Kinana acharuka: Adai kampuni ni yake lakini meno ya Tembo si yake!

Kwa sisi tuliowahi kuakaa sehemu karibu na hifadhi tunajua tembo huwakimbia wasomali, what a coincidence! Kinana msomali
 
Hiki chama jamani ni zaidi ya tukijuavyo,ni chama cha maovu yote ya duniani.Hiyo ndio CCM na hao ndio viongozi wa CCM wanaoaminika ndani ya CCM.
 
acha uongo,,hiyo kampuni haikagui mizigo,,lazima uwe muelewa ebu toa ushahidi wa hiyo kampuni ya Malekani
Wewe lazima tumbo lako litakuwa bovu!unapinga ukweli kwa kupachika uongo,eti nitajie hiyo kampuni ya marekani!!!wapi ameandika kuhusu kampuni ya marekani?kapige jaramba facebook kwanza,hujapevuka bado.
 
Aloo sasa ni dhahiri wanyama wetu wamekwisha!
Fisi kakabidhiwa bucha
 
Swali la uchokonozi

Kuna tatizo hata moja linalowasumbua watanzania ambalo halina uhusiano na ufisadi?
 
Utajiri wa kuweza kumiliki meli kaupata wapi?

kwani anamiliki meli?!!!

"Kwa bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa kupasha habari, basi umma umedanganywa,"

CHADEM MNAMUOGOPA KINANA KWA KUWA NI KICHWA,ATAWATESA SANA KAMA NAPE TU ALIWATOA JASHO ITAKUA HUYU MSOMI WA HAVARD BINGWA WA KUJENGA HOJA NA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU LAKINI ZENYE MADHARA KWA WAPINZANI?
 
...alikuja kwa upole akitaka msamaha, aloyafanya jana hakukumbuka jama! pema si japo pema, hata ukipema si pema tena, nataka kuwa nae ila naogopa kuwa nae, moyo wangu wa chuma umejenga kutu...!
 
General Patreas kaachia ngazi kwa ajili ya nyumba ndogo tu, wala siyo wizi au usafirishaji wa nyara za serikali. Lakini Tanzania sisi ni nchi maskini! hatuwezi kuruhusu maamuzi magumu ya namna hiyo!

Umasikini na kuwajibika kuna relate vipi?
 
Ingekuwa Marekani huyu jamaa angeshaachia ofisi sababu tu ya kampuni yake ya uwakala kutumika kusafirishia magendo. Hilo ndio jembe la magamba.

kweli mkuu!kule kwenye mwanga wangemmulika na angeachia madaraka.tatizo huku gizan wote hatuna tochi za kumulika..we have to take risk tuweke utawala mpya!unsuccesfull men are those who can never take risk!
 
Tatizo la kufanya kazi huku ukiangalia hii ni kampuni/wakala wa nani? Wakisikia ni kmpuni ya mkubwa fulani basi hata taratibu zinakiukwa.....sijui wanatishwa?.....je mara ngapi wamefanya hivyo? Tanzania bwana........!!!!!!!
Ni kweli kabisa wakala wa ukaguzi wa mizigo ndio wa kulaumiwa na si wakala wa kusafirisha mizigo!
 
mpiga kura peke yake ndo msafi aliyebaki CCM!

Wasiwasi wangu ni kuwa hata mpiga kura sio msafi maana analazimishwa kupiga kura kwa pilau, ama kijikofia ama kijifulana kama sio kijiupande cha khanga...! CCM imeharibu kabisa nchi aisee.

Huyu Kinana analazimisha kukanusha ukweli ambao sio ajabu watoa taarifa wana kumbukumbu zote, eti ndio anaonekana ni kiongozi makini wa CCM anayeweza kuwabana mafisadi waliomo ndani na nje ya CCM. Kama Kinana ndio anaonekana msafi pamoja na uozo huu wote, nani atakuwa mchafu sasa huko CCM?
 
mie naliona hili jambo kihivi: je kwa nini kampuni ya kinana itumike? Je kama mwenye mamlaka ya kukagua ni TRA, Je TRA anaweza na anajiamini kukagua mzigo wa namna hiyo (pembe za ndovu) ambao unasafirishwa kupitia kampuni ya Kinana? huu ni ujinga au sheria ya ajabu kuwa kampuni ya usafirishaji ina mamlaka ya kuuliza tu kuwa huu ni mzigo gani na ikijibiwa ni viazi,matango basi inatosha na haina mamlaka ya kukagua, je nauliza kama haina mamlaka ya kukagua kuwa inasafirisha nini sasa kwa nini hii kampuni ya usafirishaji iulize huu ni mzigo gani wakati haina mamlaka ya lolote, kwa sasa iulize? Jamani hapana Kinana anahusika!
 
