Kinachotokea Siku ile mtu anavyochukuliwa MSUKULE

Inakuwaje ndani ya familia au ukoo ni vigumu kuwajua wachawi hata kama ni mzazi wako ila nje ya familia inakuwa inajulikana mji ule au ukoo ule ni wa walozi? Je, ni kitu gani unaweza kufanya kujua mzazi au ndugu wa karibu ni mchawi? na je, inawezekana mchawi kumchukua msukule mtoto wake mwenyewe wa kumzaa? mwisho nini kina wa motivate watu kufanya uchawi au ushirikina?​
 
Je naruhusiwa kufanya nae mapenzi msukule kama Mimi ni boss wake
 
Iko hivi, kuna level ya uchawi unaweza kuua mtu kabisa akafa kabisa, yaani sio kumuweka Msukule bali kumuua kama vile jambazi anavyoamua kuua mtu si unakufa kabisa? sasa katika uchawi kuna uchawi wa kuua kabisa ukafa.

Ikiwa msukule amechukuliwa kwa lengo la kuliwa nyama basi ikifika siku ya 40 huchinjwa kama kuku na huliwa nyama yake na hapo hufariki kabisa. Ni kama vile katika ulimwngu wa nuru kuna watu wanauwana kabisa kabisa mtu anamchinja mwenzake au kumpiga risasi.

Sasa roho hizi huwa zinakwenda wapi?

Inasadikika roho za watu waliodhulumiwa maisha hugeuka kua mizimu. Mzimu ni nishati (energy), roho au haiba (personality) ya mtu ambaye amefariki dunia lakini Roho yake imekwama katika sehemu iliyo kati ya duniani (ulimwengu wa dunia) na mahali ambapo roho hiyo inatakiwa kwenda kuishi baada ya maisha ya hapa duniani kukamilika (ulimwengu usio onekana/ afterlife/ land of the souls).

Katika imani ya kiislamu wale waliokufa katika kutetea dini ya MUNGU hawaitwi ni wafu bali wanaitwa ni wazima au 'Mashahidi' yaani roho zao bado zinaishi.

Katika dini za asili inaaminika kwamba Roho hizi zinakuwa hazijui kama zimekufa katika ulimwengu wa dunia ama hazitaki kuamini kama zimekufa katika ulimwengu wa dunia ama hazikubaliani na kifo chao katika ulimwengu wa dunia. Mara nyingi roho hizi huwa ni roho za watu ambao walikufa katika mazingira yanayo tatanisha kama vile kufa kwa kuuliwa bila sababu (cold blood), kutolewa kafara, ama kufa baada ya maisha ya msukuleni. Kwa ufupi hizi huwa ni roho za watu ambao walidhulumiwa haki yao ya kuishi hapa duniani. Sasa roho hizo hugeuka kua mizimu. Na ndio zitasimama na aliyemuua mbele ya MUNGU siku ya malipo.
 
Nilikua nasoma uzi huku nikijua lazima utie timu boss ,mikononi mwako hii boti ya wachawi nadhani ipo salama
 
Aiseeh
 
Doh inatisha aseeh! Nngekuwa mm nachukua tu pisi kali naish nayo kiroho saf ya nn nianze kujisumbua na misukule khaa! Anyway Mungu atulinde san.
 
...Una Uzoefu Gani ? Uliishawahi Kuchukuliwa ?...
 
Hicho chumba anachofichwa ikatokea mtu asiye mchawi akaingia kwa bahati mbaya je, anaweza akawaona hao msukule kwa macho ya nyama?
 
daaah aisee....hatari sana🙌🙌🙌
 
Nina maswali mengi sana juu ya uchawi na wachawi, ila nianze na haya: Nini kinamsukuma na kumsababisha mtu kuwa mchawi? Wachawi wanapata faida (na hasara) gani kutokana na uchawi? Maana maeneo ambayo uchawi umekithiri ndio na umaskini nao umetamalaki!
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…