kwa kuwa tuko kwenye nchi yenye giza aka Tanzania ikiwa na weusi katikati ya bendera yake ya taifa kuwafanya wachache waone ukweli uliojificha kwenye hizi biashara za pembe.
 
Mwakalinga Y. R

Mwakalinga Y. R

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2008
Messages
2,717
Points
1,225
Mwakalinga Y. R

Mwakalinga Y. R

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2008
2,717 1,225
Kinana ana mengi zaidi ya hayo. Kama ni kweli amepewa ukatibu mkuu wa CCM ili kuwazibiti kina El tutayajua mengu kuhusu Kinana,subirini picha kamili ianze. Chezea EL....
 
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2010
Messages
8,543
Points
2,000
SHERRIF ARPAIO

SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2010
8,543 2,000
Waria Kinana uzalendo wa vijisenti naona unakushinda
 
H

halimbaya

Member
Joined
Oct 10, 2011
Messages
63
Points
70
H

halimbaya

Member
Joined Oct 10, 2011
63 70
Shughuli ipo huku Wilayani Tunduru, RUVUMA.

Yapata mwezi sasa tangu maofisa wa maliasili kutoka wizarani wakiwa na maaskari wapelelezi zaidi ya magari manne wameweka kambi hapa na wanasachi kila nyumba ya watu wanaojiweza kiuchumi (mabosi wakubwa) wa wilaya hii na kuwatia ndani na masharti ya dhamana yamekuwa magumu mno!

Watu wengi hasa wale wenye pesa waliokuwa wakijihusisha na hii biashara wemekimbia mji, maduka mengi yanafungwa na sasa wameanza kukamata na madereva taxi na bodaboda wanaohusishwa na usafirishaji wa meno toka porini! Kuna upelelezi mkubwa ulifanyika kabla
 
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined
Dec 22, 2010
Messages
16,656
Points
2,000
Yericko Nyerere

Yericko Nyerere

Verified Member
Joined Dec 22, 2010
16,656 2,000
Inaitwa ccm, ina kila aina ya maovu, umafia yenyewe, ujangiri yenyewe, wizi yenyewe, yani kila aina ya maovu duniani basi wahusika ni wanaccm kwani upinzani hatuwasiki wakihusika ama kusingiziwa?!
 
A

Astalavister

Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
5
Points
0
A

Astalavister

Member
Joined Feb 28, 2012
5 0
Ingekuwa Marekani huyu jamaa angeshaachia ofisi sababu tu ya kampuni yake ya uwakala kutumika kusafirishia magendo. Hilo ndio jembe la magamba.
acha uongo,,hiyo kampuni haikagui mizigo,,lazima uwe muelewa ebu toa ushahidi wa hiyo kampuni ya Malekani
 
Amiliki

Amiliki

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Messages
2,085
Points
1,195
Amiliki

Amiliki

JF-Expert Member
Joined May 6, 2011
2,085 1,195
Sasa hapa kazi ya Wakala ni nini! Kama unashindwa kujua unachokwenda kukisafirisha, ina maana kuna siku utabebeshwa hata silaha au madawa ya kulevya na wewe unapeleka kichwa kichwa kukipakia kwenye meli ya watu! Hapa tusidanganyane, Wakala anapaswa kujua aina ya mzigo anaousafirisha ili aweze kutoa tozo sahihi kwa thamani ya kinachosafirishwa kwa mteja, na pia Insurance ya kinachosafirishwa vyote vinatakiwa viwe chini ya Wakala. Kama Wakala hujui unachokisafirisha maana ya kuwepo Insurance ya mizigo inayosafirishwa ni nini? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba umetumiwa kukwepa kodi ya TRA kwa kushiriki Uongo wa mteja kuidanganya TRA. Tusidanganyane, kwenye issue hii Kinana asijitoe anahusika moja kwa moja.
 
Amiliki

Amiliki

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Messages
2,085
Points
1,195
Amiliki

Amiliki

JF-Expert Member
Joined May 6, 2011
2,085 1,195
Sasa hapa kazi ya Wakala ni nini! Kama unashindwa kujua unachokwenda kukisafirisha, ina maana kuna siku utabebeshwa hata silaha au madawa ya kulevya na wewe unapeleka kichwa kichwa kukipakia kwenye meli ya watu! Hapa tusidanganyane, Wakala anapaswa kujua aina ya mzigo anaousafirisha ili aweze kutoa tozo sahihi kwa thamani ya kinachosafirishwa kwa mteja, na pia Insurance ya kinachosafirishwa vyote vinatakiwa viwe chini ya Wakala. Kama Wakala hujui unachokisafirisha maana ya kuwepo Insurance ya mizigo inayosafirishwa ni nini? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba umetumiwa kukwepa kodi ya TRA kwa kushiriki Uongo wa mteja kuidanganya TRA. Tusidanganyane, kwenye issue hii Kinana asijitoe anahusika moja kwa moja. Alipaswa ajue ukweli wa anachokisafirisha.
 
K

KEIKEI

Member
Joined
Jun 17, 2009
Messages
24
Points
0
K

KEIKEI

Member
Joined Jun 17, 2009
24 0
Yale yale ya Muhando na mke wake pale Tanesco! Nchii hii suala la maadili ni janga la kitaifa, Kinana haoni aibu kusimama na kutoa utetezi huu dhaifu! Kampuni ni yake na hivyo anabeba dhamana kwa kashfa zote zinazohussu hiyo kampuni.
 

Forum statistics

Threads 1,283,751
Members 493,810
Posts 30,799,802
Top