Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
[video=youtube_share;J_3Y2TNSTb0]http://youtu.be/J_3Y2TNSTb0[/video]
Yaliyotokea Zanzibar leo na yale yanayoendelea ni matokeo ya kushindwa kwa utawala wa CCM kutatua matatizo ya Muungano. Lakini pia ni ishara ya kushindwa kwa viongozi wetu wa kisiasa nchini kuutetea Muungano na kujenga hoja za kwanini yapaswa uendelee. Kwa muda mrefu kikundi cha watu wachache kimekuwe kikisukumiza hoja dhidi ya Muungano na baadhi yao kuzawadiwa nafasi za uongozi licha ya msimamo wao juu ya Muungano kujulikana. Hivyo siku baada ya Muungani (A Day After the Union) itakapofika siyo Wananchi wa kawaida watakaolalamikiwa bali viongozi wale ambao wameacha siku hiyo ifike. Ukimya wa Wazanzibari wenye kuamini katika Muungano kumewachochea kundi hilo dogo. Tusije kushangaa tunashuhudia kuzaliwa kwa kikundi cha "Boko Haram" cha Tanzania!!! Yote yatakuwa ni kwa sababu ya kushindwa kwa utawala wa CCM kutoa uongozi!
Hatujasikia viongozi wa CCM wakitetea Muungano kama wanavyotetea chama chao; hatujawasikia wakiwapinga anti-unionists kwa hoja zenye nguvu bali wamekuwa wakiwapa baraza huru; na hatujawaona hata viongozi wao wa serikali - walioapa kulinda Katiba ya Muungano - wakitetea Muungano huo.
Ni kana kwamba wameshakubali kisichoepukika - kufa kwa Muungano. Sasa, kama hili ndilo wanalolitaka hakuna haja ya kuumizana, kupigana mabomu, wala kushindana. Kama kuvunjika kwa Muungano ni inevitable - basi hekima inatutaka tuweke mfumo wa kuvunja Muungano huu vizuri na kwa makusudi ili mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi mbili yaanze. Jamani, Muungano uwepo au usikuwepo watu wa Zanzibar hawaendi popote na watu wa bara hawaendi popote. Hata watu waombee vipi Wazanzibar wataendelea kuwepo na watu wa bara wataendelea kuwepo. Sasa kama hii ni kweli basi ni kushindwa tu kwa viongozi wetu na hasa kushindwa kwa sera zao mbovu ndiko kunakofanya mgogoro huu uwe mkubwa kuliko inavyopaswa.
Tusizungushe maneno! Kuvunjika kwa Muungano kutakuja si kwa sababu ya Uamsho au vikundi vya kidini; kutakuja kwa sababu wanasiasa wetu wameshindwa!
Let me be very blunt: Ajenda ya kisiasa ya Zanzibar sasa hivi inaendeshwa na watu wa CUF; wana CCM Zanzibar wamefyata mkia. hawawezi kuwapinga CUF bila kuonekana "hawaitakii mema Zanzibar" na wale wanaoamini katika Muungano hawana ujasiri wa kuwapinga hawa wengine. CUF ndio wanaendesha siasa za Zanzibar sasa.Tumeona katika jaribio lao la kuwapiga marufuku watu wa bara kufanya kazi Zanzibar. CCM imedhoofika siyo bara tu bali hadi Zanzibar!