Kichuguu, Gen. Petraeus kaachia ngazi kwa sababu ya kimada si kwamba amezini nae ila walikuwa wanatumiana e-mail hazina maadili kama mume wa mtu na yule kama mke wa mtu. That was all. Huyu kampuni yake imehusishwa na deal kama hii anasema hahusiki..nani kasema anahusika? Issue hapa Kampuni yako imetumika kusafirishia meno ya tembo. Na hii ni mara ya pili, kampuni ya Kinana kuhusika na hii kashfa so kuna walakini hapa. CCM inaifilisi nchi.
 
Ngongo hebu njoo hapa maana wewe ni wa Arusha naona watu wanapoteza muda bure kuhusu Kinana, wape data za ufisadi wa Kinana hawa wanaopoteza muda wao.
 
Last edited by a moderator:
Kinana is not clean as you may think. Kama kweli integrity yake ni ya juu, huwezi kuwa mdau kwenye kampuni inayokwepa kodi na kila mara kushiriki kwenye usafirishaji wa vitu haramu. Kwenye nchi zilizoendelea, the fact kwamba kampuni yako imehusika kwenye kashfa kubwa kama hivyo, huwezi kuwa na madaraka ya chama au umma.
 
Sasa hapa kazi ya Wakala ni nini! Kama unashindwa kujua unachokwenda kukisafirisha, ina maana kuna siku utabebeshwa hata silaha au madawa ya kulevya na wewe unapeleka kichwa kichwa kukipakia kwenye meli ya watu! Hapa tusidanganyane, Wakala anapaswa kujua aina ya mzigo anaousafirisha ili aweze kutoa tozo sahihi kwa thamani ya kinachosafirishwa kwa mteja, na pia Insurance ya kinachosafirishwa vyote vinatakiwa viwe chini ya Wakala. Kama Wakala hujui unachokisafirisha maana ya kuwepo Insurance ya mizigo inayosafirishwa ni nini? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba umetumiwa kukwepa kodi ya TRA kwa kushiriki Uongo wa mteja kuidanganya TRA. Tusidanganyane, kwenye issue hii Kinana asijitoe anahusika moja kwa moja.

Asante kwa kuiweka hii kitu katika professional terms huyu mwizi anahusika moja kwa moja.Hapa kwa watu wenye idea na shipping & port operations plus clearing & forwarding labda atafute uongo mwingine lakini kwa huu hampati mtu.Mzigo ni wake huu na alijua risk zote zinazohusika ndio maana ni dhahiri kuna procedures zimerukwa hapa tena kwa makusudi(kama ametumia kampuni yake kwa navyomjua huyu mtu ni 'smart' sana bilashaka alishajaribu hii kitu kupitia makampuni mengine na akaona system ina loopholes so sio kontena la kwanza au la pili) na kwa ushirikiano wa kampuni zaidi ya moja na taasisi za serikali.Kwa upande wa pili ya shilingi inawezekana zigo sio lake ila amecharge rate za juu sana kwa mteja ili kufunika madhambi kupitia influence yake aliyonayo kwenye 'system'.
 
Sasa hapa kazi ya Wakala ni nini! Kama unashindwa kujua unachokwenda kukisafirisha, ina maana kuna siku utabebeshwa hata silaha au madawa ya kulevya na wewe unapeleka kichwa kichwa kukipakia kwenye meli ya watu! Hapa tusidanganyane, Wakala anapaswa kujua aina ya mzigo anaousafirisha ili aweze kutoa tozo sahihi kwa thamani ya kinachosafirishwa kwa mteja, na pia Insurance ya kinachosafirishwa vyote vinatakiwa viwe chini ya Wakala. Kama Wakala hujui unachokisafirisha maana ya kuwepo Insurance ya mizigo inayosafirishwa ni nini? Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba umetumiwa kukwepa kodi ya TRA kwa kushiriki Uongo wa mteja kuidanganya TRA. Tusidanganyane, kwenye issue hii Kinana asijitoe anahusika moja kwa moja.

Nimekugongea ' Like ' ! Umemaliza kila kitu ,mimi sichangii tena !
 
Back
Top Bottom